Nampongeza Rais Samia kwa kusimama na wakulima kwa kuwaruhusu kuuza mahali popote palipo na Bei nzuri

Nampongeza Rais Samia kwa kusimama na wakulima kwa kuwaruhusu kuuza mahali popote palipo na Bei nzuri

Bei itakuwa nzuri kwa mkulima, iwapo bei jumla (general price level - gpl) itakuwa vile vile haita panda. Lkn kwa inflation iliyopo sasa, ilikuwa bora kubaki na chakula kingi kuliko kuwa na pesa nyingi. Maana kukiwa na chakula kingi kuliko pesa, nguvu ya ununuaji ya pesa (purchasing power) inakuwa kubwa. Vinginevyo kunakuwa na changamoto, ambayo mara nyingi inaanza kuonekana kuanzia mwezi Januari kipindi cha palizi.
Kwanza huo mfumuko wa Bei upo Tanzania pekee? Kwa hiyo mkulima ndio maalumu kwa kubeba gharama za mfumuko wa Bei ukitokea?

Kwani yeye Hana haki ya kuneemeka na kufaidi jasho lake? Kwani wewe huoni juhudi za mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kukabiliana na mfumuko wa Bei hapa nchini? Acha mkulima afaidike na jasho lake
 
Njaa inakuja...
Ni wajibu wako pia kutunza chakula Cha kutosha badala ya kusubiri serikali ikutunzie, lakini pia msimu mpya huoo unaanza hivyo andaa mashamba ya kuja kulima na siyo usubili wakulima wavuje jasho halafu wewe utake kuja kuwapangia Bei zako za kinyonyaji,
 
Kwanza huo mfumuko wa Bei upo Tanzania pekee? Kwa hiyo mkulima ndio maalumu kwa kubeba gharama za mfumuko wa Bei ukitokea? Kwani yeye Hana haki ya kuneemeka na kufaidi jasho lake? Kwani wewe huoni juhudi za mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kukabiliana na mfumuko wa Bei hapa nchini? Acha mkulima afaidike na jasho lake
Inflation inapimwa na bidhaa nyingi, huku bidhaa za chakula zikiangaliwa kwa ukaribu sana, maana ndizo zinazoliwa kwa wingi ukilinganisha na bidhaa zingine.
 
Ndugu zangu Sote tunafahamu kuwa secta ya kilimo katika nchi hii imeajiri na kubeba kundi kubwa Sana la watanzania, Ni secta ambayo ndio pumzi ya familia na Kaya nyingi, Ni secta inayotegemewa na watanzania wengi Kama shughuli kuu ya kiuchumi, Ni kimbilio la wengi, Ni ngazi ya wengi, Ni njia ipitayo na kupitisha watu wengi Sana kuinuka kiuchumi, kilimo Ni mgongo uliowabeba watu wengi Sana katika nchi hii, Ni ziwa ambalo kila mtanzania ananyonya , kilimo ni Mbeleko iliyowabeba wengi Sana,Kilimo Ni MAMA Mlezi wa Taifa hili,

Hivyo ukikipuuza kilimo Ni sawa na kuwa umewapuuza watanzania, ukikiacha kilimo Ni sawa na kuwa umewaacha watanzania wanyonge nyuma, ukikinyonya kilimo kibajeti Ni sawa na kuwa umewanyonya watanzania na ukikibana kilimo Koo Ni sawa na kuwa umewabana watanzania Koo na kuwanyima puumzi.

