NAJUTA SANA: Nilizaa nje ya ndoa, mke wangu haniamini tena. Natamani siku zirudi nyuma

Inauma sana ila kusamehewa ndio kazi bro ila yameshamwagika hayazoleki jaribu kumwambia hivyo akuelewe
 
Huko kujutia na kujidogosha ndo kunakomwongezea credit, maana ni kweli umemwumiza so yeye anakukomesha. GIVE UP, MPOTEZEE.

Pambana na matokeo hayo, jali watoto wako, ilee familia yako kwa ukamilifu, hicho kdg utakachojaliwa ndo chako, usijilinganishe na watu wengine.

Akiona kuna haja ya kurudi kama zamani atakukalisha chini asipoona hivyo ndo inakuwa hivyo hadi mwisho.
 
Habari,
Ngoja nianzia mbali kidogo mpate kuelewa mke wangu ni mtu wa aina gani. Na ilikuwaje mpaka nikazaa nje.

Mimi na mke wangu tulikutana kwenye kongamano la injiri kipindi namaliza chuo yeye alikuwa anasoma chuo kingine tofauti na chetu.

Ni mtu mpole sana niseme ukweli, na anavaa mavazi ya heshima sana, Nilitengeza nae urafiki mpaka kuingia kwenye mahusiano. Niseme ukweli kipindi bado sijamuoa alikuwa ni mtu wa kupenda maendelea sana tena maendeleo ya kushirikiana.

Nilikaa nae kwenye mahusiano kama miaka 6 hivi kisha baadae tukaamua kufunga ndoa takatifu. Nikili kuwa kipindi tupo kwenge uchumba au niseme urafiki nilikuwa sijawahi mgusa kabisa kwani alikuwa ni mtu mpole sana. Mimi nilikuwa na michepuko yangu.

Kipindi tumeanza ndoa yetu, mke wangu yeye wala hakuwa Mchoyo mshahara wake yeye na pesa zake zingine alikuwa anaweka mezani, kitu hiki kilipelekea mpaka mimi kumuamini mke wangu na mimi nikaanza kuweka pesa mezani na kujadili nini cha kufanya tupate maendeleo katika familia yetu itakayokuja.

Mke wangu yeye ni mtu wa kuchakarika sana, na alikuwa anapenda kufanya sana biashara za kushirikiana na mimi mume wake. Kusema ukweli tulikuwa tunainuka kiuchumi kabisa maana nilikuwa naona hali inabadilika katika ndoa yetu hasa kiuchumi,
Nilipanga mengi sana na mke wangu , nilijivunia kuwa nae sana, niliona nimepata, japo ndo kipindi kile ilikuwa still changa.

Sasa baada ya mwaka 1 na miezi 2 mke wangu alibeba ujauzito wangu, ujauzito ule tangu dalili zilipoanza ulikuwa unamsumbua sana mpaka kutafuta mfanyakazi kusaidia kazi. Baada ya miezi kama 4 hivi ya ujauzito, sisi wanaume si unajua bwana kikombe kilijaa maji maana ni miezi kadhaa sijakutana na wife sababu ni ujauzito wangu ule. Nilikuwa navumilia tuu.

Sasa karibu na office yetu kulikuwa na kampuni moja hivi inaagiza vitu china na kuuza, mara nyingi vitu vya home nilikuwa nanunua pale. Kulikuwa na mdada mmoja nilizoeana nae, yeye alikuwa anapokea wageni na kuwaonyesha bidhaa. Kipindi cha ujauzito mazoea yaliongezeka mpaka kubadilisha namba na yule dada. Niseme tu ukweli kuwa niliomba sexy kwake, mimi kwangu kisingizio ni hali ya mke wangu. Nilianza kukutana naye maeneo ya nyumba za wageni tulikuwa tunatumia kinga. Mchezo humu uiliendela mpaka mke wangu anajifungua.

Mimi nikaona mahusiano na mchepuko yameisha tayari kwa sababu mke wangu ashajifungua tayari, nilisitisha mahusiano na mchepuko.
Ila kumbe mke wangu alikuwa anamshono ulitokana na kujifungua . Home na alianza kukalia maji yaliyochanganywa na dettol. Lakini baada ya mwezi mmoja alikuwa still anaumia wakasema anakinyama kimeota kwa hio arudi hospital akashonwe tena, mimi daaa.
Siku namsindikiza hospital nilipanga tena kukutana na mchepuko wangu. Nilivyomuacha hospital mke wangu jioni nilikutana na mchepuko wangu yule kwenye bar moja hivi. Sasa kipindi tunaondoka tukajikuta kunanyanduana kwenye gari kusema ukweli sikutumia kinga kabisa.

