Nakukumbusha tena, "acha kubeti" mwisho wa betting sio mzuri

Nakukumbusha tena, "acha kubeti" mwisho wa betting sio mzuri

Mkuu Ben-adam hii dondoo yako nimei save kabisa kama funzo la kuwaelimisha wengine hapo baadaye kwa kuwa mimi mwenyewe ni mdau ambae nipo huko na madhara nayaona sana, yote hayo kama ulivyo yatiririsha hapa.

Niliwaza kipindi flani kuwa niachane na Betting labda nigeukie Forex yaani FX lakini mbona naona kama ni yale yale tu sambamba kabisa na Stock Exchange n. K vipi mkuu una wazo lolote kuhusu hizi sectors??
big up kwa kukiri hilo, uko ktk hatua nzuri maana tayari umeshatambua mahala ulipo. Sijajihusisha sana na forex lakini nakumbuka mwanzo wa kuijua forex ndo ulikuwa mwanzo wa kuanza kwangu kubeti, (ni stori ndefu kidogo) lakini kwa mtazamo 'wangu' betting na forex tofauti ni majina
 
Kijana acha kubeti, amua kuachana na utumwa huo bettingi haitakuacha salama

Katika betting sio tu unapoteza pesa bali unapoteza na uwezo wa kufikiri, ubunifu nk

Betting inaweza kuathiri sana akili ya mtu, na mara nyingi athari hizi hujikita taratibu, hivyo kuwa ngumu kugundulika mapema. Athari hizi zinaweza kubadilisha jinsi unavyofikiria, kufanya maamuzi, na hata jinsi unavyothamini mambo muhimu katika maisha yako. Hapa ni jinsi betting inavyoweza kuathiri akili yako:

1. Kuwepo kwa Msongo Mkubwa wa Mawazo

Watu wengi wanaojihusisha na betting huingia katika hali ya wasiwasi kutokana na mawazo ya kushinda au kupoteza. Uzoefu wa kushindwa mara kwa mara unaweza kuathiri sana hali ya kisaikolojia, kuleta msongo ambao hukufanya kuwa na mawazo hasi na mara kwa mara kujihisi huna thamani. Kila unapoendelea kupoteza fedha zaidi, msongo unaongezeka, hali inayoweza kupelekea mawazo ya kujihisi umefeli.

2. Kukosa Dira na Maono katika Maisha

Uraibu wa betting unaweza kufanya mtu kupoteza dira na kutoona fursa nyingine za kujikuza kimaisha. Mtu hujikuta akizingatia sana namna ya kushinda kwenye betting kuliko kuona njia nyingine za kujiongezea kipato. Kwa mfano, unaweza usione fursa za biashara ambazo zingeweza kukuingizia kipato halisi na endelevu. Mtu anaweza hata kuacha kazi au masomo kwa matumaini ya kupata "pesa" kwa kupitia betting.

3. Kujihisi Kukata Tamaa na Huzuni Kali

Kushindwa kwa mara kwa mara kunaleta huzuni na kukata tamaa. Watu wengi wanaopoteza fedha kwenye betting hujilaumu kwa maamuzi yao. Wanaweza kujiona kama watu wasio na bahati, wasio na uwezo wa kufanya maamuzi mazuri, na hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa kujithamini kwao. Kwa kuwa betting hujenga matumaini yasiyo na msingi wa uhakika, mtu anaweza kuwa na hali mbaya zaidi ya kukata tamaa kila mara anapopoteza.

4. Kupoteza Udhibiti na Maamuzi Sahihi (Impulsivity)

Betting huchochea hali ya kuamua mambo haraka na mara nyingi bila kufikiria matokeo yake. Hii hufanya mtu kushindwa kuweka mipaka ya kifedha. Mtu anaweza kutumia fedha nyingi ambazo hazikuwa kwenye bajeti, au hata kuingia madeni kwa sababu ya tamaa ya kutaka "kupata mara moja" kupitia betting. Hii ni hatari, kwa sababu hujenga tabia ya kufanya maamuzi yasiyo sahihi hata nje ya betting.

5. Kuvurugika kwa Mahusiano ya Kijamii na Watu wa Karibu

Betting inaweza kusababisha matatizo ya mahusiano, hasa na familia na marafiki wa karibu. Uraibu wa betting huleta hasira, msongo, na wakati mwingine mtu anakuwa na hatia kwa kutumia fedha ambazo zingeweza kusaidia familia au kutimiza mahitaji mengine muhimu. Mahusiano ya kijamii yanapoanza kuvurugika, unajikuta ukiwa mpweke na kuhisi watu wamekuepuka kwa sababu ya maamuzi yako.

