Nakumbusha: Kutembea kwa miguu ndio zoezi bora na salama, kukimbia ni kujizeesha kwa hiyari

Nakumbusha: Kutembea kwa miguu ndio zoezi bora na salama, kukimbia ni kujizeesha kwa hiyari

Kuna jamaa yangu ye anajiumiza kila siku kwenye mpira anapenda apungue ila anakula sana.namwambia heri ukimbie au kutembea
Na watu hasa wanawake huwa hawataki kukubali huu ukweli. Sheria namba 1 ya kupunguza mwili ni KUPUNGUZA KABISAAAA KULA. KABISAAAA. mtu unakula kula hovyo (sana) halaf utegemee kupungua eti kisa UNAFANYA MAZOEZI??? NEVER EVER!!!!!
 
Kama huwezi kukimbia tembea tu nalo ni zoezi kwako. Ila usiwabeze wanaokimbia kisa huwezi kukimbia. Wengi wanaohangaika kuponda mazoezi ni wavivu,mazoezi yamewashinda.
Sahihi kabisa. Inaonekana jamaa ni mvivu wa kukimbia hivyo anajaribu kujiliwaza. Sisemi kuwa kutembea hakusaidii ila kama unaweza kukimbia, unapata manufaa zaidi. Halafu kutembea wataalam wanakosema ni kule kutembea kwa kasi, siyo mtu kujivuta kama konokono. Pamoja na kuunguza calories kuna kuvipa viungo na misuli mazoezi na pia mapigo ya moyo.
 
Tembea KWA miguu umbali wa kukutosha.
Kama Kuna vilima na miinuko itakuwa Bora zaidi.

Kama huna muda, paki gari yako mbali au shuka KITUo kimoja au viwili kabla ya eneo lengwa Tembea KWA miguu kikakamavu.

Utanishukuru.
Mwili utabaki Bora na IMARA na mvuto hautapotea kama mkimbiaji na zile apps zao za mabio.

Ni hilo tu.

Mtumishi Matunduizi
Benefits of Brisk Walking
  • Lower impact: It's easier on your joints, making it ideal if you have arthritis, knee problems, or are new to exercise.

  • Sustainability: It can be a more sustainable and enjoyable activity, increasing the likelihood you'll stick with it long-term.

  • Accessibility: It's a great way to get started with exercise and gradually build fitness.
Benefits of Running
  • Higher calorie burn: You burn more calories per minute compared to walking.

  • Faster results: It can lead to quicker improvements in cardiovascular fitness and endurance.

  • Time-efficient: For busy individuals, running offers a more time-efficient way to achieve cardiovascular benefits.
 
Kwa kweli watu wamepotoshwa sana kuhusu mazoezi na hata wanaharibu miili yao!!

Wajasiliamali wanaojiita trainers wanawaongopea sana watu kwenye haya mazoezi....wanajikuta wanafanya mazoezi kuliko uwezo wa miili yao!!.....

Trainers hawatofautishi mazoezi ya wanamichezo ambao wapo active na watu wa kawaida......unakuta ni mchaka mchaka tu.......

Ndio maana wengi wao baada ya kuwa fit wanakuwa na injuries za kutosha kwenye miili yao na kujiongezea matatizo.......

Asilimia 70 ya fitness ipo kwenye diet na 30 ndio mazoezi......kitu ambacho ma trainers hawawaambii watu Kwa kuwa watakosa kamisheni za kwenye gym au wateja wao watawakimbia!!

Lakini pia sio lazima ufanye mazoezi kila siku za wiki inashauriwa at least mara tatu kwa wiki kutokana na life style yako.....lakini pia mazoezi ambayo yapo recommended na watu wataalamu ni kama vile Push ups, squats, pull up, Burpees, mountain climb nk...... unaweza kuongeza na dumbbells kwa ajili ya kuongeza resistance......
View attachment 3456037
I luv dumbells na Barbells na Pulling
 
Ukiwa unakula vizuri na kunywa maji mengi ukipiga mazoezi (sports) mwili unajengeka vema na hata ngozi inanawiri kama ulikuwa mweusi utajikuta automatical unaanza kun'gaa. Ila kama hauzingatii lishe na kunywa maji mengi hapo unauchosha mwili kwa mazoezi ni sawa na kujinyanyasa.

Mazoezi si mpaka utoke nje uwanze kutembea au kukimbia unaweza kujifungia zako chumbani kama kuna nafasi. Anza kwa kuruka kamba, unapiga squater, push up, unaruka mchakamchaka yaani ni mwendo wa HOME WORKING OUT.
 
Kama hatua zako ni sawa au karibu sawa na zangu, basi hapo una wastani wa kilometa 5 hadi kumi, taken that 1step= 1meter
1000 steps =1 km
12,000 steps =10-12km
Kuna siku nilikua na app ya kuhesabu hatua simu ikiwa mfukoni, kila siku nikikuwa nafikisha hatua elfu sita mpaka nane siku nyingine mpaka elfu 12 kwa siku.
 
Unamshauri vibaya wacha acheze mpira aisee ni mazoezi mengi anafanya kwa wakati mmoja.
Tatizo kazi zetu za site mtaji wake NI afya ya miguu sasa hii NI mara ya tatu kaumia mguu anachechemea ..mara kwanza alipiga jiwe bila kujua ..imagine unakaa nyumbani week nzima inakuja activity ya geo survey maporini tunakuacha
 
Jumamosi na Jumapili naenda kutembea na kukimbia bara bara ya East Afrika umbali mrefu sana siku za kawaida nacheza mpira na timu ya vijana mtaani..
Sema ni uvivu tu ila nikikimbia mara kwa mara najiona tofauti kabisa na napotembea.
 
Tatizo kazi zetu za site mtaji wake NI afya ya miguu sasa hii NI mara ya tatu kaumia mguu anachechemea ..mara kwanza alipiga jiwe bila kujua ..imagine unakaa nyumbani week nzima inakuja activity ya geo survey maporini tunakuacha
Unaweza ukawa upo sahihi ila mpira wa miguu unachukua mazoezi mengi ambayo angefanya kwa wakati tofauti anayapata kwa wakati mmoja na pia mpira ukienda wiki hii mara mbili au tatu kama utapata nafasi unaweza usicheze tena wiki nzima ijayo na ukawa na fitness ya kutosha kama kuogelea au kucheza basketball...
 
Back
Top Bottom