Utabiri wa Ezekiel sura ya 38 unatimia. Gog Yaani Urusi watajiunga na Magogu Yaani Iran kuivamia Israel, hapo ndio utukufu wa Bwana Mungu kwa watu wake Israel utakapoonekana . Hizi ni dalili tu unabii utatimia Iran na washirina wake hawataweza.
Waafrika tutaendelea kugombana na viongozi wetu kila siku kuwa hawatuletei maendeleo. Kumbe maendeleo yanashindwa kupatikana kutokana na upumbavu wa watu weusi kama wewe ambao wanaamini kuwa Mungu ana watu wake special (waisrael tu), sio mimi na wewe.
Kwanini unaamini kuwa Mungu watu wake ni waisrael tu?
Je kwanini Mungu ameamua kufanya ubaguzi wa kuchagua waisrael kuwa watu wake na sio mimi au wewe?
Je wewe mgogo au mmakonde Mungu alikuumba ili uje kuwa mtu wa nani?
Huu upumbavu sijui waisrael ni watu wa Mungu, sijui waisrael wamebarikiwa kila kitu, Wachina waliukataa, wakaamini kuwa Mungu ni wa wote, habagui kabila, rangi wala nchi.
Ndomaana leo hii wachina wamepiga hatua kubwa kiuchumi, kijeshi, kijamii, kiteknolojia na kielimu, baada ya kujiweka mbali na propaganda za taifa gani ni la Mungu.
Miaka ya 70 Afrika tulikuwa sawa kiuchumi na China, baada ya sisi kukumbatia habari za waisrael ni watu wa Mungu pekee na kuanza kujaza misikiti na makanisa mitaani. Wenzetu wachina wakawekeza katika viwanda, shule, teknolojia, biashara nk.
Sasa leo hii inasemekana kuwa China ni nchi ya pili kwa uchumi duniani, japo data zingine zinasema inawezekana ikawa ya kwanza sema tu Mmarekani na media zake wanaamua kupika propaganda ili ionekane kuwa US bado super power wa uchumi na jeshi.