Nakukumbusha tena, "acha kubeti" mwisho wa betting sio mzuri

Betting inamadhara makubwa sana ya kisaikorojia.kifupi kubet kama bahati nasibu nijambo la hatari sana ambalo badae litakupa majonzi makubwa sana.
Kunakijana nimemshuhudia anashinda betting akiwa nanguo za shule nabeg lake mgongoni.
Ukweli hadi leo nimeshindwa kuelewa akila yayule kijana niyanamna gani!
Pia sio betting tuu jalibu kukosea kuoa mke hapo utaingia katika gereza kubwa sna lenye mateso mazito.
Tunayaona nakusikia vifo na mauwaji vitokanavyo na mapenzi nivingi kwatakwimu havina idadi kabisa.
Pombe ulevi kupindukia,madawa yakulevya hivi nivitu vinavyo tafuna sana kizazi kilicho pita,sasa hadi kinacho kuja.
 
Na wewe umeona umeandika kitu cha maana sana enh!!!acha kupangia watu maisha yao,wanatumia pesa zao hivyo acha kuwashwawashwa kwa andiko la kijinga
 
Rubbish
 
Wewe inaonekana ulishawahi kuwa kwenye betting na ukawa master kabisa, ila umeona balaa lake, Kuna kipindi Fulani nilikuwa nafanya tafiti kuhusu hayo mambo lakini sikumaliza utafiti, nilichogundua aisee acha kabisa, vijana kazi hawafanyi zaidi ya kubeti tu, vijiwe vingi TZ wanaongelea hzi ishues si mjini Hadi vijijini ndani ndani hukooo, wanabeti halafu hawana kazi za kufanya au akifanya basi nusu ya pesa inaenda kwenye betting.
 
Uko sawa kabisa mkuu, hayo madhara unaweza ukaona kama hayahusiani na kamari hivi lakini ndio uhalisia ulivyo... Kisaikolojia zaidi

Kamari ina uraibu na uraibu unaathiri mfumo wa ufahamu katika ubongo na kusababisha matatizo ya kisaikolojia, ambayo sio rahisi kuyatambua/kuyashitukia, mapema.

Kitu chochote chenye uraibu kikishafikia hatua hiyo ya uraibu/chronic, iwe ngono madawa pombe kamari inaondoa utimamu wako wakuweza kuamua mambo mwenyewe (self control) badala yake chenyewe ndio kinakuendesha utake usitake, jiulize kwanini walevi, wavuta sigara, unga hawaachi licha ya mateso wanayopata.


Ni moja ya vitu ambayo watu wengi wanakujaga kujifunza muda/umri ukiwa umeshawatupa mkono/ yaani wakiwa wameshachelewa, na hapo ndipo neno ningejua huja mwisho wa safari.
 
Betting inaweza kukupa hadi shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo. Unaona timu 15 zimeshinda kwenye mkeka wako bado mbili tayari unajua una milioni kumi, Ile ya mwisho sasa. Moyo unakimbia, tumbo linacheza, kichwa kinauma, kukaa huwezi, kutembea huwezi unapoona unapigwa.

Uchungu, huzuni yake ni kama umefiwa vile.
 
Hiyo bahati ni ya muda tu utashinda ila amini hata hicho ulichojipatia kitarudi huko
Hata mkeo anaweza kurudia huko ulikomtoa kuliwa kimasihara ukaachwa ukapata msongo wa mawazo ukafwaaaa..... Kila mtu ana. Maisha yake usiwapangie Nini Cha kufanya ....Mungu kawaacha HURU wewe nani uwapangie .... Fanya yako
 
Mimi nachokifikilia huu ujumbe umetufikia sisi tu tusio jihusisha na betting lakini wahusika wenyewe wako tayari kumaliza dakika 15 kwenye kusuka mkeka ambao hana uwakika kama ata pata ama kuliwa...kusoma makala kama hizi kiufipi nikwamba hawana mda huo wakupoteza.........😂😂tuombeane uzima tu amna namna
 
kamali ya shambani (kulima) haiwezi kukuathiri kama kama ya mtandaoni
Habari ya shamba n tofauti na izi betting wakubwa......shambani kama uliandaa ili upate gunia 30 za mahindi.....ikitokea wakati wa mavuno hujata gunia 30 bas lazima utapata 10-15. Utasonga mbele kimaisha unajianda n msimu ujao. Ila betting utaweka laki 5 kwenye betting ukiliwa safari ata nusu upati kwanini usiwe kichaaa
 
Yeah, mimi nina uzoefu wa takribani miaka 10 kwenye betting siongei hapa kama motivational speaker tu bali kwa uzoefu wa hali ya juu kabisa
 
Yeah, mimi nina uzoefu wa takribani miaka 10 kwenye betting siongei hapa kama motivational speaker tu bali kwa uzoefu wa hali ya juu kabisa
Kuacha kwako pombe kusikifanye utake wote tuache pombe...ndio hivyohivyo kuacha kwako kubeti usowatake wengine waache wataacha Kwa wakati wao ukifika.
 
Uko sahihi.
Lakin kuna kubet kibiashara na kubet kiburudan.
Tofaut yake ni kubet kibiashara ni unastake high kwa odd ndogo sana kama 1.2 kwa 100k or +
Unajikuta kila siku una 30k ya mafuta na lunch nje ya kipato halali.
Kwa wenye na baby walkers
 

Acha wewe haha
Wenzako wanabetia ela ambayo angeenda kunywea pombe

Sio ela ambayo angenunua chakula

Sasa mtu anabet odds kumi Kwa elf 3 ili apate elf 30 atafilisika na nini?

Au hiyo elf tatu angefanyia kitu gani?

Hata Kadi ya mwendokasi hawez kununua Kwa elf 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…