Nilimpeleka mpaka sehemu yeye aliposema nimuache, si kujua maisha anayoishi wala kwao sikujui.
Mke wangu baada ya kushonwa tena na kurudi home, mimi niliendelea kukutana na mchepuko kwa mwezi mmoja.
Siku moja aliniambia siku zangu sizione , daaa maneno yale nilishituka sana .
Nikamwambia mimi ni mume wa mtu akasema sawa ila ninahisi ni mjauzito. Mimi daa kusema ukweli hamu naye ilikata kabisa, nikaacha kukuatana nae tena. Nilifikili anatania ila siku zinavyoenda tumbo linatoka nje.

Mke wangu alivyopona tuliendela na maisha huku mchepuko anaujauzito wangu.
Maisha na mke wangu yalikuwa mazuri sana na mafanikio, mchepuko nilikuwa namtumia pesa za kumsaidia tuu, baada ya kujifungua hata mtoto sikwenda kumuona nilikaa kama miezi 5 hivi sikwenda hata kwao.
Mke wangu alikuwa hajui kabisa, mimi na mke wangu tulipanga vingi sana kuhusu maisha yetu, na mafanikio yalikuwa yanatimia kabisa kwani nilikuwa nayaona haya mlangoni na mengine yanangia kabisa.

Siku moja nikasema ngoja nikamuone kwake huko.
Aisee yule dada kumbe anaishi maeneo ya uswazi kabisa , yani ni mtahani kwa waswahili kabisa, waswahili wenyewe wale, nyumba mbanano hata pikipiki haipiti, mimi daa ndo nimezaa na huyu, niliumia sana tena sana ndo mwanzo wa kuanza kujuta, binti anaishi na mama yake tuu, na mama yake ni mswahili kweli kweli, yani hata home wakimuona watanishangaa sana.

Niliondoka na kurudi home namawazo sana huku mke wangu hajui, nilikaa kimya kama 2 years huku maisha na mke wangu yanaendela tukiwa tunakuwa kabisa kimaisha, mke wangu alibeba ujauzito mwingine , sikuchepuka kabisa, alifanikiwa kujifungua.

Baada ya miaka 2 tangu mke wangu ajifungue mtoto wa 2, mtoto wa mchepuko alikuwa miaka 4.

Mimi niliona daa sio vyema mtoto wangu kabisa yule aishi kule kwenye mazingira yale ya mtaani tena uswazi.
Kuna siku moja nilikaa mpaka 3 night kwa niliezaa nae. Daa mazingira ni hovyo sana na kelele nyingine, watu wanapita dirishani wanatukana matusi, maisha ya uswazi mnaelewa jamani.

Mimi niliona ngoja nimshirikishe mother, nipokee ushauri mama aliniambia ni kweli kama mazingira sio mazuri mchukue tuu ila atapata kuzoeana na wenzie mapema. Ila alinisisitiza sana kutengeza kwanza vizuri na mke wangu kuepuka madhara baadae. Niliongea mpaka na viongozi wa dini, kusema ukweli walinikaripia sana kwa sababu ni uzinzi nilifanya. Wakaniambia tuu ni damu yako ongea na mke wako tuu.

Mimi niliamua kwenda kufunguka kwa mke wangu, Nilitanguliza msahama na majuto kwa wife. Niliongea nae sana kuhusu mtoto wa nje na kuacha mahusiano na mama mtoto na ishu ya kumchukua mtoto tukae nae. Mimi sikufukilia madhara yatakayo tokea baadae sikufikilia hilo.
Mke wangu yeye alijibu tuu SAWA HAKUNA SHIDA NI MTOTO WAKO NA ATAENDELA KUWA WAKO TUU.

Kusema ukweli sikufikilia labda mke wangu atapata maumivu kiasi gani mimi nilivyoona yeye kakuabali mimi nikaona sawa. Nimwambia mother akasema kama kakubali sawa mchukue tuu ila kuwa karibu na mtoto.

Baada ya kama wiki nilimchukua mtoto japo mama yake alikuwa mgumu ila nilimchukua, na kuishi nae home.

