Uchaguzi 2020 Nakubaliana na Rais Magufuli kwamba Wagombea Urais kupitia Vyama vya Upinzani wamuunge mkono ili kuokoa fedha za walipakodi

Uchaguzi 2020 Nakubaliana na Rais Magufuli kwamba Wagombea Urais kupitia Vyama vya Upinzani wamuunge mkono ili kuokoa fedha za walipakodi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wakati akiwapongeza NEC kwa kubana matumizi na kuokoa takribani sh bilioni 12 katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Rais Magufuli " alichomekea" kwamba hata wagombea urais wa upinzani wanaweza kuamua kumuunga mkono yeye ili kuokoa kodi za wananchi.

Mbatia, Prof. Lipumba na Mzee Cheyo walitabasamu na kupiga makofi kama ishara ya kufurahishwa na hoja hiyo kwa niaba ya wapinzani.

Nami kwa niaba ya CCM naunga mkono hoja hiyo kwa 100% nikiamini Chadema na ACT wazalendo nao wataunga mkono kwa manufaa mapana ya taifa.

Nawasilisha.

Maendeleo hayana vyama!
 
Si angeamua tu kuvifutilia mbali vyama vyote ibaki CCM tu!mbona katiba inayotumika ni ya mfumo wa chama kimoja?halafu mbona yeye yuko juu ya sheria,anaweza kuamua atawale milele
 
Huyu jamaa yenu ni muoga wa kampeni. Pamoja na wapinzani wake kuwafunga minyororo ya miguuni na mikononi,funga kufuli za midomo kwa miaka mitano lakini bado anaogopa kampeni za miezi miwili tu.

Huyu manager Magufuli aliingia kwenye siasa kwa bahati mbaya tu. Siasa za Kidikteta ndiyo anaziweza.
 
Aharibu tu uchaguzi na iwe kama ule wa serikali za mitaa.
 
CCM mnachekesha sana. Nyie tu juzi kwenye kura sa maoni mmemtumia ujumbe huyo mwenyekiti wenu kuwa hamkubaliani nae kwa mambo yake ya ajabu kwa kuwaangusha watu wake na watu waliokuwa wanajitanabaisha kuwa watetezi wake. Alafu mnasema wapinzani wajitoe Kwenye uchaguzi. Kweli mmekosa sana akili nyie watu.

Hakuna rangi mtaacha ona CCM mwaka huu. Lissu ndo huyo yuko njiani kuja kuchukua uraisi wake wa Jamhuri ya Tanzania
 
Wakati akiwapongeza NEC kwa kubana matumizi na kuokoa takribani sh bilioni 12 katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Rais Magufuli " alichomekea" kwamba hata wagombea urais wa upinzani wanaweza kuamua kumuunga mkono yeye ili kuokoa kodi za wananchi.

Mbatia, Prof. Lipumba na Mzee Cheyo walitabasamu na kupiga makofi kama ishara ya kufurahishwa na hoja hiyo kwa niaba ya wapinzani.

Nami kwa niaba ya CCM naunga mkono hoja hiyo kwa 100% nikiamini Chadema na ACT wazalendo nao wataunga mkono kwa manufaa mapana ya taifa.

Nawasilisha.

Maendeleo hayana vyama!
Kuna kitu umevuta leo, siyo bure.
 
Naunga mkono hoja kwa ombi lifuatalo.

Aagize maafisa wa uchaguzi watende haki. Kura za wananchi ndiyo ziamue.

Naateo onyo kwa maafisa wowte watakoviruga uchaguzi watarudia kwa gharamaa zao.

Kisha ahidi kuunda serikali ya mseto kutegemea na idadi ya wabunge wa upinzani watakao patikana.

Magufuli hoyeeeeee.
 
Wakati akiwapongeza NEC kwa kubana matumizi na kuokoa takribani sh bilioni 12 katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Rais Magufuli " alichomekea" kwamba hata wagombea urais wa upinzani wanaweza kuamua kumuunga mkono yeye ili kuokoa kodi za wananchi.

Mbatia, Prof. Lipumba na Mzee Cheyo walitabasamu na kupiga makofi kama ishara ya kufurahishwa na hoja hiyo kwa niaba ya wapinzani.

Nami kwa niaba ya CCM naunga mkono hoja hiyo kwa 100% nikiamini Chadema na ACT wazalendo nao wataunga mkono kwa manufaa mapana ya taifa.

Nawasilisha.

Maendeleo hayana vyama!
Ni kwanini aseme yeye ndiye aachiwe kuwa mgombea pekee wa Urais na wenziwe wajitoe?

Ni kwanini yeye Magu hasemi kuwa yeye atajitoa na kumuunga mkono Tundu Lissu awe mgombea pekee, ili kuokoa gharama za uchaguzi?
 
Naunga mkono hoja....

Maana kuna vyama vingine inajulikana wazi vinaenda kushindwa
Demokrasia ina gharama. Tumekubali mfumo wa vyama vingi, vinginevyo turudi kwenye mfumo wa chama kimoja.

Hoja ya kushindwa haina mashiko, mshindi huwa ni mmoja tu lakini washiriki na washindani lazima wawepo.
 
Back
Top Bottom