saidi kindole
JF-Expert Member
- Sep 21, 2012
- 310
- 792
Jecha Salim Jecha amejitokeza kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais visiwani humo kwa tiketi ya CCM.
Jecha amewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na vilevile aliwahi kugombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni.
Maoni yangu:
Vuta tafakuri hawa wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi watatenda haki kweli? Kwani wote ni makada ukimjumlisha na yule alieteuliwa jana.
UPDATES
ZANZIBAR: JECHA SALUM JECHA AREJESHA FOMU YA URAIS
Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Uchaguzi Visiwani humo (ZEC), Jecha Salum Jecha amekamilisha utaratibu wa kupata wadhamini 250 na kurejesha fomu katika Ofisi Kuu ya CCM iliyopo Kisiwandui
Jecha anakuwa mgombea wa 24 kurudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais visiwani #Zanzibar
Mwaka 2015 akiwa Mwenyekiti wa ZEC, Jeche alifuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 akidai ulijaa kasoro nyingi na kufanya Uchaguzi huo kurudiwa