Nalipa kodi TRA zaidi ya milioni tatu kwa mwezi, ni hasira sana ninapokuta umeme umekatika nyumbani

Pole mkuu na mbaya zaidi hizo fedha zinaenda kujenga magorofa ya TRA officer's!,President Jimmy Carter anaishi kwenye nyumba ya 210,000usd, shopping yake kwenye store ya jirani, TRA ofisa anaishi nyumba ya 500k usd, shopping yake Dubai, china, Mall of Africa!!,subiria kupangwa maana hutaki kujipanga mwenyewe
 
Pole sana Mkuu.

ADHA YA UMEME INATUTESA WATANZANIA WOTE, SERIKALI INABIDI ITAFUTE SULUHISHO LA KUDUMU (TUMECHOKA).

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Hilo la umeme cha mtoto, kubwa kuliko ukilipa tu yafuatayo hutokea:Baba /mama Mmoja afisa wa serikari anatoka Nyumbani kwake , familia inamuaga kwa bashsha na Upendo, anaingia ndani Land cruiser LC, dereva anauelipwa na serikali anamiendesha hadi ofisini kwake. Wafanyakazi wa ngazi ya chini wanmwamkia kwa adabu za uoga, anaingia ofisini kwake na kujifungia!

Mbwembwe zote hizo utafikiri anenda kufanya jambo la maana! Kumbe anaishia kumwagiza muhasibu ahamishe fedha ulizolipa na kuzipeleka kwenye mafungu ambapo zitapigwa kwa invoice feki zenye tarakimu nyiingi na hatimaye zitamfikia baadaye .

Kulipa Kodi hapa Tz ni Moja kati ya mambo yanayoleta stress kubwa kwa mlipa Kodi, si kwasababu hatutaki kulipa , bali kwasababu hata tukilipa tunajua zitapigwa na viongozi walafi waliovaa suti na matumbo yao makubwa. Hii nchi ngumu sana.
 
Tofautisha kulipa kodi na kulipa bili ya umeme. Kuna viwanda vinalipa kodi ya mabilioni na wana genereta.

Tulia..3m unafoooka...we vipi?

Hujui tofauti ya TRA na TANESCO ?
 
Mkuu, tumia ID yako kongwe ili wakushambulie kwa ufasaha zaidi.

3m kama kodi, hajasema kama ni kutoka kwenye mshahara au biashara ILA vyovyote vile, inaonesha ni mtu mwenye kipato kikubwa cha halali, akijipanga, jenereta sio issue kwako.

Kwako wewe sasa, inawezekana hiyo kodi anayolipa mwamba, ni kipato chako cha miezi 3 lakini unajaribu kubeza hapa kwa kufuata mkumbo wa ki-JF
 
Tumien solar
 
wewe sio mzima kichwani ukapimwe
 
Mkuu, tumia ID yako kongwe ili wakushambulie kwa ufasaha zaidi.

3m kama kodi, hajasema kama ni kutoka kwenye mshahara au biashara ILA vyovyote vile, inaonesha ni mtu mwenye kipato kikubwa cha halali, akijipanga, jenereta sio issue kwako.

Kwako wewe sasa, inawezekana hiyo kodi anayolipa mwamba, ni kipato chako cha miezi 3 lakini unajaribu kubeza hapa kwa kufuata mkumbo wa ki-JF
Tufanye simple calculations yaani pato lake(a) mara 18% ni sawa na milioni 3
18a/100=3,000,000
18a=300,000,000
A=kama milioni 16 hivi.

Sasa unatak kusema ngumu kuingiza milioni 16 ama 17 kwenye biashara yake mbona wengi tu pato hilo linapatikana kwa biashara nyingi kuanzia hardware etc.

Milioni 17 kwa mwezi ni mauzo ya kama laki 6 hivi kasoro kwa siku. Ni kawaida sana mkuu, kuna watu wengi biashara zao kwa siku wana mauzo ya milioni mpaka milioni 5
 
Pole mkuu na mbaya zaidi hizo fedha zinaenda kujenga magorofa ya TRA officer's!,President Jimmy Carter anaishi kwenye nyumba ya 210,000usd, shopping yake kwenye store ya jirani, TRA ofisa anaishi nyumba ya 500k usd, shopping yake Dubai, china, Mall of Africa!!,subiria kupangwa maana hutaki kujipanga mwenyewe
Nina ndugu yangu yupo TRA, miaka minne ya kwanza akawa amejenga nyumba tatu za maana sana hapa dar. Niliacha kabisa kuwa karibu naye maana ni mwizi wa mali za uma.
 
Pole sana Mkuu.

