Precisely the point unachosema, uzalendo unaimizwa kwa namna zingine nchi nyingi tu za europe uwa wana campign zao za support local farmers, produce na hata serikali zinatoa incentives sana kwa wakulima hili waweze endelea kulima na kufuga, lakini sera za kulazimishana kutumia products fulani bila ya kuzingatia gharama za mfanyabiashara ni ujuha hata wao wanajua ndio maana kuna sector zingine zina dorora ama kufa kabisa as in textile industry. Halafu hata huo uzalendo wa kununua bidhaa za kwenu kwa upendeleo ata kama bei ni za juu una depend na mfuko wa wananchi na how far kipato kinatimiza mahitaji mengine muhimu ya familia vinginevyo ni changamoto, huko Scandinavia wanaongoza kwa kuwa na kipato bora na maisha bora na idadi ndogo ya walalahoi ndio maana linawezekana.
Ngoja nitoe mfano mmoja korosho inayo limwa mtwara hadi kufika dar kipakti cha korosho ambayo imechomwa kienyeji kupitia mchanga, kuni/mkaa na karai na kufungwa kwenye kapakti kwa kuchomewa na kibatari kinauzwa na machinga sh.2500. Machinga alipi kodi ya ushuru, rent, umeme na gharama zingine za mwenye duka. Kipakti cha size hiyo hiyo UK kinauzwa 99p karibu paundi 1. Korosho ya dukani UK imetoka shambani huko ilipotoka mpaka port au kiwandani, imepitia industrial processes, mkulima uko kawekewa tax na yeye kaweka faida, mfanyabiasha uko kawekewa tax na yeye kaweka faida, ikapanda meli ikawekewa gharama, kufika UK tena ika wekewa tax na mwenye duka bado anaona kuna faida ya kuuza sawa na korosho ya Mtwara.
The point nayotaka toa kwanza inabidi waangalie environment inayomfanya mtu alete machungwa kutoka south africa in the first place. Tanzania gharama za chakula ni nafuu sana ukienda vijijini lakini ukianza gharama za usafirishaji, idadi ya walaji bei inabidi ziwe kubwa hili kuona faida au hata ku-break even maana wengi wetu ni wakulima. Vile vile technologia ambazo zinaweza fanya wingi wa industrial processes bado ndio maana gharama za kutoka shambani mpaka kwenye kopo zinakuwa juu na kufanya bidhaa ziwe juu kwa mlaji. Sasa supermarket ni tertiary sector wao wataangalia cheapest secondary environment hiko wapi na wanaokoa kiasi gani, lakini mtu awezi leta machungwa kutoka south afrika if it was cheap for him to buy locally independently, ujui on his bulk shipping anaokoa kiasi gani in short lazima tujue hesabu zao kabla ya kuwalaumu.
Mwisho swala la kununua shoprites lazima kwanza tuangalie wao kama biashara walikuwa wanamlenga nani na asilimia gani yetu. Mteja wa shoprite ni mtanzania yupi na mwenye kipato kipi, na kwanini aende hapo is it quality,convenience, trend shoppers, upmarket etc hili uweze hata sema ataleta impact gani kwa mkulima usije ukawa unamletea uhuni na fujo hili akachukue machungwa na mboga kwenye mashamba ya vigogo kadhaa tu, maana kwa shoprite hata kama watanunua machungwa na mboga za tanzania hawatakuwa na impact yeyote kwenye kilimo in general sana sana wataifaidika a handfull of farmers only.
Tuna environment ngumu sana kufanya biashara lakini the opportunity is vast in Tanzania tatizo ni capital, CDM vipi hawana hela za miradi nijiunge huko habari za siasa za mbele hazina mpango.