Namna ya kujilinda na kuwa salama unapokuwa Bar

Namna ya kujilinda na kuwa salama unapokuwa Bar

Yani niende kula bia nmebeba silaha...

Inakua starehe au nimeenda vitani?

Nadhani kuna aina ya bar na mikoa pia inachangia...
Aisee...
Umeniwahi, nilikuwa hata mimi nataka kusema hivo...
Naona hizo ni baa za choka mbovu...
Na uhakika baa zote zilizoko Haile Selassie Road hakuna hizo pilika..
 
  1. Usiache kinywaji chako bila uangalizi ukaenda sehemu nyingine kisha ukarudi kunywa tena hicho kinywaji chako,
  2. Usikubali offer ya kinywaji kutoka kwa mtu usiyemjua,
  3. Ukiona kinywaji chako kina ladha ya tofauti na uliyo izowea,acha kunywa hicho kinywaji mara moja,
  4. Mnapoenda grp,wakati wa kuondoka msiache kila mtu aondoke peke yake,ondokeni pamoja,
  5. Usitoe information zako kwa mtu usiyemjua,acha mazowea na watu uliokutana nao hapo Pub.
 
Aisee...
Umeniwahi, nilikuwa hata mimi nataka kusema hivo...
Naona hizo ni baa za choka mbovu...
Na uhakika baa zote zilizoko Haile Selassie Road hakuna hizo pilika..
Unaenda bar unaingia tu unakuta watu wana makovu wahudumu matusi ya kutosha... mabaunsa wamevaa kaoshi, ngeu za kutosha... Masela kibao... malaya wamemwagika... vyoo vichafu kinoma, kaunta hakueleweki... nje boda vindala zimepaki nyingi kuliko usafiri wowote. Music ni ule wa kelele n.k

Bobu kimbia au fuata masharti ya mtoa uzi umeingia uwanja wa vita sio bar😀😀😀
 
Sema mle tunakutana wababe tu.
Boss, Mbabe ni yule anayeweza kuja nyumbani kwako akakuteka na kukupeleka kusikojukikana akiwaacha majirani na mkeo wakihadithia. Hizo bar mnazosema zina wababe ni wababe baina yao, unajua hata kundi la wanawake lina mbabe. Siku akija mbabe ndo utaamini, zitabaki tu hadithi za mashuhuda ila mbabe ataondoka na mtu wake huku hata alama hana.
 
Ni vichaa wanajiita wababe.

Wababe wanarushiana risasi sio chupa.
 
Back
Top Bottom