Zanzibar 2020 Namba 14: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar. Arejesha fomu hiyo


Hii inathibitisha bila shaka yoyote kwamba watumishi wa Tume ya uchaguzi ni wanaCCM na kwa wao kusimamia uchaguzi ni kinyume cha katiba ya nchi....
Mahakama, Bunge na vyombo vyote vya dola na habari katika nchi zenye Tawala za kidikteta ndivyo zilivyo,huhakikisha wote wanaimba nyimbo za kusifu na kuabudu utawala au yeye binafsi.

Wakuu wa taasisi zote huwa ni lazima wawe ni watu walio karibu na mtawala,vyama vya siasa vinakuwa ni mwavuli tu.
Tanzania sasa ipo katika stage za mwisho kukamilika kuwa nchi ya kidikteta.
 

Dear Erthrocyte
Siku zote nazipenda sana post zake. unasema kweli sana na Allah akuzidishie. Huyo nduli jecha salum Jecha hakustahiki kuchukua fomu ya urais.

Nafkiri Mahakama ingeweka kipengele cha mtu yoyote aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi hastahiki kugombea nafasi ya urais. Akiruhusiwa huyu firauni alolaaniwa na Allah nitajuwa kuwa Tanzania tunayo safari refu kama taifa. Allah amwangamize Jecha salum Jecha
 
Jecha huyu huyu angekuwa ameenda kuchukua fomu kupitia Chadema au chama kingine cha Upinzani mngefurika hapa na kudai CCM imeisha kwa sababu Jecha kawaletea siri za kushinda uchaguzi.

Wanasheria mtusaidie kipande hiki kutoka katika katiba ya Zanzibar

119 (3) Watu wafuatao hawataweza kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi yaani:
(a) Waziri au Naibu Waziri;
(b) Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi au ikiwa ni miongoni mwa majeshi ya Tanzania au ana wadhifa wowote
ambao kisheria haruhusiki kuwa mjumbe wa Tume;
(c) Mbunge au mtu mwengine mwenye madaraka ya aina yoyote aliyotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa
mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya Ibara ya 67 ya Katiba ya Muungano;
(d) Kiongozi wa chama chochote cha Siasa.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengine ya kifungu hiki, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi atasita tu kuwa Mjumbe litokeapo
lolote kati ya mambo yafuatayo:
(a) ukimalizika muda wa miaka mitano tangu alipoteuliwa; au
(b) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mjumbe ligemfanya asiweze kuteuliwa kuwa Mjumbe wa

Tume ya Uchaguzi.

Maswali yangu
  1. Je Jecha aliwahi kuwa uongozi, madaraka au sifa yoyote iliyotajwa katika vipengere tajwa hapo juu 119(3)?
  2. Je Jecha hajatimiza masharti ya vipengere tajwa 119(4)
 
Amina
 
Sasa baada ya Ibara hiyo nzuri tuletee ibara inayoeleza sifa za ofisa wa Tume ya uchaguzi
 

Pengine amejitokeza kutokana na sababu za kimkakati. yawezekana amemambiwa achukue fomu. hatuwezi jua
 
Kuchukua fomu ya kugombea Urais kwa Jecha Salum Jecha kupitia CCM ni doa kwa Tume zetu za Uchaguzi. Maafisa wote wa tume hiz ni makada wa CCM. Ni ngumu mno kama kupika upinzani wa Tanzania kushika dola.
 
Anayo haki kama walivyo raia wengine. Lakini kwa kashfa aliyo nayo angetumia busara ya kupumzika tu.
 
Anayo haki kama walivyo raia wengine. Lakini kwa kashfa aliyo nayo angetumia busara ya kupumzika tu.
Mkuu, Jecha hata kama asingekua na kashfa yoyote, kwa nafasi aliyowahi kushika kwa mtu mwenye maadili na kujiheshimu wala hakupaswa kuchukua fomu kwa tiketi ya chama chochote.

Hii ni dosari kubwa ya kimaadili katika nchi nyingi za kiafrika ambapo Jaji wa Mahakama ya Rufaa anaweza kuonyesha mahaba yake kwa chama fulani cha siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…