Zanzibar 2020 Namba 5: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi achukua fomu kuwania Urais wa Zanzibar

Natabiri kuwa ataongoza Zanzibar kipindi kimoja na kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya Tanzania kwa vipindi viwili baada ya Mh. Magufuli kama ilivyotokea kwa Baba yake
 
Candidate na Rais wa JMT 2025-2030. Mh.Hussein Mwinyi amewekeza sana kwenye UADILIFU UAMINIFU NA UZALENDO Kinachofuata ni rewards all the way kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya uchumi mkubwa.Too humble and genius
 
Waziri wa Muungano ajaye baadae kuwa wa ulinzi
 
Ifike wakati tabia ya kurithishana madaraka ya nchi ikomeshwe , Wazanzibar ambao baba zao hawakuwa viongozi hawana haki ya kuwania uongozi ?
Tatizo ni nini? zenji ni nchi ya kisulutani, muoneni babu yenu tangu 1995 mpaka sasa bado anawania usultani. sasa kwa watoto afadhali wanaona aibu wanapokezana. mwambieni huyo mzee wa act-wazalemdo asichukue fomu awaachie na wengine wajaribu. asante. kaka tuchart
 
Hivi sheria inaruhusu mtu wa bara kuwa Rais wa Zanzibar?

Vv
 
Je John atakubali kusafiri na Husein? Kuna mwanabodi aliuza swali humu, Sasa Hussein ameamua kujitosa je, ikitokea Mkapa akampitsha kuwa mgombea kwa upande was visiwani . Je , John atakubali kusafiri na?
 
Mbona wako watoto wa viongozi wengi tu nchi hii? Wangapi wana sifa za kupigiwa mfano kama Dr. Hussein Mwinyi?

Umewahi kumsikia marehemu Thabit Kombo katika duru za siasa za Zanzibar? Mahmood Thabit ndio mwanae. Kama umaarufu wa wazazi wao na mchango wao kisiasa huko visiwani ndio vigezo basi marehemu Thabit Kombo alikuwa zaidi ya Ally Hassan Mwinyi!!!
 
Ni miaka mitano then ataswitch kuja URT kama amiri jeshi mkuu wa URT from 2025-2030, like father like son. Bonge la Rais, amepikwa na akapikika.Kudos Daktari
Kiuhakika nimefurahishwa mno. Ni kiongozi mnyenyekevu sana hana skendo za kukinga. Hata ndogo sijakusikia. Ila ninaamini ana utu sana. Akiwa waziri wa sekta nyeti ya kitaifa siyo mchezo kabisa. Zanzibar wanapata dodo la kuondoka mtini bila kupata kidonda.
 
Hakika umenena. Ninamsubiri tu 2025 aje kuwa Rais wa Jamhuri. The smartest President nakuhakikishieni. Hana makuu. Familia nzima iko cool down to earth.
 
Kama Mwinyi Angekua amewekwa wizara ngumu zinazohitaji mtu afanye kazi haswa akazimudu ningeamini anaweza Sana.
Wizara ya Mambo ya ndani
Wizara ya ujenzi
Wizara ya ardhi
Sasa Ukiwa waziri Wa wizara ya ulinzi na JKT haiwagusi wananchi moja kwa moja kwenye Maisha yao ya kila Siku.
Hata ukimuuliza mwananchi kule chini anaweza asimjue hata Huyo waziri na asijue hata anafanya kazi gani.
Ni nani alipewa Hiyo wizara ikamshinda?
Nafikiri aliwekwa makusudi kwenye wizara ambayo haiwezi kumletea madhara na wananchi haiwasumbui Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…