Namna shule za sasa zinavyoiua elimu yetu. Zimekaa kitapeli sana

Namna shule za sasa zinavyoiua elimu yetu. Zimekaa kitapeli sana

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
16,911
Reaction score
28,469
Wakuu
I salute you kinsmen..

Ukiachana na kwamba na mimi nasomesha pia ila pia nimekuwa nikifuatilia sana jambo hili linapoelekea naona sio pazuri kabisa nchi itaanguka.

Well
Hizi shule za sasa hasa hizi za mabasi ya njano tunazomesha watoto wetu ni za kitapeli sana nowdays..

1: kwanini watoto wananyimwa utoto wao??
Hili jambo linanichosha sana kwenye vikao vya shule nilishaenda na kuwaambia walimu hili jambo kuwa mwanangu hatoenda shule weekend hata kidogo!!

Mtoto wa darasa la 4 sasa aende jumamosi kufanyaje??
Mbaya zaidi leo ni sikukuu nimeona wanafunzi wanaenda shule tena shule ya kayumba tu! Means na walimu wameingia kwenye mkumbo huu?

Kiutaratibu masaa ya kazi ni 9, yaani unatoka kazini saa 9:30

Sasa mwalimu akipitiliza muda sijui wanaita remedial labda tuseme sawa ameona wanafunzi wake ni slow learner au anataka kujaza gape aliloacha!

Lakini kwanini tutozwe pesa? Kwanini? Pesa ya remedial tulipe sisi sawa mtoto anatoka asubuhi saa 12 kamili yupo anasubiri basi eti na halafu anarudi jioni saa 12 au 11 jioni.

Akifika tu hata kupumzika hakuna anakwambia anafanya homework mwalimu mkali!

Anapumzisha akili yake kama mtoto saa ngapi? Elimu imegeuka ya namba zaidi kuliko ustawi wa akili za watoto!

Lengo la shule nyingi ni kufaulisha na kupiga ada tu ili waonekano ni hatari kumbe wanakaririsha madesa wanafunzi kilazima bila kujali afya na ukubwa wa mtoto mwenyewe!

Sasa mnajiuliza wenyewe kuwa kwanini sikuhizi watu wanafaulu ila kichwani ni empty??

Jibu hili hapa tayarj tunaaandaa mashine za kusoma na sio watu wenye elimu ila mashine za kusoma tu na kufaulu!

Pia hizi day care nazo ni tatizo.
Kimsingi day care maana yake ni eneo ambalo watoto ambao wazazi wao wako busy na hawana muda wa kushinda nao huwapeleka huko kushinda mpaka jioni na kuwapitia! Ulaya ipo hivyo!

Then huko mtoto anajifunza vitu na mazingira kwa picha na physical materials basi na michezo tu..

Kisha akienda nursery school huko ndio shule anaanza kujifunza kusoma akiwa na miaka 5 to 6 au 7. Maana psychological mtoto wa umri huo ndio anaweza kufikiria na kuchanganua sawa sawa.

Sasa wazazi wa kibongo kuona ile analipa ada kubwa day care na mtoto asifundishwe kusoma na kuandika ndio ikafanya hizi day care kuforce mambo ambayo hayapo kabisa na haitakiwi.

Lakini ndio hivyo zinajitokeza mitaani kama uyoga.

"Education is the kindling of a flame, not the filling of a vessel."
-socrates..

Its Pancho
 
Tuamke badala ya kujaza vitu tu kichwani mwa watoto bila kujali ustawi wa akili yake basi

Tunaelekea kuzalisha mashine tu za kusoma vitabu sio watu wenye elimu.

Mtoto wa darasa la 4 counter book kumi za nini??
 
Inasikitisha sana
Mwalimu anasema kuwa likizo ya mwezi wa 6 waende watoto

Kufanyaje?? Muda wote kufundisha walikuwa wapi?
Mwanafunzi anapumzika saa lini? Kama na hiyo likizo kubwa nayo aende akasome tena muda ule ule asubuhi sana awahi shule??

Hapo hapo wazazi wanaambiwa walipe hela walimu wafundishe watoto
 
Mwalimu anasema kuwa likizo ya mwezi wa 6 waende watoto

Kufanyaje?? Muda wote kufundisha walikuwa wapi?
Mwanafunzi anapumzika saa lini? Kama na hiyo likizo kubwa nayo aende akasome tena muda ule ule asubuhi sana awahi shule??

Hapo hapo wazazi wanaambiwa walipe hela walimu wafundishe watoto
Kipindi nasoma kuna mwalimu alituambia Kwenye likizo ya wiki moja tuje shule ili tuichambue hisabati kwa undani zaidi 😂
 
Sasa hivi huko shule za serikali hasa sekondari za kata hali mbaya sana.
Hakuna mapumziko weekend days au public holidays. Hakuna likizo fupi wala ndefu.
Wanasoma hizo remedial classes alfajiri na jioni.
Waalimu wanalazimisha kinguvu sababu wanatoza pesa.
Sasa hivi wanajiamulia mambo hovyo kama hakuna serikali, hakuna Waziri wa elimu wala Waziri wa ustawi wa jamii au wa afya.
 
Watoto hawahitaji kusoma kwa masaa 8+ kwa siku ili aweze kujifunza na kuelewa kitu kwa undani. Unfortunately, mkakati wa shule nyingi ni kufanikiwa kama institution (kuwa na watoto wengi, kuwa na ufaulu mkubwa, na wazazi kugombea nafasi yakupeleka watoto wao shuleni kwao), na sio mafanikio ya watoto kama individuals. Ndio maana wanawanyima watoto muda wakupumzika na ku-digest hayo waliyojifunza, quality time na familia zao, all in the name of ufaulu mzuri.

Mbaya zaidi ni kwamba wazazi nao ni willing victims wa hii mentality, kwahiyo watoto wanakosa mtetezi. I wish wazazi wengi wangejitokeza kama wewe kupinga huu mfumo ili Watoto wapate nafasi ya kuwa watoto.
 
Sasa hivi huko shule za serikali hasa sekondari za kata hali mbaya sana.
Hakuna mapumziko weekend days au public holidays. Hakuna likizo fupi wala ndefu.
Wanasoma hizo remedial classes alfajiri na jioni.
Waalimu wanalazimisha kinguvu sababu wanatoza pesa.
Sasa hivi wanajiamulia mambo hovyo kama hakuna serikali, hakuna Waziri wa elimu wala Waziri wa ustawi wa jamii au wa afya.
Ndio hasa kayumba sasa hivi si kama leo nimeona wanafunzi wanaenda shule?

Wasipoenda wanapigwa
Sasa mimi huu ujinga siwezi kuvumilia remedial zao hizo ni lengo la kupata pesa.

Kwanini mwanafunzi some alfajiri? Na bado jioni sana asome?

Hizi ni pesa zinaenda kwa wakuu wa shule wakipewa sapoti na ma afisa elimu kata
Titicomb
 
Ujinga wa wazazi na walezi umefikisha huko watoto
Wazazi na walezi wengi ni malembukeni na wenye akili finyu kutwa kufuata mkumbo
Waalimu wanajua udhaifu huu wa wazazi wengi hasa hawa millenials.
Wanaitisha vikao vya wazazi na kupitisha maamuzi haya masomo ya ziada kwa vitisho.
 
Waalimu wanajua udhaifu huu wa wazazi wengi hasa hawa millenials.
Wanaitisha vikao vya wazazi na kupitisha maamuzi haya masomo ya ziada kwa vitisho.
No man kwenye vikao vyao nilishawaambia hilo kwangu halipo hawataki namuhamisha shule tu maana hawana huo ubavu ada nalipa

Mtoto wangu haendi shule weekend no nilishakataa hilo.
Michango isiyo na kichwa wala miguu nilikataa eti pesa ya remedial!

Ada tunalipa ya kazi gani? Nini maana ya ada?
 
Basi yaache yakae nyumbani yaangalie makatuni au swagia kijijini kwa babu yao wakachunge mikia kama shule ni mateso.
Wewe ni mwalimu unaye nufaika na huu upuuzi au mzazi asiyejua kuhusu umuhimu wa kupumzisha akili.
Unafikiri walioweka hayo mapumziko kisheria, kikanuni na kisera ni wapuuzi au wajinga?
Afya ya mtoto ni muhimu kuliko chochote kile.
 
Back
Top Bottom