6. Kutoweza Kupanga na Kutimiza Malengo ya Maisha

Betting inachukua muda na rasilimali nyingi, hali inayosababisha kutokuweza kuweka malengo ya muda mrefu na kuyafanyia kazi. Kwa kuwa unapata changamoto ya kujipangia bajeti, inaweza kukufanya kushindwa kuwekeza katika mambo yenye faida ya muda mrefu. Mtu anaweza kushindwa kujiwekea akiba au kufanya maamuzi mazuri ya kifedha ambayo yangemsaidia kuwa na uhuru wa kifedha.

7. Kuathiriwa na Matamanio ya Pesa Za Haraka

Betting hujenga dhana potofu ya kwamba mtu anaweza kupata pesa nyingi haraka. Hii huathiri sana mtazamo wa mtu kuhusu kazi ngumu na bidii ya muda mrefu. Unapojikuta ukitafuta njia za mkato kupitia betting, unakosa fursa za kweli ambazo zinaweza kuleta matokeo bora kwa muda mrefu.

Namna ya Kujinasua na Betting na Kurudisha Hali ya Utulivu wa Kiakili

*Kujihusisha na Shughuli za Kimaendeleo - Tumia muda wako kujifunza stadi mpya, kama biashara au ujasiriamali.

*Kuweka Malengo Madogo na Kufuata Mpangilio wa Bajeti - Kuwa na malengo yanayoweza kutekelezeka na kuwa na nidhamu ya kifedha ni hatua kubwa ya kutoka kwenye betting.
Mwisho kabisa ni kuichukia betting yenyewe
Hakika haya maneno mwenyezi mungu alishatuonya karne na karne zilizopita kwenye quran tukufu suratul maidah aya ya 90 , leo tunajionea wenyewe vijana wanavyoharibika ,mungu hajawahi kukosea kwenye kauli zake
 
Attachments

  • Screenshot_20241027-161439_Chrome.jpg
    Screenshot_20241027-161439_Chrome.jpg
    99.6 KB · Views: 8
Ndo maana nimesema ni bahati ya mtu na mtu kitendo cha wewe kuwa huna bahati hiyo basi na wenzio hawana au watakosa

Vijana wengi tu wametusua kupitia betting

Tena unakuta mwingine kaweka book tu lakin kesho yake anaamka mpaka na milion mia

Kuhusu uzoefu wako hata mimi niliwahi kutana na mtu mmoja ambaye zaman alikuwa anasali sana lakin hakuona faida ya Sala na kanisa

Jamaa akanizuia kwenda kanisan akasema yeye kashasali sana na hakupata faida au kuona faida

Lakini mimi niliendelea kusali tu kila siku na leo hii nimeiona faida ya Sala na MUNGU MWENYEZI kanibariki

Kwahiyo kushindwa kwako wewe sisi kuwa na wengine watashindwa

Asante
Sio kweli kama vijana wengi wametusua. Wengi wanaliwa, na wanachezea vipigo hawasemi, wakipata siku moja wanapiga kelele.

Waambie waliotusua wakuonyeshe account zao kwa miaka miwili iliyopita.
 
Ndo maana nimesema ni bahati ya mtu na mtu kitendo cha wewe kuwa huna bahati hiyo basi na wenzio hawana au watakosa

Vijana wengi tu wametusua kupitia betting

Tena unakuta mwingine kaweka book tu lakin kesho yake anaamka mpaka na milion mia

Kuhusu uzoefu wako hata mimi niliwahi kutana na mtu mmoja ambaye zaman alikuwa anasali sana lakin hakuona faida ya Sala na kanisa

Jamaa akanizuia kwenda kanisan akasema yeye kashasali sana na hakupata faida au kuona faida

Lakini mimi niliendelea kusali tu kila siku na leo hii nimeiona faida ya Sala na MUNGU MWENYEZI kanibariki

Kwahiyo kushindwa kwako wewe sisi kuwa na wengine watashindwa

Asante
hahah nakuelewa vizuri na najua ilivyo ngumu kukubalia na mimi.
Mimi nimewahi kupata pesa nyingi sana kupitia betting(elewa ninaposema "nyingi")

Hapo juu nimezungumzia "bajeti" sijajiandikia tu kufurahisha msomaji!

betting ni ulimwengu mwingine kabisa tofauti na unavyodhani
 
big up kwa kukiri hilo, uko ktk hatua nzuri maana tayari umeshatambua mahala ulipo. Sijajihusisha sana na forex lakini nakumbuka mwanzo wa kuijua forex ndo ulikuwa mwanzo wa kuanza kwangu kubeti, (ni stori ndefu kidogo) lakini kwa mtazamo 'wangu' betting na forex tofauti ni majina
Sawa mkuu maana forex wanadai ni fani kabisa na unaisomea that's why kuna vitabu vyake kabisa na kwamba uki specialize una kuwa huna tofauti na profession zingine kitu ambacho ni tofauti kabisa na betting ambayo wala haina kanuni isipokuwa taratibu zake tu ambazo hata layman anaweza zifuata.. Hii ikoje mkuu?
 
