Nakiri kuwa hii ni moja ya zawadi bora kwenye maisha yangu

Nakiri kuwa hii ni moja ya zawadi bora kwenye maisha yangu

Moja ya zawadi bora nilizopata kwenye maisha yangu, ni mdogo wangu wa mwisho. Hadithi muhimu ni kwamba alikuja katika wakati ambao hatukutarajia.

Mama yangu ni mtu ambaye anapenda watoto sana, ila Moja ya maombi yake makubwa ili kuwa apate mtoto wa kike lakini kwa bahati nzuri au mbaya, hilo hali kuweza kutokea hadi miaka 10 baadae.

Kama wanae aliotulea, hiyo story ya mtoto wa kike tuliisikia sana, so unaweza imagine alipokuja ilikuwa ni furaha kubwa sana. Jambo muhimu ni kwamba mimi na yeye tuna chemistry muhimu, I won't lie (tangu akiwa na miaka 2, amekuwa rafiki yangu bora Sana.)

Sometimes namwita mama, dada, toto. Kutokana na majukumu ya ki-jobless pro max, Mimi na yeye kuonana ni Mara chache Sana kwa Mwaka. Huwa nina zungumza nae Mara kwa mara, mnunulia zawadi, cheza nae. Best moment of mine.

Nikaamua likizo hii niitumie na familia, na kusema ukweli ni sehemu hii ni kumbukumbu bora Sana. Japo ni kaka yake, ila najivunia kusema yeye ni zawadi bora Sana kwenye maisha yangu. Nitaitunza, ijali na kuilinda katika maisha yangu Kikubwa heri na uzima utawale.

I mean no malice to anybody.

View attachment 3196722
View attachment 3196724
Tufanye sasa Barter Trade Mkuu 🤣
 
Honestly niwe muwazi kwenye hili
......

Upendo kwa familia mliyozaliwa ndugu wa kike na wa kiume ni Raha sana....

Pili kumwelewa ama kuwaelewa ndugu zako..... udhaifu wao na nguvu yao iko wapi......

Mfano kwenye hasira, ni mtu wa maneno mwingine mbinafsi, mchoyo n.k ukishamwelewa ni rahisi kuenda nae

Tatu ndugu muishi katika mipaka ........ Acheni mambo ya kusemana mfano Kuna ndugu wanaopatana sana na mwingine hapatani nanyi sana ko epukeni kusemana huyu kafanya hivi, huyu vile hiyo ni mbaya sana.......

Ishu za bills kwa wazazi au jambo la kifamilia kila mtu aweke wazo lake ama fungu lake hata kama kidogo lakini ushiriki wake uonekane...... Kama Hana kabisa itajulikana.......

Kila mtu ana maisha yake hasa mkishaanza kujitegemea semezaneni kwa hekima busara maake kila mtu anakuwa kavurugwa na maisha, mahusiano ama hulka ya mtu in nature inakuwa hivyo

Pia msiishi kwa kushindana najua hii ipo sana kila mtu ana bahati yake, mafanikio yake, kuzaliwa tumbo moja haimaanishi kuwa mtafanikiwa kwa level moja hapana ......... Kila mtu afanye kitu kwa nafasi yake na kwa muda wake

Sio kila Siri ama jambo utamshirikisha ndugu yako wengine mkigombana kidogo mtaanikana hewani stop that......

Nimeshuhudia kwenye familia ya mzee wangu saa hz kila mtu Yuko kivyake.....

Naomba sana Mimi na ndugu zangu tupendane till last breath kutofautiana kupo Ila kusipitilize........


Mkigombana ile serious aseeh hata mkipatana ni ile msionekane hamna mwenye kinyongo........

Ponya majeraha ya moyo........ Hakikisha umepona then samehe.....

Good luck
 
Back
Top Bottom