Najuta kuwekeza kwenye kiwanja na nyumba ya mwanamke

Najuta kuwekeza kwenye kiwanja na nyumba ya mwanamke

Hii kitu inaanza kuniingia kwenye akili polepole, NDOA INAFUNGA MAWAZO YA KIUTAFITI NA KUWAZA KWA MAPANA NA MAREFU ZAIDI, Mwenye ndoa anafungika mawazo na kubakia na mawazo ya kulisha kusomesha makazi bora na vya aina hii, huwazi tena vya kiuvumbuzi na kiutafiti, chunguza wavumbuzi wengi na watafiti hapo zamani walijifungia katika LABS, kuona wanafacilitate future.
kabisa kabisa , mwanaume ukitaka kuua ndoto zako wewe oa

hapo mwendo umeumaliza, kwisha habari yako kabisa
 
View attachment 2543623
Good
Tazama hiyo[emoji1369]
Huyu alieandika ni mwanamke [emoji16]
Yuko sawa kwa 100% ,japo maneno yake yanaweza kua yanachoma ila ndio ukweli

Thus me sijawah kufikilia kuowa mwanamke mwenye fedha au anaejiweza
Pengine IKAPUNGUZA ng’ong’oso

Make sure una kibunda+ maendelea

A place to call home

2 USITUMIE HISIA!
3TUMIA AKILI.
Unaweza ukawa na hivyo vyote na ukapelekeshwa vilevile. Omba upate mwanamke mwenye hekima regadless ya kipato chake.
 
Mkeo sio ndugu yako, wala sio mamako mzazi, ni mwanamke mmoja tu ambae hawez kukuletea miyeyusho, ni mamako mzazi baaaasi, wanawake ni opportunist mzee, katembea na gap...wanawake kila kitu kwao ni kamari yan wako hivyo usiwazingatie saaaaana watakuumiza...
Kumbuka kwamba mkeo ni mama mzazi wa wanao. Wewe shupaza kichwa halafu siku wanao wakikugeuka hauna rangi utaiona.
 
Umri wako haujakusaidia kutambua kuwa hela ya mwanamke ni ya mwanamke tu? Mwanamke akinunua kitu kwa ajili ya familia inatakiwa iwe labda ni kitu cha kula amekutana nacho kinauzwa akakipenda.
 
Biblia Takatifu imesema tuishi nao kwa akili, haikumaanisha michepuko, ilimaanisha wake zetu tena tuliofunga nao ndoa.

Mwanamke hata achangie chakula nyumbani kea wiki moja lazima atakubadilikia tu ni wachache sana watakubaliana na hali

Kushindwa kwako kutumia akili vizuri haihalalashi kuwa ndoa haifai.

Kuna sifa za mke wa kuoa, sasa Kama ukatizama uzuri ukaacha tabia unategemea nini?

Hii campaign ya KATAA NDOA, INAMAANA WANAUME WAMESHINDWA KUWA WANAUME, NA KAMA WANAUME WAMESHINDWA KUWA WANAUME, WANATAKA KUWA NINI?
 
Kwamba kwa sababu magari yanapata sana ajali basi watu wasipande magari?

Kwamba kwa sababu vyakula vimepanda bei basi watu wasile.

Wakuu, hii campaign nyuma ipo LGBT..., nasema ukweli, kwamba binadamu kasahau Mungu katuleta hapa duniani na katupa mwongozo.
 
Ila za wanawake sio za kupigia hesabu otherwise ziwe chini yako yaani atoe aweke mezani mjue Cha kufanya Kwa pamoja
Afadhali wew alikushirikisha kununua kiwanja kunawenzio wakezao Wana nyumba Hadi 3 za maana na waume hawajui
Mimi ndo nlimpa wazo la kununua kiwanja mara tu alipoajiriwa so nikamwambia nenda kakope hela kidogo utafute kiwanja then kujenga tutasaidiana mdogo mdogo maana tayari tumeanzisha familia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umejua Leo kaka?,hii ni asili yao Cha msingi ni kuwa unapokuwa kwenye ndoa hakikisha una kuwa na upeo mkubwa wa kutambua kuwa wao wako hivo na walau uwe na sehemu tofauti tofauti za kuishi ikitokea la kutokea una kuwa salama maana ni kiasi Cha kuamia sehemu nyingine na maisha yanaendelea.Vinginevyo unaweza fukuzwa Kama mbwa hawa hawanaga kufikili mlianzaje maisha ,wanaangalia kile kilichopo kwa wakati huo.Nina classmate wangu alikimbia mji wake apo dar.
Wana MMU,

Naandika huu uzi kwa masikitiko na kujuta bora ile pesa ningenywea tu bia na kula kitimoto.

Nina mke na watoto, mke alikopa hela bank na kazini kwao akanunua uwanja. Ushauri huu nilimpa mimi

Nikasimamia ujenzi nyumba ikasimama ingawa kuna vitu vilikuwa havijakamilika nikaanza kuingia gharama kumalizia nyumba.

Kipato changu cha kuunga unga ila kwa kutambua nyumba ni ya familia tuna watoto na ndoa tumefunga nikaona niendeleze ukarabati.

Sasa bwana umetokea mgogoro mdogo mimi na mke wangu kanitamkia hapa sijachangia chochote kodi yote anakula yeye.

Basi nimeamua nianze mdogo mdogo kujitoa kwenye hii nyumba.

Mchango wangu hajauthamini kabisa mwanamke amekua mbinafsi ghafla sana.

Wakuu tuwe makini kuwekeza hela na muda wako kwenye mali ya mwanamke ni kujichimbia kaburi.

KATAA NDOA
NDOA NI UTAPELI
 
Back
Top Bottom