Najuta kuwekeza kwenye kiwanja na nyumba ya mwanamke

Najuta kuwekeza kwenye kiwanja na nyumba ya mwanamke

Wana MMU,

Naandika huu uzi kwa masikitiko na kujuta bora ile pesa ningenywea tu bia na kula kitimoto.

Nina mke na watoto, mke alikopa hela bank na kazini kwao akanunua uwanja. Ushauri huu nilimpa mimi

Nikasimamia ujenzi nyumba ikasimama ingawa kuna vitu vilikuwa havijakamilika nikaanza kuingia gharama kumalizia nyumba.

Kipato changu cha kuunga unga ila kwa kutambua nyumba ni ya familia tuna watoto na ndoa tumefunga nikaona niendeleze ukarabati.

Sasa bwana umetokea mgogoro mdogo mimi na mke wangu kanitamkia hapa sijachangia chochote kodi yote anakula yeye.

Basi nimeamua nianze mdogo mdogo kujitoa kwenye hii nyumba.

Mchango wangu hajauthamini kabisa mwanamke amekua mbinafsi ghafla sana.

Wakuu tuwe makini kuwekeza hela na muda wako kwenye mali ya mwanamke ni kujichimbia kaburi.

KATAA NDOA
NDOA NI UTAPELI
Wee lengo lako Ni kukata ndoano

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Msiachane, huo ni upepo tu umepita; unaweza kutafuta part time/mchepuko wa kukuweka bize pale mtakapo tofautiana na mwenzio, ila usivinje ndoa.
Hiki kitu sitakuja kuelewa hata siku moja unajua. Yaani unamajukumu na imefikia hatua mwanamke amekupita maarifa amekuzidi kiuwezo mithili ya kukudharau lakini unalazimisha kuongeza mzigo mwingine ambapo utajiharibia ustawi wa maendeleo yako tena kwakitendo cha muda mfupi tu[emoji23][emoji23]. Sijui wanaume wengine, ila kama ikitokea nimefikia hatua hiyo my devotion is to work 2407. You put value into pleasures more than your life duh! Sijui ila nafikiri wanaume wengi kipindi cha ubachela hatuwezi kuishi peke yetu kila muda kubadilisha mwanamke ila kama ulizoea kukaa mwenyewe hata itokee nini maisha ya upeke yako yana amani sana, ninachohitaji ni pumzi na baraka za Mwenyezi Mungu ili nijitume kufika nitakapo.
 
Mkuu kiwanja aliandika jina lake maana yeye ndo alikopa hela ya kununua mimi nimechangia kwenye ujenzi lakini leo hii ananiambia sijachangia chochote hela yote ya kodi za wapangaji anakula pekeake so sitaki kuforce umiliki ila inaniuma tu pesa zangu nlizotupa hapa bora ningeenda kutafuta kiwanja changu hata kijijini huko
Nenda mahakamani kaombe mgawane mali🤔
 
Muulize Mama yako maana aliolewa na Baba yako wewe ndo ukazaliwe, umkosoe na yeye
Mada kama hizi, tena za mtandaoni kuingiza na kutukaniana wazazi ni utoto na kutokuwa na heshima. Sasa mama anaingizwa hapo ili iweje, tunawatukana wazazi bure bila sababu za msingi ili uonekane mshindi. Aisee!
 
Hiki kitu sitakuja kuelewa hata siku moja unajua. Yaani unamajukumu na imefikia hatua mwanamke amekupita maarifa amekuzidi kiuwezo mithili ya kukudharau lakini unalazimisha kuongeza mzigo mwingine ambapo utajiharibia ustawi wa maendeleo yako tena kwakitendo cha muda mfupi tu[emoji23][emoji23]. Sijui wanaume wengine, ila kama ikitokea nimefikia hatua hiyo my devotion is to work 2407. You put value into pleasures more than your life duh! Sijui ila nafikiri wanaume wengi kipindi cha ubachela hatuwezi kuishi peke yetu kila muda kubadilisha mwanamke ila kama ulizoea kukaa mwenyewe hata itokee nini maisha ya upeke yako yana amani sana, ninachohitaji ni pumzi na baraka za Mwenyezi Mungu ili nijitume kufika nitakapo.
Kuna hatua utafikia, kichwa cha chini kitakuwa kinasumbua kutaka kumuona mwenzake, sasa kama mama watoto hataki, utakimbilia wapi, au utakamata kuku?
 
Ila za wanawake sio za kupigia hesabu otherwise ziwe chini yako yaani atoe aweke mezani mjue Cha kufanya Kwa pamoja
Afadhali wew alikushirikisha kununua kiwanja kunawenzio wakezao Wana nyumba Hadi 3 za maana na waume hawajui
 
Kuna hatua utafikia, kichwa cha chini kitakuwa kinasumbua kutaka kumuona mwenzake, sasa kama mama watoto hataki, utakimbilia wapi, au utakamata kuku?
Ndio maana nikakwambia tunatofautiana hata mimi nawashangaa, nikiwa katika majukumu yaani hata hicho kichwa cha chini kama hakipo vile sembuse nikidharauliwa hivyo. Nimeishi miaka 25 bila kumjua mwanamke sembuse kukaa miezi kadhaa au mwaka 1 au 2 kujijenga. Mahusiano yenyewe nilijaribu mara 3 nayote ni stress tupu sasa sijui mtu kwanini ukimbilie vimada nahuku tayari unabomu lililolipuka ndani, yaani I just don't get it. Tamaa kama ulizoea kuzicontrol kamwe hazitakuendesha, ndiyo maana nikasema kipindi cha ubachela tunakuwaga tunaruka sana ili tu usibaki mpweke, ila kama ulishazoea, hamnaga shida.
 
[emoji419][emoji419][emoji419]Bila kusahau sauti iwe ya kiume ukifanya maamuz otherwise ni majanga
Shikamoo! Unajua kuwa mwanaume akifanya yote hayo katika kizazi hiki anatafsiriwa kuwa ni muonezi na mbabe. Mwanamke msomi hajaweza kujua anahitaji nini, ukileta full masculinity traits atalia kwa jamii kuwa unamuonea na ni mbabe pia humpendi. Pia ukiishi kistaarabu in the equilibrium anakuona fala na anaona kuwa wewe ni shoga yake. So hamuelewekagi!
 
Inabidi iwe hivo otherwise ni majanga
 
Back
Top Bottom