Najutia tukio hili: Sikuweza kumsaidia rafiki yangu akajinyonga

Majuto ya kinafiki tu asilimia kubwa wa Tanzania wagumu sana kutoa msaada kwa wanaohitaji msaada hila ukisikia amekufa ndio mnajifanya mnahuzuni na unatoa hela ya kusafirisha msiba wakati marehemu alishakuomba msaada Mara kibao ukakataa wakati uwezo ulikuwa nao na inawezakuwa ungemsaidia ungekua umeokoa maisha yake.
 
Kazi yake mola haina makosa
 
Pole sana! Inanikumbusha mimi miaka ya 90 mwanzoni. Nilikuwa nisafiri kwenda Dar bahati mbaya siku hiyo ndege ikaahirisha hai kesho yake. Basi ikanibidi nirudi zangu nyumbani. Ilipofika mida ya saa kumi na mja hivi, nikaamua kwenda sehemu kupata kiburudisha koo. Wakati naenda huko nilikutana na rafiki yangu, alikuwa akifanya kazi TRA, akataka niambatane naye, lakini akaghairi baadae kwani alidai ngoja aende kutazama sinema. Nilienda huko nilikokuwa nikienda na majira ya saa mbili usiku nilirudi zangu home. Nikiwa nimelala majira ya saa tano usiku niligongewa mlango, nikambiwa rafiki yako kachomwa kisu yuko hoi hospitali. Alichomwa kisu akiwa kabisa kakaribia nyumbani kwake mida ya saa nne akitoka kutazama sinema. Niliamka nikaongozana na majirani tukaelekea hospitali. Nakumbuka tulimkuta chumba cha daktari juu ya kitanda akiwa anakata roho. Na mimi nikamfunga macho!!!

Hadi leo huwa najilauma na kujiambia endapo ningeongozana naye labda mauti yasingemkuta. Rest in eternal peace my friend T.
 
Hembuuuu...?! sasa hii inahusiana nini na kujinyonga kwani JPM alisema anajinyonga na hatukufanya jambo kuepusha?
 
Mkuu,mambo haya yanaumiza sana moyo,unahisi ungerudisha muda nyuma anagalau ufanye jambo la kumsaidia.Pole sana mkuu!
 
Asante mkuu kwa maneno yako ya faraja na ya kunizidisha nisonge.Nimejifunza mengi kutokana na kuondoka kwake,nimejifunza nichukue hatua kwa mtu mwingine akinishirikisha jambo kama hili tena.Kusahau ndio imeshindikana mkuu.Namuona hadi leo,nahisi kuna wajib sikuuitimiza katika kumshauri kwangu.
Siku ya tukio nilienda kwenye harusi ya mfanyakazi mwenzangu alikuwa anaoa.Rafiki yangu huyo aliwapigia simu baadhi ya rafiki zake wengine kuwaaga,simu yangu niliisahau nyumbani siku hiyo sikwenda nayo kwenye harusini.Niliporudi alfajiri nilikuta missed calls nyingi sana,lakini kwa vile ni alfajiri ilikuwa nikasema nilale nitapiga kesho yake asubui.12 asubui nikagongewa mlango ya taarifa ya msiba.
Nililia sana,kwenye msiba wake nilmkumbatia mama yake nikalia sana na kumuomba nsamaha.Majibu ya mama yake aliniambia sina cha kuombea msanaha nilikuwa mtu mzuri sana kwa rafiki yangu.Laiti ningepokea ile simu nikaongea naye,laiti angeongea na mimi,labda yasingetokea hayo yote!
 
Kama alikwisha kufa msamaha unaoumba unapoteza muda wako,mgeukie Mungu wako akuondolee hiyo roho ya kujuta kwani mpaka hapo sioni kosa lako ni nini,wakati aliejiua ndio mwenye kosa mbele za Mungu.Wewe hata ungemshauri asijiue tayari mwenzako alikuwa na roho ya mauti inamfuatilia na kwakuwa hakusimama vizuri kiimani usingeweza kuzuia kujiua kwake...
 
pole sana, binafsi hakuna kitu huwa kinaniuma kama picha ya Patrick Lumumba mpambanaji wa Zaire, ile aliyopigwa wazungu wakiwa wamemkamata wamemfunga kamba na walikuwa wanaenda kumuua, hakuonekana hadi leo. it really pains, sijui waafrica tulikuwa wapi kipindi hicho. kuna watu wamezipigania sana hizi nchi, kwa damu, na wazungu walitufanyia unyama mkubwa sana.
 
Kuna jamaa nae leo ni mteja wangu sema kama baharia tu anapiga vibarua vya hapa na pale kaniambia anataka kujiua
Huyo nae hana muda,utasikia keshajipachika kitanzi
 
Huyu lumumba alifanya nini mpaka akafa?

Kifo chake kilikuaje?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Kafungue uzi wa malamiko huko tumechoka wamekufa wangapi hamkusema haya?
 
Ni miaka mingi sasa imepita, mambo mengine hayafutiki akilini ila hakuna namna kubali tu alishaondoka na hatarudi tena.

Hata mfalme Daudi alimlilia mwanaye yule aliyezaa na mke wa huria wakati mtoto anaugua, alipofariki aliacha kulia na akasema it's ok hawezi kurudi tena.

So achana na hilo. Maisha yaendelee.
 
Inaniuma sana hii na mimi?Huu ni usaliti wa waafrika mkuu!
 
hii kitu usipokuwa makini inaweza kukukuta kama yule mpiga picha kule darfur sudan yaliyompataga
Aliyempiga picha mtoto wakati anahitaji msaada,akamuacha akaliwa na Tai.Picha ile ilimpa umaarufu sana yule bwana.Alikuwa anaitwa Kevin Carter,aliulizwa baada ya kumpiga ile picha mtoto ilikuwaje kilichoendelea?Cha ajabu hakuwa na jibu na ikajulikana jibu ni alimuacha afe,watu wakaunganisha kwamba aliliwa na tai baada ya yeye kuondoka bila kumsaidia!Wazungu Bhana!
 
Marehemu alikuwa hana utimamu hata umteteeje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…