Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

mimi niliwai kuumwa rhematoid arthritis dose zake zilikuwa zinafanya nachoka na kulegea ka bwege hivi ni miaka 20 iliyopita nikiwa na umri wa 18,nilipona lkn sijarudi sawa kwa jiyo hali ua kuchoka mwili na kichwa kuwa kizito kama nahisi nisionane wala kuongea na mtu yeyote maana nikiongea mpaka nahema kwa kuchoka,miguu nikisimama au kutembea robo saa inauma na kuvimba kwenye joints.Nimechoma Neurobion,Diprofos nilipata nguvu na nafuu ktk ufahamu lkn ni kidogo kuliko matarajio yangu.Msaada tafadhali
 
Sasa doctar hizo dawa za u.t.i ulizozitaja tunazitumiaje mana umezitaja tu huwezi kutoa matumizi yake tafadhali doctor
 
Katika hospitali kuna matibabu ya upungufu wa nguvu za kiume? Achilia mbali Hawa wa tiba mbadala na wale wanaoshauri mazoezi na lishe.
Nauliza hii field ktk hospital zetu ipo na inatibu wenye tatizo hilo?
 
Mimi nilijifungua mtoto wa pili nikachanika sana na nikashonwa lakini baada ya muda mshono uliachia mpaka sasa sehemu kubwa iko wazi.Nifanyeje niweze kurudi katika hali ya kawaida?
 
kuna mdogowangu baada ya kukaa na mke
mwak1 aliend kupima mbegu za kiume spam
majibu yakwa
MICROSCOPIC EXAMINATION.
Count......2h/thousan
Motility.....2% of motile with slow foward
progressive,98 of.
doct amempa dawa aina ya Ova-mit ameze nusu
kwa muda wa miez2 na daw Testosterone
Undecanoate ameze moja kwa miez2.
Naomba kuuliza kazi kubwa za dawa hiz mbili na
utendaji kazi na pia natak kujua chakula bor cha
kutumia ili kuondokan na tatizo hilo kwan hiv
sasa ni mtu wa kuwaza tu .
naomba ufafanuz na ushauri weny ma
 
Nataka kujua ni katika mazingira yapi mgonjwa kiwango cha sukari kinaweza kupanda wakati mgonjwa mwenyewe hali... takribani wiki sasa kila anapokula anatapika.
 
Kjembe, mgonjwa wako mwenye kisukari ana kisukari type 1 au 2? Amekuwa nacho kwa muda gani? Anatumia dawa? Dawa gani anatumia? Anatumia insulin pia?Sukari inakuwa juu wakati gani?

Kuna sababu nyingi zinazoweza kufanya sukari ipande pamoja na kwamba anakula kidogo tu na kutapika.

Inawezekana kwa kuwa hali vizuri, mwili wake unajaribu kutendeneza sukari kutoka katika hifadhi ya mwilini ili kukidhi mahitaji yake. Sasa kama dawa anazotumia hazifanyi kazi, mwili unashindwa kuitumia hiyo sukari na inakuwa inaongezeka tu kwenye damu.

Ushauri wangu ni kwamba mpeleke mgonjwa kwa daktari ili amfanyie uchunguzi wa kina kujua ni nini anahitaji kama ni kubadilisha dawa, kumpa insulin, nk
 
Hi,asante doctor kwa kuanzisha thread hii.Mim naomba kujua kwa nin mke wangu ana mzunguko wa hedhi usio tulia? Mara nyingine huwa anakuwa na 32 hata miezi minne,29 kwa miezi 3 nasaiz cjui itakuwa ngapi maana cku 29 zimeisha jana.Naomba kueleweshwa kwan nahitaji mtoto.
 
Inabidi uende kwa dactari wa magonjwa ya wanawake ili ampe matibabu yanayotumia hormones na dactari atakwambia wakati wa kufanya tendo la ndoa ili uweze pata mimba. Kinachosababisha apate siku hedhi katika nyakati tofauti ni "hormonal imbalance" ambayo inaweza kuwa "regulated" kitaalamu ili awe anapata siku zake katika hali itakayomuwezesha kujua ni wakati gani muafaka wa kufanya tendo la ndoa na kutunga mimba. Wataalamu wa "fertility" wanafanya hayo matibabu kwa watu wengi tu.
 
Nadhukur kwa ushaur,mfano huo mwez ambao amemalizia jana imekuwa mp ya 30 days
 
Habari Daktari!
Nina tatizo la kuugua Amoeba mara kwa mara.Mostly nikiugua Amoeba natumia dawa aina ya Nor-T. Lakini baada ya wiki mbili ama tatu naugua tena.Naomba msaada wako, nifanye nn ili angalau nisiugue Amoeba mara kwa mara?
NB: Najitahidi sana kutokula ovyo magengeni, kunywa maji yasiyochemshwa, kutumia vyombo visivyooshwa vizuri kwa ajili ya chakula n.k.Kwa kifupi najitahidi sana kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu but ndani ya muda niliousema naugua.
 
Ndugu Jiwegangi, mara nyingi unapotumia dawa moja mara kwa mara kutibu magonjwa hasa ya maambukizo"infections" baada ya muda hivyo vijidudu vinakuwa sugu na hiyo dawa inakuwa haina uwezo wa kutibu vizuri hizo infections. Mfano mzuri ni jinsi ambavyo kwa muda tulikuwa tukitumia chloroquine kwa malaria, lakini kwa sasa malaria hasa hapa Tanzania ni vigumu kuitumia kwa chloroquine kama zamani maana vijidudu visababishavyo malaria vimekuwa sugu. Sasa, inawezekana kwamba hiyo dawa unayoitumia kwa ajili ya Amoeba, kwa kuwa umekuwa ukiitumia kwa muda sasa, imeishasababisha amoeba walioko kwenye mwili wako kuwa sugu. Nenda kapime kama kweli una amoeba, kisha jaribu kumwambia dactari akupe dawa nyingine au aongeze dose. Pia baada ya kumaliza matibabu, pima tena kuhakikisha wamekwisha mwilini. Kama bado wapo mwilini, dactari atakusaidia labda kuendeleza dose kwa muda mrefu zaidi au kufanya utafiti zaidi kuona ni kwa nini hii hali inajirudia au kuna tatizo lingine.
Tatizo letu ni kwamba baada ya kuandikiwa dawa, wengi wetu hatufanui tena ufuatiliaji kuona kama tatizo limeisha.
Pia hakikisha dawa haijaisha muda wake wa matumizi (expired).
 
Nashukuru sana kwa ushauri na maelekezo. Nitajitahidi nifate yote uliyonishauri. Mungu akubariki, akuzawadie maisha marefu.
 
Back
Top Bottom