Ila uwezi amini , ukaribu na mke wangu ulikufa kabisa , si ukaribu wa ndoa. Namaanisha ushirikiano kama Wanandoa.
Kipato chake sikukiona tena , mambo yote tuliokuwa tunashirikiana hasa ya kimaendelo na kiuchumi zilishia kabisa, ndani ya kama mwaka mmoja hivi niliona kipata ndani kimepungua kabisa, nilijua shida ni ile ishu, nilijaribu kukaa na kuongea nae tena sana, yeye anasema kuwa yeye yupo sawa hana shida. Nilijaribu kupambana mimi mwenyewe na maisha ila wapi ni vijipesa vidogo tuu ndo vinaingia ndani na mshahara wa kazini tuu.
Mke wangu yeye yupo na mambo yake haniusishi kabisa mimi.

Sometime nikawa najipa tuu moyo kuwa mimi ndo me ninatakiwa kurisha familia yangu, naamua kusonga mbele ila mambo yanaenda kawaida na mambo yangu mengi wanaanguka, mishe hacienda kabisa.

Natafuta ushauri kwa watu wa ninaokutana nao kwenye bar na sehemu zingine , wengi wanasema tuu ulizingua mara nyingi watoto hao tunawaacha kwa mama zao huko huko, kwani ulivyofanya hivyo umemwonyesha mkeo ushahidi kuwa ulimsaliti tena ukamletea home kabisa ushahidi. Wengi wanasema tuu usaliti unauma sana huyo mkeo anaumia mpaka kesho. Wananiambia tuu potezea kaka.
Ila ni kitu ninakijutia sana sio kwamba ninamchukia mtoto hapana nachukia ule uzinzi nilifanya .
Nilimueleza mother aliniambia tuu kama mtoto anaishi nae fresh hakuna shida kubali matokeo tuu.

Sometime natamani kuona siku zinarudi nyuma ila haiwezekani, Najuta sana maana naona maisha yamedrop sana. Yale maendeleo hakuna kabisa kama awali.

Sasa nina umri wa miaka 42,
Maisha napambana tuu mimi mwenyewe kama Baba wa familia sioni ushirikiano kutoka kwa mke wangu, lakini nimejipa moyo kuwa mimi ndo mwanaume nitalisha familia yangu. Ila kinachoniuma ni mahusiano wa kushirikiana na mke wangu yamekufa kabisa. NAJUTA SANA.

Marafiki zangu wengi wapo na mafanikio sana na wake zao nawaona hata jinsi wanavyoishi.
Kuna rafiki yangu mmoja wa karibu sana mwezi wa 3 aliingiza Toyota land cruiser LC300 GX la kwake na mke wake GX.
Huyu ni mmoja tuu wapo wengine wapo fresh sana , najua wapo hivyo kutokana na mahusiano na wake zao hasa ya kiuchumi.

Mimi hapa ni na ka harrier changu kimetengenezwa miaka 14 iliyopita naona hata aibu kuwakaribisha hata home friends wangu.
Na Hata kukutana nao tuu.

NB; JAMANI WANAUME WENZANGU TUTULIE KWENYE NDOA ZETU HASA TUNAPOPATA MKE MWENYE MIBARAKA KWENYE NDOA ZETU. NI MUHIMU SANA UNAWEZA UKAONA STORY ILA MWENZENU YAMENIKUTA.

SOMETHING NAJIRAUMU KUWA NINGEJUA NINGEMUACHA KWA MAMA YAKE NIKABAKI MUUDUMIA.
SOMETHING NAONA NILIKUWA SAHIHI KUMCHUKUA.

Sorry mimi sio mwandishi mzuri, naomba radhi kwa makosa mtakayo baini.

Mwanamke mkubalie ume cheat endapo tu kakukuta uchi mmelaliana, na vimeingiliana.

Akikukuta uchi na mmelala havijaingiliana wewe goma kwamba asifikirie hivyo, uja cheat.

Wewe unaleta ushahidi home, blal gambush, itakugharimu for the rest of your life.

Mtoto wa nje msomeshe, akue huko huko kwa Mama yake, atazoea uzao wa uswazy maana hajui mwingine.

Omba Mungu, ndo namna pekee ya kurudisha mahusiano na mke wako, umeharibu mwenyewe.
 
Mungu hakupi mtihani au mzigo ambao upo nje ya uwezo wako.

Yatapita na changamoto zipo maishani hata hao marafiki zao sio kwamba wana furaha milele.

Kwa vile ushatambua wapi umekosea basi Mungu anasamehe ,mtoto ni furaha haijalishi na ni kiumbe hakina makosa .

Kwa hiyo Mungu kampa huu Mthihani? Jehovah Mungu uturehemu hata kwa maneno yetu.
 
Eti kuleta mtoto ni vizuri kuliko maradhi..kwa hiyo hapo anatakiwa ashukuru Mungu hakuletewa Ukimwi[emoji1787]

Haki acha tu wababa waendelee kuona kuchepuka hadi kuzaa ni haki yao..sio kwa mentality hii[emoji119]
Na siku yakiwakuta lawama kwa mke, uzuri visasi vya wanawake wanavijua akiamua hakosei

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo Mungu kampa huu Mthihani? Jehovah Mungu uturehemu hata kwa maneno yetu.
Kutmani nje ni mtihani wa wanaume na itabidi kuushinda ndo maana tunaambia tusizini tufanye tuoe.

Hapo kazini nje ya ndoa means mtihani umemshinda ila anaweza kuomba msamaha
 
Mchuma janga hula na wa kwao [emoji23]huyu mke ukute ameshajijengea lijumba walilopanga wajenge nacheka kama mazuri
Huyo alipopata taarifa kalia machozi na ndugu zake wakampa pole, haya dada yetu jipange umeshaanza kuletewa watoto huyo mmoja tu je waliofichwa [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Habari,
Ngoja nianzia mbali kidogo mpate kuelewa mke wangu ni mtu wa aina gani. Na ilikuwaje mpaka nikazaa nje.

Mimi na mke wangu tulikutana kwenye kongamano la injiri kipindi namaliza chuo yeye alikuwa anasoma chuo kingine tofauti na chetu.

Ni mtu mpole sana niseme ukweli, na anavaa mavazi ya heshima sana, Nilitengeza nae urafiki mpaka kuingia kwenye mahusiano. Niseme ukweli kipindi bado sijamuoa alikuwa ni mtu wa kupenda maendelea sana tena maendeleo ya kushirikiana.

Nilikaa nae kwenye mahusiano kama miaka 6 hivi kisha baadae tukaamua kufunga ndoa takatifu. Nikili kuwa kipindi tupo kwenge uchumba au niseme urafiki nilikuwa sijawahi mgusa kabisa kwani alikuwa ni mtu mpole sana. Mimi nilikuwa na michepuko yangu.

Kipindi tumeanza ndoa yetu, mke wangu yeye wala hakuwa Mchoyo mshahara wake yeye na pesa zake zingine alikuwa anaweka mezani, kitu hiki kilipelekea mpaka mimi kumuamini mke wangu na mimi nikaanza kuweka pesa mezani na kujadili nini cha kufanya tupate maendeleo katika familia yetu itakayokuja.

Mke wangu yeye ni mtu wa kuchakarika sana, na alikuwa anapenda kufanya sana biashara za kushirikiana na mimi mume wake. Kusema ukweli tulikuwa tunainuka kiuchumi kabisa maana nilikuwa naona hali inabadilika katika ndoa yetu hasa kiuchumi,
Nilipanga mengi sana na mke wangu , nilijivunia kuwa nae sana, niliona nimepata, japo ndo kipindi kile ilikuwa still changa.

Sasa baada ya mwaka 1 na miezi 2 mke wangu alibeba ujauzito wangu, ujauzito ule tangu dalili zilipoanza ulikuwa unamsumbua sana mpaka kutafuta mfanyakazi kusaidia kazi. Baada ya miezi kama 4 hivi ya ujauzito, sisi wanaume si unajua bwana kikombe kilijaa maji maana ni miezi kadhaa sijakutana na wife sababu ni ujauzito wangu ule. Nilikuwa navumilia tuu.

Sasa karibu na office yetu kulikuwa na kampuni moja hivi inaagiza vitu china na kuuza, mara nyingi vitu vya home nilikuwa nanunua pale. Kulikuwa na mdada mmoja nilizoeana nae, yeye alikuwa anapokea wageni na kuwaonyesha bidhaa. Kipindi cha ujauzito mazoea yaliongezeka mpaka kubadilisha namba na yule dada. Niseme tu ukweli kuwa niliomba sexy kwake, mimi kwangu kisingizio ni hali ya mke wangu. Nilianza kukutana naye maeneo ya nyumba za wageni tulikuwa tunatumia kinga. Mchezo humu uiliendela mpaka mke wangu anajifungua.

