TOKA MAKTABA
2023 March 23
WALIOHUSIKA OPARESHENI LOLIONDO WATUHUMIWA KUTOWEKA KWA MWANANCHI
View: https://m.youtube.com/watch?v=ffjYDY1gRtM
Wakili msomi Joseph Oleshangay akifafanua masuala katika shauri la Kesi ya kulazimishwa kupotea ( Enforced disappearance)kwa mzee Oriais Oleng’iyo (85) wa Ololosokwan, Loliondo katika Wilaya ya Ngorongoro Miscellaneous Criminal Application No. 67 of 2022 imeahirishwa hadi machi 30/2023 kwa ajili ya kusikilizwa mbele ya jaji Gwae wa mahakama kuu ya Tanzania, masijala ya Arusha ambapo mlalamikaji ambaye ni mtoto wa mzee Oriaisi anapaswa kuhudhuria mahakamani pamoja na walalamikiwa ambao wamehusika kwenye oparesheni ya kuweka vigingi eneo la Loliondo.
Madai ya Kupigwa risasi na kupotezwa kwa Mzee Oriais Oleng’iyo yameelezwa kuwa ni matokeo ya operesheni iliyofanyika Loliondo tarehe 10.06.2022 wakati wa uwekaji vigingi (beacons) eneo la vijiji 14 vya Loliondo lenye kilometa za mraba 1502.
Walalamikaji wanaiomba mahakamaIamuru walalamikiwa kumleta mahakamani Oriaisi Pasilange Ng’iyo ambaye amepelekwa kusiko julikana tangu alipokamatwa nyumbani kwake Engong’u Nairowa, Kata ya Ololosokwan, Loliondo wilaya ya Ngorongoro.
Ombi la pili ni mahakama ina amuru na kuwaelekeza walalamikiwa kumwachia huru Oriasi Pasilange Ng’iyo Kurosawa alikoshikiliwa tangu 10.06.2022.
Mahakama iamuru walalamikiwa waje Mahakamani kueleza sababu za kushikilia Oriasi Pasilange Ng’iyo kinyume cha Sheria. Pamoja na kuiomba mahakama iamuru na kuelekeza walalamikiwa kuleta mwili wa Oriasi Pasilange Ng’iyo akiwa hai au asipokuwa hai.
Sambamba na hilo wameomba walalamikiwaOCD - Ngorongoro, Kamanda wa polisi mkoa (RPC) wa Arusha, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Mkuu wa jeshi la polisi( IGP ) pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wafike mahakamani kujibu tuhuma za utokuonekana kwa mkazi huyo wa Loliondo kwani kwa namna moja ama nyingine wanahusika kwa kile kilichoelezwa walihusika na zoezi la uwekaji vigingi eneo hilo.