Nakerwa sana na haya maneno: "P,PW,K,JOMONI"

Nakerwa sana na haya maneno: "P,PW,K,JOMONI"

Watanzania wengi wamekuwa wabahili sana.yaan wabahili mpaka kwenye maneno wanapunguza herufi!!!!au wameiga kwenye Yale makabila ya kulee
 
Nimejifunza sana kwakweli,situmii tena jomoni,
Kiswahili uchwara kwendraaaaa!
 
Kimbe tuko wengi tunaochukia haya maneno, kingine nachochukia n hiki ki kijinga [emoji120]
 
Dawa yake we usiyatumie mkuu utakuwa na amani

Hiyo lugha inatumiwa na visichana vya sekondari vinapokuwa vinachati na mabasha wao I wonder dume zima linapoandika kwa kutumia lugha hiyo na hiyo jomoni wanaitumia mademu umboko ukiwa umezama kule papuchini
Kwao
 
Neno poa lina versions 3 yani pow, pw na p. Mi mtu akishaniambiaga hivyo nafutaga namba yake. Na saivi wameleta mtindo wa kusema tyu badala ya tu.
Kuna kamjomba kangu kalikuwa kanataka msaada kikaja na hayo makitu kalikomaje!
"Xaxa uncl vp".mie kimya "nkclzia uncl"kimya
Baada ya wiki tatu " shikamoo mjomba"
Mimi "marhaba" yeye "vipi meseji zangu hujazipata?
Mimi"zipi hizo mjomba "
Yeye "nimekutumia kama wiki tatu na kila baada ya siku mbili nakukumbusha na naona umesoma ila hunijibu sasa vipi utanisaidiaje maana siku ndio zinaenda"
Mimi"unamaanisha yale maandishi nikiyoshindwa kuyasoma?mimi nilifikiri ni smart phone inajigusagusa sijafatilia hata kidogo !".
Yeye" Dah Mjomba basi naandika upya!
Mimi "sawa ila kwa lugha fasaha "
Yeye "samahani mjomba sifanyi tena!
Hapo nokamsaidia japokuwa kiukweli muda ule nilikuwa sina kitu ndio nikapata sababu ya kutoka nduki nikijifanya namnyoosha!
 
Jomoni maana yake nini? Hili neno naliona sana humu jf
"Jamani"ila ile mi shoga kutamka jamani kwa kubenua midomo yao hawawezi ndio wanatumia jomoni kwa kuwa silabi "o"ina wapa wanachokitaka au wengine hutamka"jamwani"ambapo "w"ina serve same purpose kama "o"
Kingine hilo neno jamani ni neno la kudeka kqma litatumiwa peke yake au kuwatayarisha watu kupokea habari .
Mfano jamani eeh!hii kazi ianze sasa hivi"
Au mtoto wakike kwa mama yake"ai mama JAMWANI/JOMONI /JAMANI ndio hutaki eh?"
Au demu kwa mpenzi wake" George JAMANI /JAMWANI/JOMONItwende basi!"
Kimsing kuna maneno wanaume hatutumii.
Mfami mwingine huwezi kusema "rafiki yangu eh !jana club si nilimkuta Rose na SHOGA yake Amina!
Mwanaume utasema tu jana club nilimkuta Rose na rafiki yake Amina"
 
hilo "jomoni" nikiliona huwa sisomi text ya mtu. Linachefua sana
 
Back
Top Bottom