Kila kitu ni kamari katika hii dunia hata ukilima shamba ni kamari,, hata kuoa au kuolewa ni kamari,, ukigombea uongozi ni kamari...faida kuu ya betting inafanya mtu aishi kwa matumaini ya baadaye kama ulikuwa hujui.
kamali ya shambani (kulima) haiwezi kukuathiri kama kama ya mtandaoni
 
Shsr
hahah nakuelewa vizuri na najua ilivyo ngumu kukubalia na mimi.
Mimi nimewahi kupata pesa nyingi sana kupitia betting(elewa ninaposema "nyingi")

Hapo juu nimezungumzia "bajeti" sijajiandikia tu kufurahisha msomaji!

betting ni ulimwengu mwingine kabisa tofauti na unavyodhani
Share kidogo nasi ulibutua mpaka shilingi ngapi mkuu?
 
Sawa mkuu maana forex wanadai ni fani kabisa na unaisomea that's why kuna vitabu vyake kabisa na kwamba uki specialize una kuwa huna tofauti na profession zingine kitu ambacho ni tofauti kabisa na betting ambayo wala haina kanuni isipokuwa taratibu zake tu ambazo hata layman anaweza zifuata.. Hii ikoje mkuu?
siwezi kuizungumzia sana forex lakini kuna nyuzi humu zimeielezea kwa upana, ukitaka kujifunza unaweza kuzisearch hapa hapa JF
 
hahah nakuelewa vizuri na najua ilivyo ngumu kukubalia na mimi.
Mimi nimewahi kupata pesa nyingi sana kupitia betting(elewa ninaposema "nyingi")

Hapo juu nimezungumzia "bajeti" sijajiandikia tu kufurahisha msomaji!

betting ni ulimwengu mwingine kabisa tofauti na unavyodhani
Bas Amna ndugu yangu Ben-adam
 
Naungga mkono hoja. Pia inaweza kukufanya uwe mtumia vilevi kupindukia kama pombe, bangi nk. Pamaja na umalaya mkubwa. Sababu kubwa ni ukipoteza pesa nyingi kwa wakati mmoja ni lazima upunguze machungu kwa aina moja au nyingine, mbadala wa kujiua unajizuru kwa namna nyingine.
amini amin nakuambia.
Umeandika kinyume.
Ieweke tu kwamba betting inaua nguvu za kiume.
Betting ni aina ya ulevi unaokumiliki viungo vyako vyote na hisia.
Ila betting tunapenda kuijadiri kijuu juu mno bila kuelewa aina za betting na uwezekano wa kukosa na kupata na kwa kias gani!
Wanaojua betting na aina zake hawafikirii kuacha bali chaguzi bora za kubet.
Kuanzia aina ya betting, machaguo na kiasi.
 
thread zako nyingi ni kupinga betting,unaonaje uegemee zaidi kuandika makala za ndoa?
Nafikiri ungeegemea zaidi ktk kushauri wana ndoa
 
Hii nimekutana nayo mahali flani, wanasema kuwa uoga wa kupoteza pesa umewagawanya wawekezaji(investors) katika makundi manne kama yalivyooneshwa kwenye picha niliyoattach hapo. Na kundi mojawapo ni la Gamblers. Tofauti kati ya gambler na true investor ni kwamba, for a gambler investing is a game of chance and for a true investor, investing is a game of skills...
1000009808.jpg
 
amini amin nakuambia.
Umeandika kinyume.
Ieweke tu kwamba betting inaua nguvu za kiume.
Betting ni aina ya ulevi unaokumiliki viungo vyako vyote na hisia.
Ila betting tunapenda kuijadiri kijuu juu mno bila kuelewa aina za betting na uwezekano wa kukosa na kupata na kwa kias gani!
Wanaojua betting na aina zake hawafikirii kuacha bali chaguzi bora za kubet.
Kuanzia aina ya betting, machaguo na kiasi.
hahah umeanza vizuri, ila hapo mwisho hapo; betting ikishakukamata vizuri, ukikosa unahisi kama uliweka option mbovu! hivyo ndivyo ilivyo
 
Kuna ukweli hapa.
Sema wale wamiliki wa betting ni illuminated, wana nguvu kubwa nyuma na mbele yao
 
Back
Top Bottom