Naliona anguko la Diamond linakuja kwa kasi

Naliona anguko la Diamond linakuja kwa kasi

Na wakumbuke pia godfather ameshatengeneza video za watu kadhaa

Alikiba - Mwana
Linah - No stress, olethemba
Yamoto - Cheza kwa madoido

Ila kwanini za Diamond pekee ndio zinakuwa zinatisha sana, na kupata mafanikio makubwa zaidi??

1) Diamond anapokuwa anashoot video, uandishi wa script huwa anahusika saana..! Na kutokana na yeye kutumia lugha ambayo Godfather haifahamu huwa anafanya zaidi ya kumpa idea ya wimbo. Uunganishaji wa matukio n.k Ndio maana kila la muhimu kwenye video huwa linawekwa, kiasi kwamba hata asiyejuwa lugha na yeyote asiye na uwezo wa kusikia anapata kitu pindi atapoiona tu video...!!

2) Diamond ni booonge moja la actor. RIP Kanumba, Diamond siku moja aliconfess kuwa anamkubali sana na vitu vingi sana alikuwa anaiga kwake (tofauti na Sharuh Khan) .. Huyu jamaa huwa anauvaa uhusika vilivyo.

JE UTANIPENDA??
King Of Afropop...

Kula "like" kaka kwa ufafanuzi zaidi japo watajifanya hawaelewi lkn kimoyomoyo wanakubali
 
Wale wanaotabiri anguko la Diamond hawako sawa. Diamond kama msanii hawezi kuwa juu milele hata Amerika wasanii kama akina R.Kelly game inawakimbiza. Kitu muhimu cha kuzingatia ni kwamba Diamond ameplay part yake katika kuusogeza mziki wetu mbele hivyo atakapoishiwa itakuwa ni jukumu LA msanii mwengine kuendelea kuusogeza mbele mziki wetu. Wale wanaomshabikia Akikiba watasubiri sana maana muda wake ulishapita na aliplay part yake angalau Afrika Mashariki mziki wetu ulisogea, Diamond ameupeleka mbele zaidi hivyo aje mwengine ausogeze zaidi pengine mpaka America.
 
Wale wanaotabiri anguko la Diamond hawako sawa. Diamond kama msanii hawezi kuwa juu milele hata Amerika wasanii kama akina R.Kelly game inawakimbiza. Kitu muhimu cha kuzingatia ni kwamba Diamond ameplay part yake katika kuusogeza mziki wetu mbele hivyo atakapoishiwa itakuwa ni jukumu LA msanii mwengine kuendelea kuusogeza mbele mziki wetu. Wale wanaomshabikia Akikiba watasubiri sana maana muda wake ulishapita na aliplay part yake angalau Afrika Mashariki mziki wetu ulisogea, Diamond ameupeleka mbele zaidi hivyo aje mwengine ausogeze zaidi pengine mpaka America.
Bora uwaeleweshe maana watu wanajifanya hawaelewi sasa ni zama za Diamond Na yeye wakati Wake utafika atapita watakuja wengine jamani khaa maana anguko anguko ataanguka mungu akitaka si nyie binadamu looh!
 
Inawezekana ikawa unaufahamu muziki lakini unaonekana huifahamu tasnia ya muziki! Kwa bahati mbaya sana; dunia ya leo wanaofanya vizuri ni wale ambao; cha kwanza kabisa wanaifahamu tasnia ya muziki na ndipo linapofuata suala la kuufahamu muziki!

AGAIN: Tofautisha kati ya Music and Music Industry! Kabla hamjahangaika kupiga ramli, mnatakiwa kwanza kuifahamu tasnia ya muziki na sio kujigamba kuufahamu muziki wakati tasnia hamuijui.....

Unaongeaga point hadi unakeraa..!!
 
Zinga la emotional song inagusa wanaoponda wametanguliza chuki mbele
 
Tukiachana na ushabiki Diamond siku hizi kaishiwa kabisa no ubunifu yaan ukisikiliza nyimbo anazotoa siku izi na zile za kitambo kuna utofauti mkubwa mno coz siku izi anatoa nyimbo mbovu sana na kinachombeba na kuendelea kusikika ni kuwa na fan base kubwa na video za god father lasivyo...?

je utanipenda?..hii post ifute mara moja
 
Mambo yake imeishaisha kitambo. Bado kidogo ajiunge na TOT aanze kuimba nyimbo za CCM
 
Wabongo bana...

Nakumbuka nikiwa shule ya msingi, kuna kabinti karembo kalikuwa kanaitwa Betty, alikuwa anaonyesha kila dalili kuwa ananipenda/ananikubali....kwa mfano, ilikuwa nikiingia darasani anashtuka na kusogea kwenye deski ili nikae( kwa anayejua madeski yetu yale ya watatu watatu)...nikichapwa atatafuta muda na kuja kuniambia pole sikioni....akinunua kashata mbili basi ataniletea moja...nakumbuka siku moja tulikuwa na kesi ya kutodeki darasa....akawataja watuhumiwa na kuniacha mimi ingawa nami sikutokea kwenye kazi ile... na kadhalika.

Lakini cha ajabu ilikuwa mtu akimwambia Fyatu ni mchumba wako analia, kama si kuanzisha ugomvi, au kwenda kushtaki kwa mwalimu.

Mpaka tunaachana darasa la nne (nilihama shule) sikuwa nimemuelewa...na labda naye hakunielewa...I dont know.

Nilikuja kumuhadithia mtu siku moja akaniambia neno moja tu "action speaks louder"
 
Huu wimbo kiukweli jaman tuache na ushabiki mhhh mie kwangu big NO
huu unafki siupendi.akitongozwa dadaako unakasirika siku akiolewa unavaa suti.
sasa hapa unaukataa.akizoa tuzo na wimbo huo utasifia!unafki!
 
Huu wimbo sio wa Mike T kweli? "JE UTANIPENDA"
Dah, hivi ni Kweli mpaka anaandika, anafanyia mazoezi na marekebisho na kwenda ku record hakukumbuka Kama mwenzie alishaandika na kuimba huo wimbo.... ??? Kuna Wakati Q chief aliwahi kulalamika kua dogo anatembelea nyota Yake nikajua ni kutapata tu, Ila sasa naelewa.
 
Back
Top Bottom