Alipohoji Gwajima , Amenusurika kutekwa, Kafungiwa Kanisa, Wamefreeze accounts zake za Bank.
Alipohoji MPINA, amekatwa Jinakwa Maneno ya RAIS.
Alipohoji MH POLEPOLE, Dada yake ametekwa, anatafutwa ni wapi alipo, naamini wakimpata tu ni Ama Kumuua au kumpa Kesi kubwa.
Amewahi Ongea Mzee Warioba, wakamumsumbua sumbua.
SASA KAONGEA MZEE BUTIKU, MWENYEKITI WA KIGODA CHA MWALIMU NYERERE.
Hofu yangu sanasana, ni juu ya UHAI wa Hawa wazee wetu wawili Wazalendo wakuu wa Taifa hili, Mzee Butiku, Mzee Warioba .
Kwa namna Genge la Utekaji na Uuaji lisivyokua na Aibu, huku Afande Muliro akisema Wanatekwa ni sababu ya Ushirikina na Mapenzi , Basi Maisha ya Mzee Butiku na Mzee Warioba mpaka Sasa yako hatarini.
Yako hatarini Kwa sababu ndio Wazee pekee waasisi wa Tanzania yetu ambao Kwa pamoja bila kupepesa macho, wamekea Utekaji, wamekemea Utaratibu wa Rais Samia kujiteua.
Ni Rai yangu, JWTZ itachukua Jukumu la kuhakikisha Usalama Wazee Hawa.