Nampongeza Rais Samia kwa kusimama na wakulima kwa kuwaruhusu kuuza mahali popote palipo na Bei nzuri

Chakula cha kutosha kwa muda gani?!

Na huko kutosha kwake kumezingatia affordability?! Kama nilivyosema, kuna globe food crisis... je, hicho chakula cha kutosha kimezingatia hayo?!
Kalime pawe na chakula Cha kutosha kwa kuzingatia vigezo vyako...na mvua msimu huu hakuna,njaa itazidi mwakani
 
Kalime pawe na chakula Cha kutosha kwa kuzingatia vigezo vyako...na mvua msimu huu hakuna,njaa itazidi mwakani
Kwahiyo uwezo wa kufikiri ndo umeishia hapo, sio?!

Anyway, busara inanishawishi nikupuuze!
 
Kwahiyo uwezo wa kufikiri ndo umeishia hapo, sio?!

Anyway, busara inanishawishi nikupuuze!
Nenda zinakopatikana takwimu za chakula,uwezo wa kufikiri umeishia kwa Mimi kukuletea hapa!?
 
Ok poa ukifika hospital utajua na wewe kwa nn hukusoma utapigwa gharama na uclalamike c unataka kila mtu akalime
 
Huu ni ukweli mchungu ambao wauza maji wa Dar hawawezi kukuelewa..

Mwendazake aliwahi sema kwamba ukiona Bei ni kubwa kalime.
 

Mkuu, anayefaidika na mazao yake kuuzwa nje ni wale wanaojiita madalali. Mkulima hana chake katika biashara hiyo.
 
Bei ya mazao ilikuwa Ni nzuri Tangia wakati wa mavuno ambapo mkulima aliuza kwa Bei nzuri ukilinganisha na miaka mingine ambapo mkulima amekuwa akiuza kwa Bei ya hasara
Mkuu, anayefaidika na mazao yake kuuzwa nje ni wale wanaojiita madalali. Mkulima hana chake katika biashara hiyo.
 
Umetumia lugha kali ya kuudhi lakini unachosema ni sahihi

Mkulima anateseka na kilimo mbolea bei juu haina ruzuku na kuna misimu anapoteza pesa kwa kukosekana kwa mvua .halafu watu wa white collar na ties wanataka wapate chakula kwa bei ya mserereko,
Wakulima waachwe wauze chakula kwa bei wanayoitaka hata kama tutapatwa na njaa , ili next life kila aliyeguswa na maamuzi haya aende shamba akalime na yeye apate faida .
 
We Chawa anayenufaika ni mfanyabiashara aliyehifadhi mazo,mkulima hakuvuna chochote na Hana akiba hata ya gunia moja,

Nenda kijijini ukatangaze kuwa unanunua mazao,Kama utapata ya kununua
 
Food security ? Ilitakiwa serikali itoe ruzuku kwenye pembejeo ili mkulima auze sehemu ya mazao yake kwa serikali, na kama akipata hasara ya kutovuna kwa kukosekana mvua serikali nayo iwe imeliwa kekundu keusi.!!!

Sio mkulima ahangaike na mambolea mfuko laki halafu serikali inakuja mwishoni baada ya muhindi kuonekana, hell no!
 
Wakulima tunasubiri mvua inyeshe tufanye yetu.
Bei imetuhamasisha.
Ila elimikeni na nyie , next time nendeni wenyewe sokoni, msitumie madalali kuja kununua mazao yenu.
Bei kweli zimesimama mwaka huu ,ila mkulima hakupata sana faida , wameneemeka wafanyabiashara
Next life , nendeni wenyewe sokoni, au muuze kwa bei ya sokoni
 
Bei ya mazao ilikuwa Ni nzuri Tangia wakati wa mavuno ambapo mkulima aliuza kwa Bei nzuri ukilinganisha na miaka mingine ambapo mkulima amekuwa akiuza kwa Bei ya hasara

Bei itakuwa nzuri kwa mkulima, iwapo bei jumla (general price level - gpl) itakuwa vile vile haita panda. Lkn kwa inflation iliyopo sasa, ilikuwa bora kubaki na chakula kingi kuliko kuwa na pesa nyingi. Maana kukiwa na chakula kingi kuliko pesa, nguvu ya ununuaji ya pesa (purchasing power) inakuwa kubwa. Vinginevyo kunakuwa na changamoto, ambayo mara nyingi inaanza kuonekana kuanzia mwezi Januari kipindi cha palizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…