Nakubaliana na ndugu Bashe kuruhusu wakulima kuuza mazao popote wanapotaka

Ebu tukumbushe kipindi cha Mwinyi na Kikwete walipofunga mipaka,maana mi sikumbuki kabisa kama ilitokea.

Unamaanisha nini unaposema kufunga mipaka? Tangia lini mipaka ya Tanzania ikawa wazi na wapi ambapo iko wazi?
 
Nakuhurumia Kwa jinsi usivyojua biashara zote duniani zina middle man kuwepo kwa middle man hakuathiri mwenendo wa bei hata hao middle man katika soko huria nao hushindana mwenye bei nzuri kumzidi mwenzie ndie hufanya biashara sana.

Tatizo ni kwamba mkulima akikosa soko middle man anageuka mwokozi kwa kumtafutia soko ila pia soko likiwa zuri middle man asilaumiwe.

Ule ni mnyororo wa thamani. Yaani haiwezekani mkulima akafanya kazi zoote yeye mwenyewe Iko hivyo nyakati zote kwenye biashara ya kilimo.

Hata leo chukua lory la mananasi peleka stereo ni ngumu sana kutana na mlaji wa mwisho lazima ukutane na mtu kati ndiye akuunge Kwa mlaji wa mwisho.
 
Wakulima mnaiwasema hamuwajui.

Sasa hivi wanao uza ni wafanya biashara. Wakulima wananunua vyakula pia.

Nahisi mnaishi nje ya hii nchi.

Waliuza Sasa hivi Wana Lia njaa. Serikali haiwezi kukwepa hii aibu.
Ikiwa Kuna mkulima wa aina hiyo basi ni wale wakulima waliokata tamaa ya maisha na Hana lengo lolote la maisha. Mkulima halisi huuza mazao ili kufidia gharama alizotumia Kwa maana ya kununua pembejeo kuhifadhi akiba na ziada hutumika Kwa matumizi mengine.

Hivyo unapomlazimisha auze Kwa bei ndogo kitakachotokea ni kwamba atakosa hela za kufidia gharama ya kuzalisha itabidi apunguze shamba au aache kulima ageuke machinga na utaratibu huu ukiendelea Kuna mwaka taifa litaagiza chakula chote Toka nje baada ya wakulima kuachana na kilimo na kuhamia kwenye kazi za kijinga tu zinazotabirika.
 
Ungeelewa kwanza nilichomaanisha.

Sijasema middle men hawafai nimewajibu hao wanaokazana kusema bora bei ipande ili wakulima wafaidike ndo nikawajibu hata hao wakulima hawafaidiki kama inavyoonekana huku nje. Wanadhani mchele ukiuzwa 4,400 huku dar basi yule mkulima wa chini kabisa aliuza 2500 per kilo. Unakuta mkulima aliuza gunia la mpunga kwa laki, tajiri analiweka ghalani anakuja kuuza baadae. Sasa mkulima anafaidika vipi na laki? Hiyo 2500 unakuta ni bei ya alienunua kutoka kwa mkulima na sometime wanauza hata zaidi. Wanaofaidika ni middle men na wale wakulima wenye direct access na soko kuu. Sio wale wa chini. Na kwa utafiti wako, large scale Farmers Tanzania unajua wako wangapi? Kwamba umkute mkulima wa ifakara kule anaelima na tractor la kuazima atakua na hata tani tatu ghalani?
 
Nimeelewa mantiki yako biashara ikiwa mbaya Kwa middle man hata huyo mkulima mdogo anaumia zaidi ingawa manufaa ya mkulima wa chini hapa ni uhakika wa soko la bidhaa zake
 
Kumbe Marais waliopita walikuwa wanazuia mazao kuuzwa nje? ndio maana kilimo kipo ICU

Samia ndio atakipaisha kilimo cha Tanzania na kukifanya kiwe biashara na ajira nzuri, kwa kuwapa uhuru wakulima
 
Hii hoja mfu inapigiwa bango na watu wasio wakulima na wasiojua hata biashara ya kilimo ipo vipi

Hakuna kuzuia mazao ya mkulima
 
Hakuna soko lisilokuwa na madalali, kanunue hisa kwenye soko la hisa Dar, lazima kuna dalali, kanunue gari Japan lazima kuna dalali, nyumba n.k
 
Hapo wanaofaidika ni middlemen, wakulima wa chini wataendelea na hali zao zilezile kama hawauzi mazao yao kwenye vyama vyao vya ushirika
Wewe ni mkulima ? Usijitie kutetea wakulima kama wewe hulimi, maana unaongea usichokijua
 
Mkulima hana jukumu la kukulisha wewe, mkulima anatafuta faida kama wafanyabishara wengine wanavyotafuta faida kwa kutafuta masoko mazuri
 
Bro Mimi nimeuza ton 30 za mshindi siku chache zilizopita
Dalali alinipigia simu nikampa Bei yangu ni elfu 98 kwa gunia
Yeye kamwambia mnunuzi elfu 99 mia 5
So hapo shida nini
Mimi nimefikia matarajio yangu
Nimeuza mahind
Nimenunua mbolea
Maisha yanaendelea
 
Mkulima hafaidiki, mnufaika ni Dalali
 
Ko ulitaka Kila kitu kipande ila mazao ya mkulima yashuke bei kwani yeye ana dunia yake?
 
Jamaa zetu walisahau kabisa kuwa maridhiano si leseni ya kuwafurahisha CHADEMA wa mjini kwa kuwagandamiza Wakulima. Dhana yao ni kwamba bei ya vyakula itashushwa na tumehuru. Badala ya kuipongeza Serkali kwa kuruhusu wakulima wetu wafaidike kwa bei nono, wao wanatumia hili jambo kisiasa.
ZFZMWCCM
 
Dah sijui kwanini watu wanakua wagumu kuelewa. Sasa wewe una tani 30 ndugu yangu mimi naongelea wale small scale farmers mbona tangu mwanzo kabisa wa mada hiyo ndo ilikua point yangu?

Hivi unadhani nchi nzima wakulima wana simu, wana tani 30 ghalani. Sasa basi acha taifa liongelee shida za matajiri wenzao hawa wa chini atawasemea nani? Mimi siwaongelei nyinyi mnalima na mna mishe zinawaingizia hela.

Kuna kulima anategemea heka yake moja tu ndo isomeshe wanae. Hata mimi ni mkulima na muuzaji wa mpunga. Nielezeeje aisee? Au ulitaka tujue kuwa una tani 30 ndani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…