Mimi nikaona mahusiano na mchepuko yameisha tayari kwa sababu mke wangu ashajifungua tayari, nilisitisha mahusiano na mchepuko.
Ila kumbe mke wangu alikuwa anamshono ulitokana na kujifungua . Home na alianza kukalia maji yaliyochanganywa na dettol. Lakini baada ya mwezi mmoja alikuwa still anaumia wakasema anakinyama kimeota kwa hio arudi hospital akashonwe tena, mimi daaa.
Siku namsindikiza hospital nilipanga tena kukutana na mchepuko wangu. Nilivyomuacha hospital mke wangu jioni nilikutana na mchepuko wangu yule kwenye bar moja hivi. Sasa kipindi tunaondoka tukajikuta kunanyanduana kwenye gari kusema ukweli sikutumia kinga kabisa.

Nilimpeleka mpaka sehemu yeye aliposema nimuache, si kujua maisha anayoishi wala kwao sikujui.
Mke wangu baada ya kushonwa tena na kurudi home, mimi niliendelea kukutana na mchepuko kwa mwezi mmoja.
Siku moja aliniambia siku zangu sizione , daaa maneno yale nilishituka sana .
Nikamwambia mimi ni mume wa mtu akasema sawa ila ninahisi ni mjauzito. Mimi daa kusema ukweli hamu naye ilikata kabisa, nikaacha kukuatana nae tena. Nilifikili anatania ila siku zinavyoenda tumbo linatoka nje.

Mke wangu alivyopona tuliendela na maisha huku mchepuko anaujauzito wangu.
Maisha na mke wangu yalikuwa mazuri sana na mafanikio, mchepuko nilikuwa namtumia pesa za kumsaidia tuu, baada ya kujifungua hata mtoto sikwenda kumuona nilikaa kama miezi 5 hivi sikwenda hata kwao.
Mke wangu alikuwa hajui kabisa, mimi na mke wangu tulipanga vingi sana kuhusu maisha yetu, na mafanikio yalikuwa yanatimia kabisa kwani nilikuwa nayaona haya mlangoni na mengine yanangia kabisa.

Siku moja nikasema ngoja nikamuone kwake huko.
Aisee yule dada kumbe anaishi maeneo ya uswazi kabisa , yani ni mtahani kwa waswahili kabisa, waswahili wenyewe wale, nyumba mbanano hata pikipiki haipiti, mimi daa ndo nimezaa na huyu, niliumia sana tena sana ndo mwanzo wa kuanza kujuta, binti anaishi na mama yake tuu, na mama yake ni mswahili kweli kweli, yani hata home wakimuona watanishangaa sana.

Niliondoka na kurudi home namawazo sana huku mke wangu hajui, nilikaa kimya kama 2 years huku maisha na mke wangu yanaendela tukiwa tunakuwa kabisa kimaisha, mke wangu alibeba ujauzito mwingine , sikuchepuka kabisa, alifanikiwa kujifungua.

Baada ya miaka 2 tangu mke wangu ajifungue mtoto wa 2, mtoto wa mchepuko alikuwa miaka 4.

Mimi niliona daa sio vyema mtoto wangu kabisa yule aishi kule kwenye mazingira yale ya mtaani tena uswazi.
Kuna siku moja nilikaa mpaka 3 night kwa niliezaa nae. Daa mazingira ni hovyo sana na kelele nyingine, watu wanapita dirishani wanatukana matusi, maisha ya uswazi mnaelewa jamani.

Mimi niliona ngoja nimshirikishe mother, nipokee ushauri mama aliniambia ni kweli kama mazingira sio mazuri mchukue tuu ila atapata kuzoeana na wenzie mapema. Ila alinisisitiza sana kutengeza kwanza vizuri na mke wangu kuepuka madhara baadae. Niliongea mpaka na viongozi wa dini, kusema ukweli walinikaripia sana kwa sababu ni uzinzi nilifanya. Wakaniambia tuu ni damu yako ongea na mke wako tuu.

Mimi niliamua kwenda kufunguka kwa mke wangu, Nilitanguliza msahama na majuto kwa wife. Niliongea nae sana kuhusu mtoto wa nje na kuacha mahusiano na mama mtoto na ishu ya kumchukua mtoto tukae nae. Mimi sikufukilia madhara yatakayo tokea baadae sikufikilia hilo.
Mke wangu yeye alijibu tuu SAWA HAKUNA SHIDA NI MTOTO WAKO NA ATAENDELA KUWA WAKO TUU.

Kusema ukweli sikufikilia labda mke wangu atapata maumivu kiasi gani mimi nilivyoona yeye kakuabali mimi nikaona sawa. Nimwambia mother akasema kama kakubali sawa mchukue tuu ila kuwa karibu na mtoto.

