Ndugu Jiwegangi, mara nyingi unapotumia dawa moja mara kwa mara kutibu magonjwa hasa ya maambukizo"infections" baada ya muda hivyo vijidudu vinakuwa sugu na hiyo dawa inakuwa haina uwezo wa kutibu vizuri hizo infections. Mfano mzuri ni jinsi ambavyo kwa muda tulikuwa tukitumia chloroquine kwa malaria, lakini kwa sasa malaria hasa hapa Tanzania ni vigumu kuitumia kwa chloroquine kama zamani maana vijidudu visababishavyo malaria vimekuwa sugu. Sasa, inawezekana kwamba hiyo dawa unayoitumia kwa ajili ya Amoeba, kwa kuwa umekuwa ukiitumia kwa muda sasa, imeishasababisha amoeba walioko kwenye mwili wako kuwa sugu. Nenda kapime kama kweli una amoeba, kisha jaribu kumwambia dactari akupe dawa nyingine au aongeze dose. Pia baada ya kumaliza matibabu, pima tena kuhakikisha wamekwisha mwilini. Kama bado wapo mwilini, dactari atakusaidia labda kuendeleza dose kwa muda mrefu zaidi au kufanya utafiti zaidi kuona ni kwa nini hii hali inajirudia au kuna tatizo lingine.
Tatizo letu ni kwamba baada ya kuandikiwa dawa, wengi wetu hatufanui tena ufuatiliaji kuona kama tatizo limeisha.
Pia hakikisha dawa haijaisha muda wake wa matumizi (expired).