Uchaguzi 2020 Namba 3: Lazaro Nyalandu achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, asema watahakikisha mechi wanaipeleka sawasawa

Uchaguzi 2020 Namba 3: Lazaro Nyalandu achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, asema watahakikisha mechi wanaipeleka sawasawa

Lumumba mtaongea lugha zote mwaka huu. Kwa kifupi mwaka huu upinzani wanawaletea mtu msiyemjua ambaye hamjawai kuwa nae. Mtu makini Mwenye roho ya ujasiri, si mwingine ni TUNDU ANTIPASS LISSU.

Mtaleta thread zote mwaka huu ila mjue tu msiyempenda ndo huyo kaja. Ni TUNDU ANTIPASS LISSU.
Raisi wa mashoga
 
Lazaro Nyalandu yuko live Clouds tv akiweka wazi mipango yake endapo atachaguliwa kuwa Rais wa JMT.

Maendeleo hayana vyama!
=======

Nyalandu: Mbowe ni mtu ambae amestahimili, amepambana na amekuwa muaminifu kwa chama hiki. Amekuwa ni kiongozi ambae ni mfano wa kuigwa na historia itamkumbuka kwamba ni mtu aliekipigania chama kuanzia ujana wake.

Usiku mmoja tulikuwa tumelala kwenye hoteli moja inayojulikana kama King David Hotel iliyoko katika mji mkuu wa Yerusalem. Mimi na Mbowe majira ya saa sita usiku tukasema tukatembelee eneo linajulikana na Waislam kama msikiti wa Suleyman na kwa wayahudi kama eneo takatifu lililojengwa na Suleyman, twende usiku wa manane na nakumbuka tulitafuta Taxi wakati huo uber hamna.

Mahali ambako kuna haki kila mtu atakuwa na amani, mfumo wa utoaji utahitaji maboresho makubwa, mwananchi yeyote anaweza akashtakiwa kwa kosa ambalo Jamhuri inaona ametenda. Mwananchi huyo bado hana hatia mpaka mahakama itakapomtia hatiani.

Kwa hiyo habari za watu amekutwa na kosa alafu anakaa keko, anakaa kizuizini mwaka wa nne, habari hizo zitakuwa ni historia ya kusikika. Hatutawaweka watu kizuizini wawe wanaCCM au wanaCHADEMA, tutataka haki na mifumo iwe sawa kwa watu wote.

Yeyote atakaeteuliwa na chama tutamuunga mkono, tunaweza tukashinda kama tutakuwa wamoja.

Tutahakikisha tunaipeleka hii mechi sawasawa, magoli tutafunga asubuhi, mchana. Hakuna goli la kisigino na niwahakikishie watanzania ambao wameingiwa na hofu, mtanzania anatembea anaona jani limedondoka anadhani nyoka anageuka. Naomba niwaambia saa ya kuondoa woga ndani ya nyoyo zetu, ndani ya nchi yetu imefika.

Hofu huua creativity, mtoto akiingiwa na hofu, maono yake yanakufa. Tuondoe hofu. Uchaguzi utakuwepo, hakuna ambae atapitishwa kwa sababu mtu mmoja amesema atapitishwe, niwahakikishia nchii hii ina mkubwa ambae anaitwa Mungu alie hai, nchi hii ina mwenyewe.

Mwanamuziki wa Kenya amesema muombee jirani yako aishi muda mrefu ili unapobarikiwa ajionee mwenyewe. Ni matamanio yangu, wakati niko CCM tulikuwa tunaimba wacha waisome namba. Hatutaki mtanzania yeyote aisome namba yoyote zaidi ya namba ya heri ya Tanzania.

CHADEMA ikichukua madaraka, ijiandae kukosolewa na wale wanaoikosoa warudi nyumbani wakalale salama kwa sababu katika kukosoana tunaandaa taifa lililo bora.

Katika mandhari mpya ya CHADEMA tukishirikiana na wengine, tutamruhusu kila mtanzania astawi tena, talanta zistawi tena, tukalijenge upya taifa ambalo alikuwa na maono nalo baba wa Taifa.

Hata Mobutu alikua anasema hivi hivi pia
 
Kaongea vizuri Nyalandu yuko perfect kichwani.
Mr Nyalandu leo nimemuaminia. His ideas are very constructive,kiasi kwamba unasikia mwili kusisimka na kuitamani kuiona Tz ya hivo. Mungu ni mwema atatenda haki na umoja ni nguvu siku zote.
 
Kiukweli Nyalandu kaongea point nyingi sana leo
 
Ni makosa kukata tamaa mapema kabla ya mechi lakini sioni Tume hii ikimtangaza mtu mwingine yeyote zaidi ya Magufuli. Tume hii sio huru na inaongozwa na mwana CCM na matokeo ya urais hayapingwi popote hata kama kuna wizi wa wazi kabisa.

