Nakubali mkuu,lakini matajiri wetu exposure kama hawana hilo ni kosa lao binafsi,wao ndo wanapaswa kutafuta hizo exposure,na uzuri pesa za kusafiri wanazo hiyo haishindikani.Dangote ametoka kule Nigeria kaskazini,kwa anaefuatilia masuala ya Nigeria anafahamu Nigeria kaskazini ndo jamii ambayo iko nyuma kwenye kila kitu hasa kielimu wenyewe wanachojua ni kujifunza dini na kuoa/kuolewa mapema,hata Dangote mwenyewe kafanikiwa kusoma hadi level za juu ila kaoa akiwa na miaka 20 tena mke wa kuchaguliwa na familia,hapo jiulize sasa wasiosoma wanaoa na kuolewa wakiwa na miaka mingapi,yaani kama huku Bongo tunavyowachukulia watu wa kusini ndo Nigeria wanavyowachukulia watu wa kaskazini.Lakini hakukubali kuachwa nyuma,kafanya juhudi zake binafsi mpaka kafika hapo. Halafu njoo huku kwetu sasa,Mengi katoka kwenye kabila ambalo lilielimika mapema sana ,akapata fursa ya kusoma nje tena Scotland, akafanya kazi kwenye kampuni ya kimataifa na alikuwa anapenda sana kusoma vitabu . Mengi alikuwa na exposure ya kutosha tangu akiwa kijana mdogo, lakini kashindwa kufanya succession. Kila anachofanya Dangote,Mengi alikuwa na uwezo wa kufanya,ila ndo hivyo tena.