Najuta kuoa Single mother, kila nikimtazama huyu mtoto wake Moyo wangu Unaumia kwa machungu makali. Nahitaji msaada

Najuta kuoa Single mother, kila nikimtazama huyu mtoto wake Moyo wangu Unaumia kwa machungu makali. Nahitaji msaada

Sema tu umemla mtoto wa watu umemchoka. Hana tena jipya kwako. Huenda haibani tena kama zamani. Unatafuta kisingizio umteme.
 
WanaJF
Habari zenu, heri ya Ramadan na Kwaresma, matumaini yangu wote wazima, waliyo na changamoto Mungu akawape njia.

Ni kijana barubaru wa miaka 28 mwenye nguvu na Afya.

Wakuu kama kichwa Cha habari hapo juu kinavyo jieleza, nilioa huyu single mother mwaka mmoja uliyo pita baada ya kujiridhisha tabia zake zinafaa kuwa mke na mm bila hiyana nikachukua nikaweka ndani, nikatia pamba maskioni kuzuia kelele za "KUOGOPA SINGLE MOTHER" kumbe nilikua najidanganya nafasi yangu.

Wakuu kila kukicha nikimtazama huyu mtoto wake Roho yangu inauma kwa uchungu wa majuto ya kuoa huyu single mother ni kama nilirogwa hivi kuoa huyu mwanamke, kivipi yaani natunza mbegu za mwanaume mwingine naye yupo tu anakula Bata at the end mtoto aje kunikana mimi siyo baba yake, kwanini hata sikuchukua mdogo wangu nikae naye , kuliko kuhudumia damu ambayo siyo yangu. Wakuu najuta sana.

Niwe Mkweli nafsi yangu inajuta sana. Nahitaji msaada wa kisaikolojia nijinasue kutoka hapa nilipo kwama, imefika hatua hata kukaa nyumban siwezi kabsa.
Pia naomba wale waliyo wai pitia hii situation walijinasuaje? Mnisaidie.
Tunza tu baba yake nipo hapa nitawaita waje tujue maendeleo ndani na nje ya mkeo
 
Serious hiyo ni roho mbaya mtoto kafanya nin? Malaika asiyejua A au B amekukosea nin? Hajawah saidia watoto yatima? Watoto wa mtaan je?? Ingekua huyo mwanamke anamawasiliano na mzaz mwenzake bas iyo ni mbaya
Huyo Malaika si ana Baba Yake?
 
To yeye umesikia anavyosema mwenzio? Yaan pamoja na kuoa singomaza bado anakwea mnazi kwa mkono mmoja
you have a problem somewhere, unapata wapi mda wa kufukunyua thread ya two years ago? Na huyo niliyemuombea ushauri he was my young Bro.

Mkuu tafadhari stay aside this's serious issue nahitaji msaada zaidi ya hichi unacho fanya.
 
Kwenye maelezo yako hujasema kama mtoto anakupa shida yoyote. Anakudharau au anakuwekea kiburi? Kama yupo vizuri mi naona shida kubwa ipo kwako wewe.
 
Kwenye maelezo yako hujasema kama mtoto anakupa shida yoyote. Anakudharau au anakuwekea kiburi? Kama yupo vizuri mi naona shida kubwa ipo kwako wewe.
Nafsi mkuu haikubali.....hasa pale unakuta Dogo anaumwa hamjalala usiku kucha. Ila unasikia Baba yake jana alikuwa kalewa anagombana na Bar Maid.

Lakini Mtoto anaitwa kwa jina la mlevi sio lako wewe unayehustle.
 
Ili kweje? Kwani kukomoana?
Huyo mtoto wa kambo akipata dada zake na wadogo zake watamuita kaka/dada, tayari umetengeneza bond kati ya damu yako na damu isiyokuhusu. Inasaidia kuondoa chuki za kishamba.
 
Back
Top Bottom