Namna wenzetu wanavyowaandaa watoto wao kuja kuwa wasimamizi wa biashara zao

Namna wenzetu wanavyowaandaa watoto wao kuja kuwa wasimamizi wa biashara zao

Wengine hawa hapa
IMG_3676.jpeg
 
Mo dewji akifika miaka 60 anatkaa pending ,kijana anapata uzoefu ila sisi black mpaka mzee anakufa na miaka zaidi ya 70 kashikilia kila kitu cha kampuni.
 
Watoto wa ngozi yetu hawaaminiki. Akishajua njia zote za mali zako anaweza akakutanguliza ahera ili yeye ndio awe bosi aonyeshe ukidume wake duniani kwani ulikuwa unamchelewesha
Jichanganye, ataletewa demu atapagawa watafubaza mali zote mtabaki kulaumiana tu. Ngozi zetu hizi ni bahati nasibu kwenye mambo haya
 
Generational inheritance, ngumu sana kwa watu weusi japo naona kuna watu wameanza kuyafanyia kazi, kuna familia kwa mitaji hiyo ya kawaida wanawapa watoto access ya biashara, channels zote ili nao waje kuwa kama wazazi wao.

Ninachoona tunapofeli, kumwambia tu mtoto nenda kakae dukani leo haitoshi, tunatakiwa kuwa zaidi ya hapo. Tuwape watoto elimu ya kutosha, uzalendo wa kupenda mali na kuzitunza, matumizi sahihi ya fedha(hapa wengi tunafeli sana), baba akishakuwa na uwezo kidogo anawa expose watoto kwenye maisha ya kifahari, watoto hawajui thamani ya ile fedha inayotumika, wao wanataka watumie tu coz wanaviona na hawajui how it cost to accumulate them.

Wahindi wana nidhamu sana ya fedha, unlike sisi, wana nidhamu ya muda, unlike sisi, hawana extravagant life wakishakuwa matajiri, unlike sisi, wanatumia elimu zao vizuri, unlike sisi.
 
Mithali 22:6
[6] Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.



Kuandaa kizazi kijacho kuingia katika urithi, biashara, au usimamizi wa biashara ya familia kunahitaji kuhama kutoka katika mfumo wa udhibiti na tuje katika mfumo wa kumjengea uwezo. Kubadili mfumo wa kazi/biashara ya watangulizi kwenda kwa warithi hufanya kazi vizuri zaidi inapopangwa katika awamu tano tofauti.

1. Kuonyesha kazi/ biashara kwa vitendo na Simulizi (Umri wa miaka 6-12)

Washirikishe watoto mapema kupitia kazi unazofanya wajue mkate unavyotafutwa hadi kufika mezani wakiwa na umri mdogo, badala ya maelezo ya nadharia zaidi. Watoto wa umri huu wanajifunza zaidi kwa kuona. Waache waangalie utaratibu wa kila siku, mwingiliano wa mteja, au kazi ya uendeshaji moja kwa moja.

2. Mafundisho kwa vitendo (Umri wa miaka 13-18)

Anza chini: Hakikisha wanafanya kazi katika majukumu ya uendeshaji wa ngazi ya kwanza ambapo lazima wapate mafunzo namna ya kuzungumza na wateja, kuuza bidhaa/huduma, namna ya kurudisha chenji n.k.

Ujuzi wa kifedha na uendeshaji: Kufundisha namna ya kurekodi na kutunza hesabu za mauzo na nidhamu ya mtiririko wa pesa. Mazoezi ya ulimwengu halisi wa bajeti ndogo hujenga misuli muhimu ya kufanya maamuzi.

Wahusishe watu wa nje unaowaamini : Washauri wasio wa familia, washauri wanaoaminika, au wasimamizi wa kitaalamu kutathmini utendaji wao.

3. Uthibitisho wa mafunzo kwa kufanya biashara/kazi nje ya nyumbani.

Waombe wafanye kazi kwingine kwa miaka 3-5 kabla ya kujiunga na biashara ya familia au kuchukua majukumu rasmi ya urithi. Mafanikio kwa kufanya kazi kwingine (na kushindwa) hujenga kujiamini na uaminifu wa kweli.

Wape mamlaka huru: Wanaporudi na kuchukua jukumu rasmi, wape kitengo tofauti, mradi mpya, au jukumu maalum la upanuzi wa biashara/kazi ambapo wana uhuru kamili wa kufanikiwa au kushindwa kutokana na kufanya maamuzi yao wenyewe.

4. Utawala na Ushauri Uliopangwa wa namna ya kurithisha majukumu.

Unda utawala ulio wazi: Tenganisha umiliki, utawala, na usimamizi. Unda ukaguzi rasmi, mikutano ya familia, au bodi za ushauri ili kupitia mkakati kwa uwazi.
Badilisha jukumu kutoka kwa Bosi hadi Mwenyekiti: Watangulizi lazima wabadilike kikamilifu kutoka kwa wadhibiti wa uendeshaji hadi washauri wa kimkakati, hatua kwa hatua wakipanua wigo wa kufanya maamuzi wa mrithi.

5. Namna nzuri ya kuhamisha majukumu ya kiutawala

Fafanua kwa uwazi namna mamlaka inavyotumika kwa kusaini vitu kama hundi za akaunti za benki, mikataba na nyaraka mbali mbali za kampuni.

Ruhusu mageuzi: Watangulizi lazima wakubali kwamba warithi watabadilisha mifumo, kutumia zana mpya, na kuboresha mikakati kutokana na teknolojia na kubadilika kwa soko n.k. Kuhifadhi maadili ya msingi ni muhimu; kuhifadhi mbinu halisi za kihistoria ni muhimu katika kuendeleza maono ya mtangulizi wa kazi/biashara.
 
heheee mnachekesha sana, mnaongelea mtoto kuachiwa usukani aongoze kampuni wakati Mdingi kumwachia mtoto gari tuu ni kipengele.

kwa ufupi madingi zetu na mababu ni wachoyo sana, ndio maana tamaduni zetu zina sera za ajabu, utasikia Paja na fikigisi ni za baba, mama mjamzito asile mayayi, ..
 
Huyo dogo anaweza kuwa hajarithishwa ila anaandaliwa kuwa kiongozi wa kizazi cha nne cha mali hiyo. Kama ambavyo baba yake alivyoandaliwa na babu zake, kwa kumpa elimu nzuri, uzoefu na exposure kuendeleza na kuotanua mali na kubaki vile vile ya ukoo kama ulivyosema.
Hapo kila mtu atakuwa msimamizi wa kitu flani, lakini huyo dogo ndio atakuwa overall in charge.
Ni succession plan katika usimamizi wa biashara hasa hizi za vizazi (lineage), na wahindi ni mabingwa wa kuandaa wabeba maono.
Alishasema mwenye mtoto kpitia kurasa zake za mitandao ya kiamii kwamba huyu ndio mrithi wake,baada ya kuhitimu masomo yake uingereza,hili kalifanya hata Rostam,kwa sisi wenye shauku na GW tunafuatilia.
 
heheee mnachekesha sana, mnaongelea mtoto kuachiwa usukani aongoze kampuni wakati Mdingi kumwachia mtoto gari tuu ni kipengele.

kwa ufupi madingi zetu na mababu ni wachoyo sana, ndio maana tamaduni zetu zina sera za ajabu, utasikia Paja na fikigisi ni za baba, mama mjamzito asile mayayi, ..
Nawewe kuwa dingi na babu baadae tuone kama utwaachia watoto wako haya unayoyasema kwamba sisi madingi hatuwaachii.
Usifikiri utabaki mtoto hivyohivyo. Halafu usikute wewe uko 30+ halafu hujioni ni dingi.
 
Huyukushoto ni mtoto wa Mohamed Dewji,anaitwa ABBAS ndiye mrithi wa mali zote za ukoo na msimamizi (ameshateuliwa),sasa hivi anazunguka nae katika kila sula la biashara na anaingia naye kwenye vikao vya bodi ya wakurugenzi ya METL.

Huyu katikati ni WAMKELE MENE , Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA).

Wazzi wa ngozi nyeupe utasikia hizi mali ni zangu na mama yenu tafuteni zenyu,wanakufa wanaaca migogoro ya mali,shenzi.

View attachment 3667186
Huyu dogo naye mvivu tu saiv angekuwa anapigana vita kuitetea Gaza
 
Mkuu maada ni nzuri lakini ni lazima turudi nyuma na kujiwazisha wenyewe.

As a nation tumepata uhuru 1961, nchi yetu ilikua na wasomi wasiozidi 100. Asilimia kubwa ya Babu yangu na Babu Yako walikua wajinga tuu.

BAADA ya kupata uhuru Nyerere akaja na sera za kipumbavu za ujamaa na vijiji vya ujamaa. Hii iliwafilisi sana Babu zetu.

Turudi kwenye misingi, Babu zetu kama walifanya biashara bhasi walifanya biashara za kawaida ambazo zilihitaji ufahamu wao binafsi, Lakini asilimia kubwa wazee wetu waliamini katika nguvu kazi ya uzalishaji Yaani aoe wanawake wengi azae watoto wengi ili apate kulima sehemu kubwa ya ardhi. Pia uwekezaji mkubwa kwao ilikua ni ufugaji, mashamba na misitu. Nje ya hapo ilikua inahitaji elimu ili kufanya uwekezaji kitu ambacho ilikua vigumu kwa Babu zetu maana shule zilikua chache pia hata wenye access nazo bado hawakuona umuhimu sana.

Huo uwekezaji walifanya ulikua ni rahisi sana kupotea baada ya wazee kufariki, Fikiria Mzee alikua na wake 3 watoto zaidi ya 15.
Hawa wakigawana mashamba, miti na ng'ombe bhasi ndio utajiri wa Babu umeshakwisha.

Angalau wasukuma wao bado wanazingatia Mila zao unakuta wanaishi sehemu Moja, Pia wanapotoa mahali ya ng'ombe wao pia hupokea mahali ya ng'ombe kitu ambacho kinafanya utajiri usipungue sana.

Haya ni baadhi ya matatizo ambayo wazazi wetu waliyarithi kutoka kwa wazazi wao. Tushukuru Mungu sisi tumepata elimu Sasa tuanzie hapa kuelekea huko waliko wenzetu akina MO DEWJI.

ShesRise_1 naona JF ya zamani inarudi, karibu uweke michango yako hapa.
Mkuu,vipi matajiri kama kina Mengi,yeye alipata elimu kwenye chuo kizuri kabisa huko Scotland. Kwanini tangu afe vitu vyake pia havieleweki? .
 
Mkuu punguza dharau mbuzi sio Mali???😂😂😂 Jokes

Nafikiri wazee wetu wamekosa elimu tuu ya succession plan, tumeona matajiri wengi wakishindwa kufanya hiyo kitu.

Vivid example ni Mengi, yale makesi ya yule mrembo na watoto wa marehemu.

Pia tumesikia ya HANSPOPE na juzi nimeona bandiko la watoto wa mama Rwakatare.
Tajiri mmiliki wa mahoteli maarufu huko Arusha eg Ngurdoto. Kuna hoteli yake nzuri sana kama upo Dubai vile, sasahivi imegeuka sehemu ya kulazia magari.
 
Back
Top Bottom