ADHA YA UMEME INATUTESA WATANZANIA WOTE, SERIKALI INABIDI ITAFUTE SULUHISHO LA KUDUMU (TUMECHOKA).

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Hawa viongozi ni dhaifu sana kwakweli maana umeme wala sio teknolojia complex kwenye kuuzalisha.
 
Hilo la umeme cha mtoto, kubwa kuliko ukilipa tu yafuatayo hutokea:Baba /mama Mmoja afisa wa serikari anatoka Nyumbani kwake , familia inamuaga kwa bashsha na Upendo, anaingia ndani Land cruiser LC, dereva anauelipwa na serikali anamiendesha hadi ofisini kwake. Wafanyakazi wa ngazi ya chini wanmwamkia kwa adabu za uoga, anaingia ofisini kwake na kujifungia!

Mbwembwe zote hizo utafikiri anenda kufanya jambo la maana! Kumbe anaishia kumwagiza muhasibu ahamishe fedha ulizolipa na kuzipeleka kwenye mafungu ambapo zitapigwa kwa invoice feki zenye tarakimu nyiingi na hatimaye zitamfikia baadaye .

Kulipa Kodi hapa Tz ni Moja kati ya mambo yanayoleta stress kubwa kwa mlipa Kodi, si kwasababu hatutaki kulipa , bali kwasababu hata tukilipa tunajua zitapigwa na viongozi walafi waliovaa suti na matumbo yao makubwa. Hii nchi ngumu sana.
Huwa simuelewi kabisa mtu anayekwenda ofisini na anapokea mshahara wa kodi za raia wenzake masikini huku akijua kabisa hakuna value yoyote anayowapatia.

Nchi hii kwa hali ilivyo, haikupaswa kiongozi yoyote atumie gari linalozidi milioni 50.
 
Tofautisha kulipa kodi na kulipa bili ya umeme. Kuna viwanda vinalipa kodi ya mabilioni na wana genereta.

Tulia..3m unafoooka...we vipi?

Hujui tofauti ya TRA na TANESCO ?
Ficha ujinga wako. Unafahamu kwamba serikali inatoa mabilioni mangapi kwa mwaka kulipia uendeshaji wa tanesco?
 
inaonesha ni mtu mwenye kipato kikubwa cha halali, akijipanga, jenereta sio issue kwako.
Umeme wa tanesco una raha yake maana unawasha chochote nyumbani. Generator zile nzuri zenye silencer ni gharama sana kuzinunua kwa matumizi ya nyumbani, labda iwe kwenye biashara.

Generator hizi ndogo ukiziwasha ni kelele mtaa mzima na kusumbua majirani huku umeme wake hauwashi hata ac.
 
Tofautisha kulipa kodi na kulipa bili ya umeme. Kuna viwanda vinalipa kodi ya mabilioni na wana genereta.

Tulia..3m unafoooka...we vipi?

Hujui tofauti ya TRA na TANESCO ?

Huyu anaongea utumbo gani hujii kodi zinalipwa ili iweje ? Au
 
Tufanye simple calculations yaani pato lake(a) mara 18% ni sawa na milioni 3
18a/100=3,000,000
18a=300,000,000
A=kama milioni 16 hivi.

Sasa unatak kusema ngumu kuingiza milioni 16 ama 17 kwenye biashara yake mbona wengi tu pato hilo linapatikana kwa biashara nyingi kuanzia hardware etc.

Milioni 17 kwa mwezi ni mauzo ya kama laki 6 hivi kasoro kwa siku. Ni kawaida sana mkuu, kuna watu wengi biashara zao kwa siku wana mauzo ya milioni mpaka milioni 5
Chukua hizo hizo hesabu, nenda nazo kwenye population, kisha uniambie kama wako wengi wa kipato halali hicho, kwa wingi huo unaousema, TAKWIMU ya kuwa NCHI MASIKINI kwa kiwango cha kuishi chini ya Tzs 2,400 kwa siku inatokea wapi?

Kwa mujibu wa TRA, TZ ilifikia/ipo hatua ya kukusanya tzs 2trln kwa mwezi kama kodi. Hii ni wastani wa tzs 32,260 kwa kila mtanzania kwa mwezi.

Kumaanisha, average kipato kwa hesabu ifafanayo na yako(18%) kwa kila mtanzania ni tzs 179,222 kwa mwezi.

Sasa huoni inatisha kama average inamshusha Mo, Bakhresa pamoja na wezi wote wakijani na wa kimtamdao, mpaka kwenye kipato cha tzs 179,000 kwa mwezi?

Hao wengi wenye kipato halali cha mpaka 5m kwa mwezi ni wangapi kati ya 6m population ya watu wa Dar? Tuanzie hapo kwanza!
 
Back
Top Bottom