Uelewa wangu, nilidhani ufiti wa Askari, ni katika utendaji kwenye majukumu yake, kumbe ni kwenye ngumi.
Sasa huku manzese kuna watu wanarusha mkono, kuliko hao magereza na JWTZ, angalau FFU hata hivyo sidhani kama mafunzo yao, yanajikita sana kwenye mkono kuliko kutuliza fujo kutumia nyenzo.
Ila mtaani mtu, anajifua kila siku tangu miaka kumi iliyopita anafanya mazoezi ya mkono. Na mafunzo ya karate, moja ya miiko yake, ni kuwa mpole, siyo kujivunia karate, bali utumie katika kujihami.
Sasa ukimkuta mtu eti sababu yeye ni askari ananzisha fujo kijivunia uaskari wake, jua huyo mikononi mtupu.