Nakubaliana na ndugu Bashe kuruhusu wakulima kuuza mazao popote wanapotaka

Ni Kweli Ni wajibu wa serekali Sasa kutoa ruzuku kwa wakulima has a pembejeo kilimo Ni ngumu hata ulaya huko wakulima wao wanapewa ruzuku kubwa Sana ili kustablize Bei ya vyakula

Ila Huku cc hatuwapi ruzuku ya maana badala yake wanawalazimisha kuuza ndani hpn Kama wakulima wakipewa ruzuku mnk Ni kwamba hata wakat was kuuza wapeww Bei elekezi ili kufidia ruzuku serekali iliyolipa kupitia ruzuku yetu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hii hoja mfu inapigiwa bango na watu wasio wakulima na wasiojua hata biashara ya kilimo ipo vipi

Hakuna kuzuia mazao ya mkulima
Kichwa panzi kingine hiki hapa. Nani kasema wazuie mazao ya wakulima?

Wakulima wa chini wajikusanye na wao waweze kupeleka mazao yao nje waione faida. Mijitu inayo comment kwa mihemko inanichosha!
 
Sema mfanya biashara na madalali na sio mkulima.
 
Sema mfanya biashara na madalali na sio mkulima.
Soko la mkulima ni Kwa dalali hatimae Kwa mfanya biashara siku zote Iko hivyo hata huyo mfanya biashara nae anatake risk Kwa kununua mazao ambayo yakishuka bei huwa inakula kwake
 
Uchumi wetu haujatengemaa. Ni sawa na wafanyakazi, wanalipwa kila mwezi ila mshahara hauja wahi kukutana.

Kwa hiyo usidhangae mkulima anae vuna mara moja ama mbili kwa mwaka.

Cha msingi serikali ijiandae kwa hari hii ambayo ndio maisha harisi ya matanzania.
 
Hiyo ni lugha ya picha, mtu kulumangila picha ya samaki kwa ugali mkavu hadi anashiba!

Ni jambo linalotia matumaini lakini lisilowezekana.

Hakuna "class"ya ukulima wa kilala hoi itakayofaidika na sera hiyo, never!

Watakaofaidika ni "class" ya wafanyabiashara, kuanzia walanguzi mpaka ma exporters na kufanya maisha ya wakulima walala hoi yaendelee kuwa duni mno!
 

Kwa hiyo unakusudia kusema wakulima wakiuza Kwa bei ndogo ndio watafaidika eee?

So far kama unafahamu kuhusu hali ya gharama ya kilimo ya sasa Kwa heka moja niwekee hapa mchanganuo alafu upendekeze bei itakayomlipa mkulima tolea mfano zao la mahindi.
 
Kichwa panzi kingine hiki hapa. Nani kasema wazuie mazao ya wakulima?

Wakulima wa chini wajikusanye na wao waweze kupeleka mazao yao nje waione faida. Mijitu inayo comment kwa mihemko inanichosha!
Nimekuuliza wewe ni mkulima?
Maana hujui unaloongea
Utanunua mazao kwa bei ya juu ama ukalime na wewe, hakuna wa kukulisha hapa
 
Nimekuuliza wewe ni mkulima?
Maana hujui unaloongea
Utanunua mazao kwa bei ya juu ama ukalime na wewe, hakuna wa kukulisha hapa
Kila mtu jf anataka avimbe. Nije hapa nikwambie kwamba nna mashamba mbarali, kyela na ifakara itakusaidia nini. Sijaja hapa kujiongelea mimi naongelea small scale farmers acha ubinafsi!
 
Kila mtu jf anataka avimbe. Nije hapa nikwambie kwamba nna mashamba mbarali, kyela na ifakara itakusaidia nini. Sijaja hapa kujiongelea mimi naongelea small scale farmers acha ubinafsi!
Mwezi aprili 2021 kilo ya mahindi ilikuwa ikiuzwa 250 hadi 400, serikali ikawa inanunua mahindi kwa wakulima kwa ajili ya kuweka ghalani na kusisitiza sana ni lazima waweke mahindi ya akiba

Kama kuna mkulima aliuza mahindi yote unataka serikali imsaidieje? Serikali ihangaike na kila shida ya kujitakia?
 
Sijui nielezeje uweze kunielewa!

Gharama za kuzalisha eka 1 ya mahindi ninaijua, ukianzia kuilima, mbolea, palizi, viuatilifu hadi kuvuna.

Na ni kweli kabisa kuwa, gharama za uzalishaji zipo juu kuliko bei ya kuuzia hayo mazao sokooni.

Wewe nadhani ni mkulima mwenye uwezo wa kusafirisha, lakini si wakulima wote wenye uwezo hata tu ile ndoto ya kuweza kutimiliza ndoto hii!

Je ni wakulima maskini wangapi wanaoweza kuchukua vibali na wakasafirisha mazao yao mpaka letsay Kenya ama Uganda?

Wakulima wetu wengi ni wakulima wa kujikimu tu.

Ninachodhania mimi, Serikali ikitaka kuwasaidia wakulima maskini, ni kuimarisha vyama vya Ushirika vitakavyowatafutia masoko yenye bei nzuri wakulima, kukusanya mazao yao na kwenda kuwauzia kwa bei yenye tija.

Na si kwa kila mkulima mmoja mmoja asiye hata na uwezo wala connection yoyote ya kuweza kujitafutia masoko yeye mwenyewe!
 
Mkuu naomba nikiri kwamba wewe unakielewa kilimo ni kama mimi na wewe sote tunapambania maslahi ya mkulima mimi ninachopinga ni kugandamiza bei ya mazao bila kujali mzalishaji ataingia hasara. Lazima zitafutwe njia za kumlinda mzalishaji ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha na masoko mazuri lkn pia serikali iweke ruzuku nyingi kwa wakulima.

Maana ukishusha bei Kwa kudhani unamkomoa mfanyabiashara sio kweli hiyo bei ndogo utakayomwagiza mfanya biashara itaenda kuleta maafa Kwa mkulima Kwani huyu mfanya biashara Hana shamba anakusanya mazao Toka Kwa mkulima mdogo.

Nakumbuka mwaka Jana maembe ya wakulima yalianza kuozea shambani sababu wafanyabiashara walipangiwa kulipa laki tatu Kwa lory kama ushuru Kwa h/shauri matokeo yake wafanyabiashara wakasusa maembe yalianza kuozea shambani.

Kwa hiyo ukipunguza bei ya mazao maana yake umemtuma mfanyabiashara akamkalie kooni mkulima mdogo ambako mfanyabiashara anapata mazao.
 
Sasa ndo umekuja kwenye point yangu. Kwamba asilimia kubwa ya wakulima wana hali ya chini sana hawana uwezo wa kutunza hayo mazao ghalani. Wanauza kwa bei iliyopo sokoni kwa muda huo hata ikiwa sh 200 kwa kilo. Tofauti na wanaojiweza wanatunza ghalani wanaweka akiba. Wakulima wengi nikimaanisha wa hali ya chini wanalima ili wakivuna wauze wasaidie familia zao.

Na point yangu ambayo wote mnairuka mnakuja kucomment kwa mihemko ni kwamba. Hawa small scale farmers na wao wasaidiwe kupata kikundi chenye uaminifu cha kiserikali ambacho kitakusanya mazao yao na wao wakauze nje ya nchi. Kwasababu sio wote wenye access ya kwenda kuuza nje ya nchi. Sijui kama naeleweka au unajiskia tu kubishana.

Na labda nikuongezee tu, unaongea na mtu ambae mwaka wa tisa huu nna lima mpunga na nna nunua kwa wakulima pia. Na mwaka 2021 niliuza mchele shillingi 800 kilo ifakara, mwaka jana nimeuza bei nzuri tu.
So nnapoongelea maswala haya sio kwamba nimekurupuka, nawaongelea small scale farmers na wao watazamwe: mnanichosha mnakuja kucomment wakati point yangu hamuielewi
 
Kutunza mazao sio lazima ghalani, kuhifadhì gunia moja la mahindi unahitaji ghala?

Hata hivyo serikali imegawa vyakula kwa maeneo yaliyoathiriwa na njaa, ila sio wpte watakaopata

So huwezi kuharibu soko zima ili kuweza kunuaisha watu ambao hawaweki akiba

Mimi ni mkulima pia na najuana na wakulima wadogo ambao wanahifadhi na kuna ambao hawahitadhi kwa kupuuza

Vitu vingine ni uzembe, ukilea uzembe utaendelea kujitokeza tu kila mwaka acha wazembe wapate njaa ili wajifunze
 
Asa mnacholalamika ni nini nyie wajuba? Kumbe mazao hayajapanda bei, jamani twendeni tukanunue mazao Kwa wakulima tuweke stoo, kama madalali wanaweza kwanini Sisi raia mmoja mmoja tushindwe.
 
Ewaaa!
Hapo naona tunaruka kwa uelekeo mmoja.
Pamoja sana mkuu👍
 
Kwanza mkulima anauza mazao yake akisha vuna tu kwa mfanyabiashara. Labda Serikali iwe inanunua na kuhifadhi(NFRA) kwa bei ya soko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…