Kwa upande wangu mimi sioni kama ni tatizo kwa nakumat kuinunua shoprite sababu nakumat wanauzoefu na biashara hiyo kwa mda mrefu, na katika biashara huwezi ukafanya vitu vyote peke yako, kwa hiyo kama ndugu zetu wakenya wanaweza wapewe wafanye kazi, najua kuwa kuna watanzania ambao wanaweza kununua hiyo kitu ila hawana tu uzoefu na vitu kama hivyo... Pia suala la gesi sio rahisi kiasi hicho, ku invest kwenye gesi tunaongelea ma trillion na sio ma billion, nimeuona mchanganuo wake ila kwa mtanzania kumuliki kitalu haiwezekani labda wanunue share kidogo sana... Mwenye hela hapa bongo kwa sasa kwa mujibu wa forbes ni rostam aziz ambae anakadiriwa kuwa na utajiri wa USD 1bn kama trillion 1.6 za kibongo, kumbuka utajiri huo sio hela alizonazo benki ila huwa wanajumlisha mali zake zote kama,viwanda, share, majumba, biashara. N.k sasa kama kujenga tanki moja tu la gesi ni wastani wa trillion 16 za kibongo na unatakiwa ujenge atleast matanki matatu nani ataweza hapa bongo?kwa gharama kama hizo utaona hata billgates hawezi kutoa kiasi hicho mwenyewe manake kianaenda hata zaidi ya nusu ya utajiri wake kwa hiyo anaweza kununua share.. Mengi, dewji, bakhresa na utajiri wao haujafikia hata kwenye trillion 1( wana around billion 750_800 kwa mujibu wa forbes)... Kwa hiyo tuache politics... Wawekezaji watakuja tu, tena tutegemee wengi zaidi hasa kwenye suala la gesi, cha msingi nikuwabana tu hao jamaa ili nasisi watanzania tunufaike na huo uwekezaji wao.