Kweli Mkuu.
Mimi binafsi wazazi wangu waliachana tangu nikiwa na mwaka 1. Na nikalelewa na Mama pekee.
Mara nyingi tangu nikiwa mdogo mama amekuwa akinifanya nimchukue Baba, alikuwa akinijaza Maneno mabaya tu ya Baba. Kwamba Baba haunitaki, amenitoa zawadi Kwa Mama. Akawa anahasira nae sana Kila akimkumbuka.
Sasa Mimi nimekuwa mkubwa. Nimesoma Kwa shida sana Hadi nimemaliza chuo. Nimeipata kazi ni nimefunga ndio.
Kuna tukio Moja limenikuta. Nimemfumania live mke wangu akigegedwa na mtu mwingine. (Hii kitu isikie tu, usiombe ikukute nusu niue mtu). Nashukuru nikipata hekima za kimungu. Niliwaacha salama
Nilienda kumpa taarifa Mama kuwa nimemfumania mke wangu, hivyo naachana nae. Nikamsimulia kilakitu kichotokea kwenye like fumanizi.
Cha ajabu nikamuona mama anabubujikwa tu na machozi, akaniambia Mwanangu hayo matukio Yako yote unayonisimulia ndiyo yaliyonikuta Mimi Kwa Baba Yako Hadi akaniacha na wewe Mwanangu akakutelekeza.
(Nikajikuta namwambia mama huyu mwanamke siwezi kumsamehe hata akija Rais wa nchi, akiwa na bastola mkononi)
Kikubwa nilichojufunza ni kwamba wanawake Huwa hawasemi mabaya Yao Kwa watoto wao. Wanawajaza chuki tu watoto Kwa makosa yaliyosababishwa na wao wanawake.