Chadema wanaweza kuendelea na michakato yao kama takwa la demokrasia lakini pia katika ile kuleta hamasa na kusaidia wabunge wa upinzani wengi zaidi wachaguliwe. Ili hili lifanikiwe, mgombea wao apatikane fairly and squarely na mtu yeyote asishinikize kupitishwa yeye/rafiki yake.
 
Ni makosa kukata tamaa mapema kabla ya mechi lakini sioni Tume hii ikimtangaza mtu mwinginte yeyote zaidi ya Magufuli. Tume hii sio huru na inaongozwa na mwana CCM na matokeo ya urais hayapingwi popote hata kama kuna wizi wa wazi kabisa.

Chadema wanaweza kuendelea na michakato yao kama takwa la demokrasia lakini pia katika ile kuleta hamasa na kusaidia wabunge wa upinzani wengi zaidi wachagulie. Ili hili lifanikiwe, mgombea wao apatikane fairly and squarely na mtu yeyote asishinikize kupitishwa yeye/rafiki yake.
Sio vibaya kukata tamaa mapema tu ila ni kosa kubwa sana kukata tamaa wakati wowote. Unapokosa utakacho ni hatua moja mbele ya kukipata utakacho.
 
Sawa, tunamtakia Mnyampaa Nyalandu kila la heri kwenye uwendawazimu uliomuingia!!

huyu mnyampaa ni mtu hatari manake kuna stori kuwa wakati akiwa sisiem wale waliokuwa tishio kwake waliogombea nae kura za maoni kuchaguliwa kugombea ubunge kwa ticket ya sisiem kuna wengine walilamba udongo huko Singapore!!

hivi kama si ukichaa ninini? mtu mzima msomi kama Nyalandu unaacha cheo kizuri cha level yako yaani ubunge unavamia urais ambao ni oversaiz? pumbavu kabisa huyu! watu wanauana kutafuta ubunge ye anaacha! ni mtu mwenye dharau sana!!

hivi kwa kazi alizofanya Magufuli , Rais anaekubalika Dunia nzima kwasasa unaanzaje japo kufikiria kwa mbali kupambana nae? si ukichaa huo!! Yaani Francis Cheka akazipige na Tyson yule wa wakati ule hiyo ni akili au matope!!

Kwanza sijui kwanini Nyalandu yuko huru na twiga wetu aliuza Dubai wakiwa hai na hajui hadi sasa tumekosa watalii wangapi wa twiga??huyu ni kiongozi mwenye ubinafsi sana na mpumbavu, hana uchungu na nchi hii!!

Namuonea huruma sana Nyalandu sababu ameshashindwa na Magufuli kabla mbio hazijaanza!!na hajijui!!

Nimwambie ukweli tu Nyalandu na aweke kichwani kuwa unapodhani una akili na sifa za kuendesha mambo zaidi ya boss wako alie madarakani ambae hakwambii purukushani anazopambana nazo basi daima huwezi kuwa na cheo cha boss huyo!!!

he should know and accept that he will never be a president kwakuwa anajiona yeye ni mtu mwenye akili kuliko watu wote bongo kumbe hata ‘Slow times two’ kamzidi kiakili mbali kabisa kwenye siasa hizi za majitaka na kuchafuana!!

zama hizi chama kilianza kufa wakaja na mbinu za kisasa kwanza nunua, akikataa piga katafunua, akiendelea kubisha vunja miguu na mikono akiendelea kupinga juhudi piga risasi akipona mdake mpoteze huku miradi mikubwa ikikonga mioyo ya wapiga kura na bao la mkono at work, Nyalandu atapita njia gani?
 
Lazaro Nyalandu yuko live Clouds tv akiweka wazi mipango yake endapo atachaguliwa kuwa Rais wa JMT.

Maendeleo hayana vyama!
=======

Nyalandu: Mbowe ni mtu ambae amestahimili, amepambana na amekuwa muaminifu kwa chama hiki. Amekuwa ni kiongozi ambae ni mfano wa kuigwa na historia itamkumbuka kwamba ni mtu aliekipigania chama kuanzia ujana wake.

Usiku mmoja tulikuwa tumelala kwenye hoteli moja inayojulikana kama King David Hotel iliyoko katika mji mkuu wa Yerusalem. Mimi na Mbowe majira ya saa sita usiku tukasema tukatembelee eneo linajulikana na Waislam kama msikiti wa Suleyman na kwa wayahudi kama eneo takatifu lililojengwa na Suleyman, twende usiku wa manane na nakumbuka tulitafuta Taxi wakati huo uber hamna.

Mahali ambako kuna haki kila mtu atakuwa na amani, mfumo wa utoaji utahitaji maboresho makubwa, mwananchi yeyote anaweza akashtakiwa kwa kosa ambalo Jamhuri inaona ametenda. Mwananchi huyo bado hana hatia mpaka mahakama itakapomtia hatiani.

