Wamissionari kutoka Ulaya na Marekani walioeneza ukristo hapa nchini; walikuja kutoka mashirika mbalimbali ya huko kwao, na waligawana maeneo ya uinjilishaji; ambapo African Inland Mission (ambao ndio chimbuko la dhehebu la AIC), kutoka Amerika; walianzia uinjilishaji Kanda ya Ziwa hususan Mwanza (maeneo ya Nassa, Kijima, Sumve, Geita, n.k)
Baadae kanisa lilienea taratibu maeneo ya jirani na Mwanza na milia jirani kama Shinyanga; (maeneo ya Kolandoto, Ilula - Kishapu, Nyamalogo - Nindo n.k)
Makao makuu ya AICT ni Makongoro jijini Mwanza.
Askofu wa kwanza wa AICT alikuwa Jeremiah Kisula Mahalu; ambaye kwa wakati huo alikuwa ni Askofu pekee Tanzania nzima, alifuatiwa na Askofu Nyagwaswa, ambaye baadae alileta mabadiliko ya muundo wa kanisa kwa kuanzisha maeneo mbalimbali ya kiutawala; ambapo zilianzishwa Dayosisi mbalimbali zikipngozwa na Maaskofu wa kuchaguliwa.
Sasa AICT imepanuka; iko nchi nzima mpaka Mtwara, Sumbawanga, Kigoma; Dar n.k.