Baada ya kama wiki nilimchukua mtoto japo mama yake alikuwa mgumu ila nilimchukua, na kuishi nae home.

Ila uwezi amini , ukaribu na mke wangu ulikufa kabisa , si ukaribu wa ndoa. Namaanisha ushirikiano kama Wanandoa.
Kipato chake sikukiona tena , mambo yote tuliokuwa tunashirikiana hasa ya kimaendelo na kiuchumi zilishia kabisa, ndani ya kama mwaka mmoja hivi niliona kipata ndani kimepungua kabisa, nilijua shida ni ile ishu, nilijaribu kukaa na kuongea nae tena sana, yeye anasema kuwa yeye yupo sawa hana shida. Nilijaribu kupambana mimi mwenyewe na maisha ila wapi ni vijipesa vidogo tuu ndo vinaingia ndani na mshahara wa kazini tuu.
Mke wangu yeye yupo na mambo yake haniusishi kabisa mimi.

Sometime nikawa najipa tuu moyo kuwa mimi ndo me ninatakiwa kurisha familia yangu, naamua kusonga mbele ila mambo yanaenda kawaida na mambo yangu mengi wanaanguka, mishe hacienda kabisa.

Natafuta ushauri kwa watu wa ninaokutana nao kwenye bar na sehemu zingine , wengi wanasema tuu ulizingua mara nyingi watoto hao tunawaacha kwa mama zao huko huko, kwani ulivyofanya hivyo umemwonyesha mkeo ushahidi kuwa ulimsaliti tena ukamletea home kabisa ushahidi. Wengi wanasema tuu usaliti unauma sana huyo mkeo anaumia mpaka kesho. Wananiambia tuu potezea kaka.
Ila ni kitu ninakijutia sana sio kwamba ninamchukia mtoto hapana nachukia ule uzinzi nilifanya .
Nilimueleza mother aliniambia tuu kama mtoto anaishi nae fresh hakuna shida kubali matokeo tuu.

Sometime natamani kuona siku zinarudi nyuma ila haiwezekani, Najuta sana maana naona maisha yamedrop sana. Yale maendeleo hakuna kabisa kama awali.

Sasa nina umri wa miaka 42,
Maisha napambana tuu mimi mwenyewe kama Baba wa familia sioni ushirikiano kutoka kwa mke wangu, lakini nimejipa moyo kuwa mimi ndo mwanaume nitalisha familia yangu. Ila kinachoniuma ni mahusiano wa kushirikiana na mke wangu yamekufa kabisa. NAJUTA SANA.

Marafiki zangu wengi wapo na mafanikio sana na wake zao nawaona hata jinsi wanavyoishi.
Kuna rafiki yangu mmoja wa karibu sana mwezi wa 3 aliingiza Toyota land cruiser LC300 GX la kwake na mke wake GX.
Huyu ni mmoja tuu wapo wengine wapo fresh sana , najua wapo hivyo kutokana na mahusiano na wake zao hasa ya kiuchumi.

Mimi hapa ni na ka harrier changu kimetengenezwa miaka 14 iliyopita naona hata aibu kuwakaribisha hata home friends wangu.
Na Hata kukutana nao tuu.

NB; JAMANI WANAUME WENZANGU TUTULIE KWENYE NDOA ZETU HASA TUNAPOPATA MKE MWENYE MIBARAKA KWENYE NDOA ZETU. NI MUHIMU SANA UNAWEZA UKAONA STORY ILA MWENZENU YAMENIKUTA.

SOMETHING NAJIRAUMU KUWA NINGEJUA NINGEMUACHA KWA MAMA YAKE NIKABAKI MUUDUMIA.
SOMETHING NAONA NILIKUWA SAHIHI KUMCHUKUA.

Sorry mimi sio mwandishi mzuri, naomba radhi kwa makosa mtakayo baini.
uzinzi haujawahi kumuacha mtu salama
 
Nikioa nitazingatia sana hili,hata hivyo mimi ni mtu wa kutosheka.Na inawezekana mkeo yupo hapo nawe kwa sababu ya watoto wake,vinginevyo!

Pole sana
 
Acha kulialia maisha yaendelee. Muache anune, so long us hajaomba talaka wewe kula maisha. Tena tafuta demu mkali mwingine zalisha
 
ninachoweza kusema... ulitoa BOKO Part I.... Ukabug ukatoa BOKO Part II... Pile sana!
 
Back
Top Bottom