Nakupenda sana baby ila kila mwezi utanipa laki tatu (3)

Nakupenda sana baby ila kila mwezi utanipa laki tatu (3)

Unaweza kumpa lakini sio kwa kujiombea tena mwanzoni kabisa.
Kumpa hata million sio tatizo, inategemea uwezo na hadhi, viwango vya mahusiano plus ubora wa binti.

Ubora wa binti ni hekima na busara, hatangulizi pesa mbele, anaonyesha uthamani wako kwake, binti akionyesha kuwa wewe ni bora zaidi kwake utampa hata nyumba.

Lakini binti anayetanguliza maslahi yake binafsi mpe 30,000 apite hivi.

Dunia hii kuna wanawake wenye akili na ndio wanaofaidi nyumba, magari na pesa.
Binti anaipandisha thamani yako balaa.
Kila wakati anataka kuwa nawe, ukipita muda kidogo anakujulia hali, mara hivi mara vile na anaonyesha amezama kwako balaa.

Anajifanya hataki chochote kwako zaidi ya wewe na penzi lako.
Si kuwa hataki pesa zako laah hasha bali amechagua FUNGU JEMA nalo ni kumpata mwenye vyake kwanza na mengine atazidishiwa.

Yaani anakuonyesha amezuzuka nawe kama vile duniani umebaki mwanaume peke yako[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mwanamke wa hivi si tu utampa laki 3 bali utampa maisha yako.
Hii siri nimewaibiwa .
Heaven Sent
Sky Eclat
Joannah

Kaka tule wa ir town yupo kund gani hapa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyu dem napishana nae kila mara hapa mtaani kwetu na kwa kuwa mimi si mtu wa story sana na washikaji hapa kitaa yaani nikitoka nimetoka nikiingia nimeingia hivyo sijazoeleka sana na watu wengi.

Sasa huyu dem kila nikirudi hua namkuta kibarazani kwao (sijui kakariri muda wangu wa kurudi home) yeye ndo huwa wakanza kunisalimu, yeye anaishi nyumba jirani.

Siku moja nikiwa kwa daladala narudi home nikakutana nae kwenye gari tukakaa siti moja, story zikaanzia hapo hadi kubadilishana no za simu.

Baada ya wiki mambo yakawa moto, mitoko ya hapa na pale n.k, hana kazi yoyote yupo yupo tu mtaani na sikutaka kumdadisi sana kujua maisha yake.

Sasa leo tukiwa tunachati kanambia kuwa ananipenda sana muda mrefu alitamani kuwa na mimi.

Nikamuuliza sababu ya kuachana na ex wake (mana alikuwa anamponda sana) akasema wameachana sababu jamaa alikuwa hamjali kwa mahitaji yake yoyote yani kifupi hamthamini.

Nikamuuliza unadhani mimi naweza kukujali na kukupa mahitaji yako yote. Akasema hapana huwezi kuwa na yote ila kwa kiasi fulani nitashukuru.

Nikamuuliza ni kipi hasa unakihitaji akasema anataka apate angalau laki 3 kwa mwezi.

Nikamuuliza kazini kwako unalipwa sh ngapi kwa mwezi hadi udai laki tatu kwa mwanaume ?

Bado hajanijibu hadi sasa.

Dada zetu naona sasa mapenzi wameyageuza kuwa ajira wanadai mpaka mishahara sasa!!
Huyo ni zwazwa eti angalau laki 3 kwa mwezi
 
Wewe kama unaweza kumpa hizo pesa mpe kama huwezi acha

Wavulana mbona hamna vifua aseee!jambo dogo kama hili umeshindwa kabisa kulimezea,tena ni same old story🙄
waliona jambo dogo sio laki 3 kila mwezi na amekaa tu
 
tatizo wanawake wanawaona wanaume wapole wakimya wasiozoeana na watu wengi mtaani kama maboya.. kumbe akili nyingi kama movies za James Bond..

na hapo sio kwamba anataka laki tatu kama laki tatu.. amesema angalau, yani hiko ndio kima cha chini kisishuke hapo.. aisee [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Unaweza kumpa lakini sio kwa kujiombea tena mwanzoni kabisa.
Kumpa hata million sio tatizo, inategemea uwezo na hadhi, viwango vya mahusiano plus ubora wa binti.

Ubora wa binti ni hekima na busara, hatangulizi pesa mbele, anaonyesha uthamani wako kwake, binti akionyesha kuwa wewe ni bora zaidi kwake utampa hata nyumba.

Lakini binti anayetanguliza maslahi yake binafsi mpe 30,000 apite hivi.

Dunia hii kuna wanawake wenye akili na ndio wanaofaidi nyumba, magari na pesa.
Binti anaipandisha thamani yako balaa.
Kila wakati anataka kuwa nawe, ukipita muda kidogo anakujulia hali, mara hivi mara vile na anaonyesha amezama kwako balaa.

Anajifanya hataki chochote kwako zaidi ya wewe na penzi lako.
Si kuwa hataki pesa zako laah hasha bali amechagua FUNGU JEMA nalo ni kumpata mwenye vyake kwanza na mengine atazidishiwa.

Yaani anakuonyesha amezuzuka nawe kama vile duniani umebaki mwanaume peke yako[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mwanamke wa hivi si tu utampa laki 3 bali utampa maisha yako.
Hii siri nimewaibiwa .
Heaven Sent
Sky Eclat
Joannah
Mmmmh

We unaota wewe[emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom