molwe
JF-Expert Member
- Jan 10, 2015
- 416
- 440
Yaani pointi moja kubwa sana! Ukiona ndugu wa upande mmoja hawakubaliana na ndoa yenu, hiyo ndoa haitadumu!! Kutakuwa na vita na uchonganishi sio wa nchi hii! Watahakikisha hiyo ndoa inakufa!! Take care!!Yeah, nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....
Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana, talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.
Nina watoto wawili, nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu[emoji24]
Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.
Majibu yote napokea ndugu zangu[emoji1431]
Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app