Nakumat yainunua Shoprite Tanzania

Nakumat yainunua Shoprite Tanzania

Kampuni ya Nakumat ya Kenya inakamilisha mchakato wa kuinunua kampuni ya Shoprite Tanzania, yenye maduka matatu nchini. Hii imekaaje? Watanzania tumeshindwa kuingia kwenye retail business? Hawa wafanyabiashara wetu wanaolilia Vitalu vya gas wako wapi?

WEWE UKO WAPI? ACHENI KULALAMIKIA WATU WENGINE WAKATI NINYI WENYEWE MMEZEMBEA KWENYE MAISHA YENU HATA KIBANDA CHA NYANYA HAMNA, ndio akili ya kina muhongo kwamba maendeleo yataletwa na wazungu.

WEWE SIO MTU? AAAAHHHHGGGGG....
 
Kwa upande wangu mimi sioni kama ni tatizo kwa nakumat kuinunua shoprite sababu nakumat wanauzoefu na biashara hiyo kwa mda mrefu, na katika biashara huwezi ukafanya vitu vyote peke yako, kwa hiyo kama ndugu zetu wakenya wanaweza wapewe wafanye kazi, najua kuwa kuna watanzania ambao wanaweza kununua hiyo kitu ila hawana tu uzoefu na vitu kama hivyo... Pia suala la gesi sio rahisi kiasi hicho, ku invest kwenye gesi tunaongelea ma trillion na sio ma billion, nimeuona mchanganuo wake ila kwa mtanzania kumuliki kitalu haiwezekani labda wanunue share kidogo sana... Mwenye hela hapa bongo kwa sasa kwa mujibu wa forbes ni rostam aziz ambae anakadiriwa kuwa na utajiri wa USD 1bn kama trillion 1.6 za kibongo, kumbuka utajiri huo sio hela alizonazo benki ila huwa wanajumlisha mali zake zote kama,viwanda, share, majumba, biashara. N.k sasa kama kujenga tanki moja tu la gesi ni wastani wa trillion 16 za kibongo na unatakiwa ujenge atleast matanki matatu nani ataweza hapa bongo?kwa gharama kama hizo utaona hata billgates hawezi kutoa kiasi hicho mwenyewe manake kianaenda hata zaidi ya nusu ya utajiri wake kwa hiyo anaweza kununua share.. Mengi, dewji, bakhresa na utajiri wao haujafikia hata kwenye trillion 1( wana around billion 750_800 kwa mujibu wa forbes)... Kwa hiyo tuache politics... Wawekezaji watakuja tu, tena tutegemee wengi zaidi hasa kwenye suala la gesi, cha msingi nikuwabana tu hao jamaa ili nasisi watanzania tunufaike na huo uwekezaji wao.
 
Kila baada ya miaka 10,kampuni zinauzwa ama kubadilishwa majina na kupata misamaha mikubwa ya kodi,hivi tunaviongozi wanaofikiri ? Hizi trick jamani hua hatuzioni kweli are you serious ? Kikwete na wenzako,haya watanzania washaanza kudai stahiki zao kwanza nawahurumia kwa sababu wengi wao hawana mikataba so walikua kama vibarua....jamani jamani eeeeeeh, kwani nini hivi..? Hivi tumekosea wapi ?
 
Mfanyabiashara siku zote lazima atumie mapungufu ya sheria zetu, hata ungekuwa ni wewe ungefanya hivyo
 
umeuliza au umetoa taarifa!maana mm sijui ulichosema!!...imeuzwa??..inaviongozi??...wafanyabiashara??sasa mbona yote maswali!
 
Kila baada ya miaka 10,kampuni zinauzwa ama kubadilishwa majina na kupata misamaha mikubwa ya kodi,hivi tunaviongozi wanaofikiri ? Hizi trick jamani hua hatuzioni kweli are you serious ? Kikwete na wenzako,haya watanzania washaanza kudai stahiki zao kwanza nawahurumia kwa sababu wengi wao hawana mikataba so walikua kama vibarua....jamani jamani eeeeeeh, kwani nini hivi..? Hivi tumekosea wapi ?

Dah!.. naona mkichanganywa majumbani kwenu hasira mnazimalizia huku!..basi hata ww kichwa maji?
 
Mfanyabiashara siku zote lazima atumie mapungufu ya sheria zetu, hata ungekuwa ni wewe ungefanya hivyo

Wewe hujaelewa kinachoongelewa hapa...nikusaidie kidogo HAPA mtoa hoja hana shida na wafanya biashara analia na usaliti wa baadhi ya wenye mamlaka
 
Dah!.. naona mkichanganywa majumbani kwenu hasira mnazimalizia huku!..basi hata ww kichwa maji?
We usingekua kichwa maji usinge kua ulivyo....ahaha ahaaaa kama uko Tanzania chini ya CCM kwisha habari yako kwa hiyo tuko sawa wala usinishangae mimi jiangalie na wewe.....mimi ni kweli nimevurugwa kitambo sana ukisoma post zangu utanielewa
 
umeuliza au umetoa taarifa!maana mm sijui ulichosema!!...imeuzwa??..inaviongozi??...wafanyabiashara??sasa mbona yote maswali!
Mkuu unaelewa mtu akiuliza anatumia alama gani ? na mtu akitoa taarifa inakuaje ?! sasa nakujibu hivi,nimeuliza na kushangazwa pia sana !
 
Wamiliki wa msululu wa supermarket kubwa za Kenya, Nakumatt, watatakiwa kusubiri hadi katikati ya mwaka huu kabla ya kununua supermarket tatu za kampuni ya Shoprite ya Afrika Kusini zilizopo nchini.



nakumatt.jpg



Manunuzi hayo yalitakiwa kufanyika mwezi huu wa nne lakini sasa yatafanyika baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa tume ya ushindani Tanzania, FCC. "Hatu na uhakika lini tutachukua maduka hayo kwakuwa tumeambiwa na tume ya ushindani ya Tanzania kungoja kwa miezi mitatu mingine," alisema Thiagarajan Ramamurthy, Head of Strategy and Operations wa Nakumatt.
Sababu za kuchelewa huko hazijatajwa.

Supermarket hizo zitauzwa kwa gharama ya dola milioni 40.45. Nakumatt imeahidi kuwaajiri wafanyakazi wa Shoprite pale itakapozinunua ili kupunguza gharama ya kuajiri wafanyakazi wapya. Kampuni hiyo ya Afrika Kusini inaondoka Tanzania baada ya kuonywa kuacha kuchukua bidhaa kutoka Afrika Kusini na kutopromote zile za Tanzania.
Kwa upande wake Nakumatt imepanga kuwapa kipaumbele wazalishaji wa bidhaa wa Tanzania na wale wa Kenya waliopo Tanzania. Hatua hiyo ya kuchelewashwa kwa manunuzi hayo kunaiathiri Nakumatt ambayo ilikuwa imejipanga kuanza biashara mwezi huu.
Chanzo: VenturesAfrica
 
sina tatizo na nakumatt toka kenya kuweza nchini au kampuni kubwa zinazo milikiwa na wahindi since indians have been trading in tz before independence.
tatizo labda lije liwepo ktk uduni wa utoaji huduma.
nakumatt mnakaribishwa.
 
Tumekupata sana mkuu hiyo ni kampuni kubwa ila sasa malipo yao ndo yako chini hata wafanyakazi wengi huacha kazi mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom