Nakusudia kuandika kitabu kuelezea UDIKTETA wa Magufuli

Kitabu kitaandikwa iwapo utatueleza wewe ni me au ke!
 
Copy ya kwanza kabisa nanunua mimi
 
Utaandika na mazuri yake au mabaya tu?
 
Andika Tu
 
Usisahau kuandika kingine kuhusu Masters of theft and embezzlement!!!
 
Magufuli ataibuka shujaa kwa vizazi vingi sana vijavyo kupitia huo udikteta, Maana;
1. Ye ni kiongozi wa pili katika miaka 60 ya uhuru kununua ndege mpya toka zile zilizonunuliwa enzi ya Nyerere.

2. Ndie mtu aliyehakikisha umeme unafika karibia asilimia 90 ya vijiji vyote Tanzania tena kwa gharama ya TZS 27000 tu.

3. Ni katika kipindi chake toka uhuru ndipo tembo walizaliana kwa wimbi na kuishi bila hofu, mauaji ya albino na vikongwe yalikoma.

4. Ndie kiongozi aliyejitolea kulinda rasilimali za nchi ikiwemo madini na wanyama kwa maslahi ya wote bila kujali ataumiza wanaccm wenzake au watu waliomsaidia kufika hapo.

5. Tofauti na nchi nyingine wakati wa covid, udikteta wa Magu ulisaidia kuokoa vifo vingi vilivyotokana na presha, visukari, uzito mkubwa na njaa kwa kuzuia lockdown na kufanya maisha yaendelee kama kawaida. Maana kungekuwa na lockdown ingekuwa shida kupata huduma za afya na chakula.

6. Ndiye aliyeanzisha ujenzi wa bwawa la umeme la mwl nyerere miaka zaidi ya 50 toka plan ilipotengenezwa.

Yapo mengi mno ambayo udikteta wa magu ulisaidia kufanikisha kwa kipindi kifupi mno.
 
Kama hautakuwa na double standard usisahau kuandika haya.

Dkt Ulimboka alivyong'olewa meno na kucha kwa kupambania maslahi ya madaktari.

Mwangosi alivyolipuliwa mabomu pale Nyololo Mufindi kwa kosa la kuhoji kuhusu kuzuiwa kwa mikutano ya Chadema, wakati ya CCM ikiendelea.

Utuambie na wale waliolipua mabomu pale Arusha kwenye mkutano wa Chadema wakafa watu.

Waliommwagia tindikali aliyekuwa mmiliki wa gazeti la mwanahalisi.

Waliomteka mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Kibanda.
 
Naongezea tu, maisha mazuri au mabaya yanategemea na mtawala aliyopo ikulu, kwahiyo kuchezea sanduku la kura ni kuchezea maisha yako.
 
Kitabu kitamhusu Magufuli na matukio ya udikteta aliyoyafanya ktk awamu yake
 
TUTAKUUNGA MKONO

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Niliwashauri CdM Leo huko Twitter nawe umesikia sauti yangu.

Bora kiandikwe kitabu kuliko kusema kila siku matendo yake.

Wazungu wangeandaa hadi movie
Kama wataalamu wanavyoendelea kuandal eventual docs ya Ukraine na urusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…