tang'ana
JF-Expert Member
- Apr 3, 2015
- 11,931
- 15,849
Kuna kipindi nilikwenda Japan kwa shughuli flani.
So nikawa nacheck news kwenye television, na uzuri Station niliyokua naangalia ilikua inatumia lugha ya Kiingereza katika kurusha matangazo yake so nilielewa vizuri tu kilichokua kinazungumzwa.
Mtangazaji alitangaza kwamba kuna maiti ya mwanaume mmoja imekutwa kwenye chumba cha hotel, police wakasema mwanaume huyo inasadikiwa aliamua kujiua kwa sababu ya aibu aliyoipata baada ya kugundulika kwamba alitumia fedha kutaka kuwahonga maofisa wa serikali ili aweze kupata tender flani kutoka serikalini.
So nikakumbuka huku kwetu Tanzania mtu anasifika na kuonekana mjanja kwa sababu ya kuiba mali za umma, kumbe huko kwenye nchi za wenzetu ni suala la aibu sana kuiba mali za umma.
Kwa kweli nilijifunza kitu kipya katika maisha yangu na ndio maana wenzetu wanapiga sana hatua za kimaendeleo.