Juzi kati niliona kuna Mdau amelalamika kuwa kuna kampuni imekuwa ikimtumia ujumbe na wakati mwingine kumpigia kwamba wanataka kununua mkopo wake uliosalia kutoka Bosi ya Mikopoy a Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), sasa nami nimeona niweke hapa kero yangu inayoendana na hiyo.
Kuna hii kampuni imekuwa ikinitumia ujumbe wa kuomba kununua mkopo wangu ambao umesalia kutoka HELSB kila wiki.
Imekuwa kero kubwa kwangu kutumiwa ujumbe huo na mara kwa mara hasa kwa kuwa sikutoa namba yangu katika hiyo kampuni sijui taasisi ya kukopa, sasa wametoa wapi namba yangu au HELSB ndiyo wanagawa kama yule mwingine alivyosema.