Nakiri kuwa hii ni moja ya zawadi bora kwenye maisha yangu

Nakiri kuwa hii ni moja ya zawadi bora kwenye maisha yangu

Honestly niwe muwazi kwenye hili
......

Upendo kwa familia mliyozaliwa ndugu wa kike na wa kiume ni Raha sana....

Pili kumwelewa ama kuwaelewa ndugu zako..... udhaifu wao na nguvu yao iko wapi......

Mfano kwenye hasira, ni mtu wa maneno mwingine mbinafsi, mchoyo n.k ukishamwelewa ni rahisi kuenda nae

Tatu ndugu muishi katika mipaka ........ Acheni mambo ya kusemana mfano Kuna ndugu wanaopatana sana na mwingine hapatani nanyi sana ko epukeni kusemana huyu kafanya hivi, huyu vile hiyo ni mbaya sana.......

Ishu za bills kwa wazazi au jambo la kifamilia kila mtu aweke wazo lake ama fungu lake hata kama kidogo lakini ushiriki wake uonekane...... Kama Hana kabisa itajulikana.......

Kila mtu ana maisha yake hasa mkishaanza kujitegemea semezaneni kwa hekima busara maake kila mtu anakuwa kavurugwa na maisha, mahusiano ama hulka ya mtu in nature inakuwa hivyo

Pia msiishi kwa kushindana najua hii ipo sana kila mtu ana bahati yake, mafanikio yake, kuzaliwa tumbo moja haimaanishi kuwa mtafanikiwa kwa level moja hapana ......... Kila mtu afanye kitu kwa nafasi yake na kwa muda wake

Sio kila Siri ama jambo utamshirikisha ndugu yako wengine mkigombana kidogo mtaanikana hewani stop that......

Nimeshuhudia kwenye familia ya mzee wangu saa hz kila mtu Yuko kivyake.....

Naomba sana Mimi na ndugu zangu tupendane till last breath kutofautiana kupo Ila kusipitilize........


Mkigombana ile serious aseeh hata mkipatana ni ile msionekane hamna mwenye kinyongo........

Ponya majeraha ya moyo........ Hakikisha umepona then samehe.....

Good luck
Ushauri nzuri sana
 
Inasikitisha sana mkuu, familia moja mnakuwa na mabeef ya kijinga.

Braza alikuwa best sana yani, niwe na issue gani nisimwambie au yeye akiwa na mambo yake lazima aniambie. Ila sentensi moja tu ilivuruga mahusiano hadi leo.
Mkuu ERoni hapo kwenye sentesi, uli mu undermine nini???
 
Mkuu umefukua tena,
Aliniambia kitu kikanikwaza, sikuvunga nikamwambia bro umezungua na sijapenda, si unajua zama hizi hata ukiwa mdogo unasema tu! That's how it started.
Hahaha, sija fukua kwa makusudi. Nili kuwa nasoma kitu.
Ndo nika ona hiyo sentence, but make sure you talk about it.

Fanya hata kesho umpigie, mwambie nakupa hi bro. Mwaka mpya huu.
 
Back
Top Bottom