Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,683
- Thread starter
- #321
Polycystic ovary inatokana kwenye ugonjwa unaoitwa POLYCYSTIC OVARY SYNDROME(PCOS).Vipi kuhusu polycystic ovary?
Naweza kushika Mumbai?
Polycystic ovary inaweza kujulikana kupitia kwenye ultrasound na dalili nyingine ambazo nimeziorodhesha chini.Wanawake wote wana follicles kwenye mayai na kila mwezi kundi la follicles linatengenezwa ambalo lina follicle mmoja inayotawala na kupevusha yai.
Wanawake wenye PCOS wanakuwa na follicles nyingi ndogo ambayo hazina uwezo wa kupevusha yai kila mwezi.Na hizi follicles zinashindwa kukua kawaida kutokana na hormonal imbalance.
Na kwasababu yai halipevuki kama linavyotakiwa inasababisha wanawake wenye ugonjwa huu kupata shida kubeba ujauzito.
Ovary(Jinsi follicle inavyopevusha yai)
Utajuaje kama una PCOS
- Irregular periods:Siku za hedhi zisizo na mpangilio.Mara nyingi wanawake hawa hupata jumla ya menstruation period 6-8 kwa mwaka.Wanaweza kupata hedhi ya kawaida kwa miezi kadhaa kisha kuruka mwezi au miwili au kuenda miezi kadhaa bila ya kuona siku za hedhi.Watu wenye tatizo hili wanashida kupata mimba kutokana na siku za hedhi kuwa irregular na hata wakishika mimba kuna risk ya hio mimba kutoka.
- Kuongezeka kwa andorgens/testosterone(homoni za kiume) mwilini,hii inaweza kuonekana kwenye damu kwa vipimo tofauti au kwa dalili kama kutokwa na chunusi nyingi(ngozi kuwa na mafuta mengi),vinyoleo kukua kwa wingi mf wanawake wanaoota vinyoleo usoni au kifuani.
- Polycystic ovaries:hii inaonekana kwenye ultrasound
Cc babuukikolo

