Nakukumbusha tena, "acha kubeti" mwisho wa betting sio mzuri

thread zako nyingi ni kupinga betting,unaonaje uegemee zaidi kuandika makala za ndoa?
Nafikiri ungeegemea zaidi ktk kushauri wana ndoa
kila kona kuna ushauri wa aina hiyo, kwahiyo mimi naona mambo ya ndoa yana wasemaji wengi inatosha, hata hivyo kamari inaweza kuwa sababu ya hizo ndoa (baadhi) kufarakana.
 
ndio maana ya pili ikawa "true investor" tena ni "a game of skills..."
 
Vijana hatuwezi kukuelewa, wwngine hiyo nd'o kazi pekee inayotuweka hapa mjini!

Muungane muanzishe kampuni ya betting au kama zile michezo ya wachina mtakuwa hambahatishi.

Katika watu elfu moja wanaobeti buku buku kila siku ni labda kumi tu watashinda pesa za maana kwa wiki. Hata hao wakaoshinda hupotezi unaweka bima.

Ukiamua unaweza kupotea mazima na billioni pesa zao ukiwaambia kuna technical issue unapambana nazo.

Baadaye unaanzisha kampuni nyingine unaanza mchezo upya.
 

Nakubali matumaini ni kitu muhimu kwa binadamu ndio maana kuna manabii feki kibao, kampuni kibao za kubet, forex.

Ukitaka utajiri wa haraka na wa uhakika anzisha, kampuni ya kubet. kuuza forex, anzisha kanisa, kuwa chawa wa watawala,, uganga wa kienyeji uwasaidie waliologwa.
 
Makampuni mengi yaliyofanikiwa duniani yamewekeza kwenye hisia. Furaha, matumaini, status, nk. Hakikisha bidhaa au huduma yako inagusa hisia fulani kali ya watu. Ukishateka hisia za binadamu hauwezi kumpoteza kirahisi.
 
ukishaamini ktk betting akili inafungiwa humo humo huwezi kuona fursa nyingine nje ya hapo
 
ukishaamini ktk betting akili inafungiwa humo humo huwezi kuona fursa nyingine nje ya hapo
Sidhani kama hilo unalosema ni kweli kwa wengi.

Ila kama nilivyosema betting kama jambo lingine lolote, inabidi ulifanye kwa akili na bila mihemko. Nikikupa mfano, mimi siku hizi nacheza Jackpot pekee na nacheza tiketi moja tu. Sasa buku litanivuruga vipi? Nasema kama umeandikiwa kushinda utashinda tu hauhitaji kucheza kwa fujo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…