Nimefurahishwa na kitendo cha Jeshi la Polisi kutimiza wajibu wake bila upendeleo.
Leo kwenye hadhara ya kutafuta wadhamini, mgombea urais kwa tiketi ya chadema, Bw. Tundu Antipas Lissu akiwa mkoani Morogoro, askari wa Jeshi la Polisi walionekana wakiimarisha ulinzi na kuhakikisha Bw. Tundu Antipas Lissu anakuwa salama muda wote.
Mpaka hadhara inaisha, amani ilikuwa imetamalaki na hakuna vurugu zozote zilizotokea.
To be honest; from the bottom of my heart nalipongeza jeshi la polisi kwa
fairness ya leo. Natamani na maeneo mengine ambayo bado Bw. Tundu Antipas Lissu hajapita, polisi waonyeshe
fairness kama walioonyesha polisi wa Morogoro.
Kama hali ikiendelea hivi; uchaguzi utakuwa huru na wa haki na amani itazidi kudumu katika taifa letu.
Mungu awabariki polisi wote