Kwa hiyo habari za watu amekutwa na kosa alafu anakaa keko, anakaa kizuizini mwaka wa nne, habari hizo zitakuwa ni historia ya kusikika. Hatutawaweka watu kizuizini wawe wanaCCM au wanaCHADEMA, tutataka haki na mifumo iwe sawa kwa watu wote.

Yeyote atakaeteuliwa na chama tutamuunga mkono, tunaweza tukashinda kama tutakuwa wamoja.

Tutahakikisha tunaipeleka hii mechi sawasawa, magoli tutafunga asubuhi, mchana. Hakuna goli la kisigino na niwahakikishie watanzania ambao wameingiwa na hofu, mtanzania anatembea anaona jani limedondoka anadhani nyoka anageuka. Naomba niwaambia saa ya kuondoa woga ndani ya nyoyo zetu, ndani ya nchi yetu imefika.

Hofu huua creativity, mtoto akiingiwa na hofu, maono yake yanakufa. Tuondoe hofu. Uchaguzi utakuwepo, hakuna ambae atapitishwa kwa sababu mtu mmoja amesema atapitishwe, niwahakikishia nchii hii ina mkubwa ambae anaitwa Mungu alie hai, nchi hii ina mwenyewe.

Mwanamuziki wa Kenya amesema muombee jirani yako aishi muda mrefu ili unapobarikiwa ajionee mwenyewe. Ni matamanio yangu, wakati niko CCM tulikuwa tunaimba wacha waisome namba. Hatutaki mtanzania yeyote aisome namba yoyote zaidi ya namba ya heri ya Tanzania.

CHADEMA ikichukua madaraka, ijiandae kukosolewa na wale wanaoikosoa warudi nyumbani wakalale salama kwa sababu katika kukosoana tunaandaa taifa lililo bora.

Katika mandhari mpya ya CHADEMA tukishirikiana na wengine, tutamruhusu kila mtanzania astawi tena, talanta zistawi tena, tukalijenge upya taifa ambalo alikuwa na maono nalo baba wa Taifa.

Tusubiri tuone MTIFUANO ndani ya CHADEMA kuhusu uteuzi huo wa mgombea wao. Na hapo ni kuwa ACT - Wananchi hawajaja na mgombea wao na kutaka kufanya coalition huku Bara kwa nia na lengo la kupata wabunge ili kupata ruzuku for their survival kwani handouts kutoka kwa wafadhili zinaelekea MWISHONI.
 
Kilichonishangaza ni hotuba ndefu aliyoitoa kiasi cha waandishi wa habari kuchoka,
Lakini pamoja nahutuba yte ile hakuruhusu maswali ambayo waandishi walitaka kujua yafuatayo.

1.Alimlipia mbowe nauli yakwenda islaeli km alivyosema lakini waandishi walitaka ufafanuzi kuhusu kulala je walilala chumba kimoja?
Maana alisema usiku wa manane waliamua waende huko kwenye kanisa alilojenga suleimani
Naalitaja hotel waliyolala bila kufafanua je vyumba tofauti?
2.wakati wanaweka vikaratasi waliangaliana na kucheka, kivipi! Maana kwenye maombi kila mtu anakuwa serious na anachoomba
3. Walikuwa kwenye tax moja, wte walikaa nyuma? Au .

Maelezo ya nyarandu yalikuwa na maswali mengi ambayo hayakujibiwa maana ilikuwa ni hotuba hivyo alipaswa aulizwe maswali haya.

Basi atujibu kupitia hapa jf kwakuwa amejileta, bila majibu basi tutaandika chochote.
 
Wagombea wote wa kiti cha urais kupitia vyama vya upinzani wanajua wamepata fursa adimu ya ku-update CV zao kuwa walishiriki uchaguzi mkuu wa 2020.
 
Daah kama mgombea ni huyo ndio amewasilisha upupu wake hivi hafai hata nyumba kumi!
 
Huu ni utafiti wangu Binafsi. Ndugu Lazaro Nyalandu amekuwa akionekana anatumia vyema vyombo vya Habari kuliko watia nia Wengine ndani ya chama Chake.

Je Hii ni Juhudi binafsi ya team yake, ambayo inahakikisha inakuza Personal Brand ya mtu wao au Mkakati maalumu ndani na nje ya Chadema.

Kwa namna yoyote ile naona kuanzia 2015 hadi Sasa Nyalandu ndio amekuwa mtu pekee aliyejiandaa kwa nafasi hii kwa upande wa Chadema au Upinzani Kwa Ujumla.

Chadema Nyalandu ni Asset kubwa sana Kwenu hasa kwenye Siasa za Kisasa. Kama Chadema hamtaungana na ACT ili mumsimamishe Benard Membe tafadhalini hakikisheni Nyalandu anapeperusha Bendera yenu.
ni sawa ila Lissu kiboko ya pombe
 
Back
Top Bottom