Nakuwa na maamuzi ya kusitasita kuolewa tena tangu ndoa ya kwanza inishinde 2021

Yaani pointi moja kubwa sana! Ukiona ndugu wa upande mmoja hawakubaliana na ndoa yenu, hiyo ndoa haitadumu!! Kutakuwa na vita na uchonganishi sio wa nchi hii! Watahakikisha hiyo ndoa inakufa!! Take care!!

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Ndoa ngumu mkuu,Mwenyezi Mungu awapambanie sana.Asante sana
Hapa namjibu mtu aliyeuliza kuwa mliona red flags na bado mkaoana? Ni hivi: Mtu kama hajaingia kwenye ndoa hawezi kujua mambo mengi. Kuna viashiria unaweza kuviona kabla hamjafunga ndoa ukavipuuza lakini baada ya ndoa ndiyo vinakuwa dhahiri na unavikumbuka. BTW hata mimi ni me na nimepitia sokomoko kama ulizopitia hivyo nakuelewa sana. Ushauri wangu ni kuwa chukuwa muda kumsoma. Usiogope kuchewa. Bora hata muwe marafiki kwa miaka miwili ili kupimana.
 
Ni kweli Kabisa mkuu
 
Ukitaka udumu na huyo mchumba wako wa sasa hakikisha hao watoto wako uliowapata katika ndoa yako ya kwanza hawakai na nyie (mumeo na wewe).

Kwakuwa umri wako umesonga (naamini hivyo) kutokana na maelezo yako kuwa ulishaolewa ukatalikiana na x wako, basi tumia hili kama sehemu ya kujifunza na kujirekebisha kwa yale unayojua ni wazi hayafai kumfanyia mwenza wako.
 
Masingo maza nawaomba muachane na habari ya kuolewa, muendelee kuwa mali yetu sote. Tuendelee kuwafaidi zamu kwa zamu[emoji2][emoji2]
 
Sikuzote sipo nao
 
Za asubuhi mwanangu wa kiroho?naona unamwaga madini!hakika ndoa ni baraka kutoka Kwa Mungu naungana nawe kikubwa aingie na amani na imani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…