From above quote,
1. Rais wa TEC
2. Askofu mkuu
So hakunaga more seniors huko? You dont answer to nobody since you are a sovereign? Mimi nilifikiri those guys they report to Ruwaichi
Therefore that guy kuwa Cardinal basi Ruwaichi do surrender to the cardinal.
Hakuna Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania…
Kuna Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania - TEC (Askofu Mkuu Gervas J. M. Nyaisonga) ambaye husaidiwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Askofu Flavian Kasala Matindi)…..Na kuna Mtendaji wa TEC ambaye ni Katibu Mkuu wa TEC (Padre Dr. Charles Kitima)…
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ni muunganiko/mkusanyiko wa Maaskofu wote Katoliki Tanzania….
Askofu Yuda Thadei Ru’Waichi yeye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam (Metropolitani ya Dar es salaam)…..
Kanisa Katoliki Tanzania lina jumla ya Majimbo Makuu Saba na majimbo 27 (7 ecclesiastical provinces/metropolitan dioceses and 27 suffragan dioceses)
Majimbo makuu saba ni Dar es salaam (Askofu wake Mkuu ni Yuda Thadei Ru’waichi O.F.M.Cap), Mwanza (Askofu wake Mkuu ni Renatus Leonard Nkwande), Arusha (Askofu wake Mkuu ni Isack Amani Massawe), Tabora (Askofu wake Mwandamizi - Coadjuctur Protace Rugambwa ambaye amekuwa elevated kuwa Kadinali), Dodoma (Askofu wake Mkuu ni Beatus Kinyaiya O.F.M.Cap), Songea (Askofu wake Mkuu ni Damian Dennis Dallu) na Mbeya (Askofu wake Mkuu ni Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga).
Kila Askofu ni Kiongozi katika Jimbo lake (hii ni kwa Maaskofu Wakuu Jimbo Kuu-Archbishops na Maaskofu wa Majimbo-Bishops).
Kuhusu cheo/hadhi ya Mwadhama Kadinali ndani ya Kanisa…Kadinali huteuliwa na Papa na huwa ni Cheo cha Maisha yote…Polycarp Kadinali Pengo haitwi Kadinali Mstaafu, Kikanuni Askofu akitimiza miaka 75 hustaafu majukumu yake ya Kiaskofu (ingawa bado huwa na fursa ya kuendelea na majukumu yake ya Kichungaji).
Hivyo Pengo ataendelea kuwa Kadinali mpaka siku yake ya mwisho Duniani. Na kwa sasa yeye anaitwa Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.
Hivyo Maaskofu Katoliki wote wakiwemo Makadinali (bila kujali hadhi zao) wanawajibika moja kwa moja kwa Baba Mtakatifu ambaye kwa sasa ni Papa Francis.
Mojawapo ya role ya Kadinali wa Kanisa Katoliki ni kushiriki katika Uchaguzi wa Papa.
NB: Kadinali huteuliwa miongoni mwa Maaskofu Wakuu, Maaskofu na Mapadri…Hivyo hata Padri wa kawaida anaweza kuwa elevated to Cardinal Priest.
Huu ndio ufahamu wangu kidogo…..Nipo tayari kusahihishwa pale nilipoteleza.