Sote Ni mashahidi namna ambavyo wakulima wa nchi hii kwa miaka mingi tu ambavyo wamekuwa wakipata hasara kubwa licha ya kuwa wamekuwa wakihenyeka na kuvuja jasho mwaka Hadi mwaka, lakini maisha ya mkulima yamekuwa yakibaki na kuwa duni tu kila siku, hii nikutokana na Bei mbaya ambayo mkulima amekuwa akiuza na kuipata, mkulima licha ya kutumia gharama kubwa katika uzalishaji lakini amekuwa akipangiwa Bei ya kuuza na mahali pa kuuza, amekuwa akipewa mashariti ya kwamba hutakiwi kuuza kule na kule na utauza hapa nchini pekee na mipaka ikawa inafungwa,

Hivyo mkulima amekuwa kwa miaka mingi akibeba misalaba ya watanzania wote, licha ya kulilisha Taifa hili lakini mkulima huyu amekuwa akibaki fukara Sana kwa kuwa Hana uamuzi katika kujitafutia na kuuza mahali ambapo soko Ni zuri na Bei ni ya uhakika,

Rais Samia alipoingia na kuapishwa kuwa Mkuu Wa nchi na Amiri Jeshi mkuu amekuja na mtizamo tofauti wa kukifanya kilimo Ni biashara ,hivyo biashara yoyote lazima itoe faida na itafutiwe soko zuri lakini pia kuwe na mipango mizuri yakuifanya biashara inawiri na kushamiri, mh Rais Samia amekataa kufunga mipaka kuzuia mahindi yasiuzwe nje ya nchi, Jambo lililopelekea mkulima kuuza Bei nzuri Sana mwaka huu tangia wakati wa mavuno,, huku mh Rais akihakikisha kuwa chakula kinakuwepo nchini Cha kutosha kwa usalama wetu

Sasa wakulima wanafaidi jasho lao, wanafaidika na juhudi zao, Sasa vijana wanahamasika kujiingiza katika kilimo, Sasa uzalishaji wa kilimo unaongezeka kwa kila mtu , Sasa watu wanaitafuta Aridhi ili walime maana Sasa kilimo kinalipa na hakimtupu mtu, Sasa kilimo kinakwenda kuwa kimbilio lenye matumaini kwetu vijana, Sasa kilimo kinatoa nuru ya kuinuka kiuchumi, Sasa kilimo kinarudi katika mioyo ya watanzania waliokuwa wameanza kukata tamaaa baada ya kuwa wahanga wakupata hasara kila mwaka,

Nataka niwaulize mnaolalamika uamuzi wa mh Rais wetu mpendwa kutofunga mipaka, Hivi mnajuwa adha za kilimo? Hivi mnajuwa gharama za kilimo nyie? Hivi mnajuwa misukosuko ya kilimo nyie? Hivi mnajuwa ugumu wa jembe nyie? Mmewahi kulima? Mmewahi kushika jembe nyie? Mnajuwa hata namna ya kushika mpini wa jembe au jembe la kukokota na ng'ombe? Mnajuwa mkulima anaamka saa ngapi na kulala muda upi? Mnajuwa mwili wa mkulima unapata maumivu kiasi gani? Au kwa kuwa mnaona vitu vikija sokoni tu? Jembe Ni Vita inayohitaji kujitoa kujitolea na kuwa mvumilivu Kama Asikari Jeshi aliye vitani kupigania nchi yake, mkulima amechoka kupata hasara kila mwaka

Muwe na huruma na mkulima jamani, jaribuni kuvaa viatu vya mkulima muone Kama vitawatosha, vitawashinda kwa uzito na ukubwa wake, lazima vitawapwaya na mtavivua tu, Kama mnaona mkulima hastahili kufaidika na jasho lake Basi nendeni nanyi mkalime, nendeni mkashike jembe, msikae tu kunyonya jasho la mkulima huku mkiwa kimvulini

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Unajidanganya mzee, wakulima masikini wote walishauza mazao yao pale tu walipovuna, anaefaidika ni yule mtu wa kati mwenye mtaji aliyenunua mazao kwa wakulima kwa bei ndogo
 
Unajidanganya mzee, wakulima masikini wote walishauza mazao yao pale tu walipovuna, anaefaidika ni yule mtu wa kati mwenye mtaji aliyenunua mazao kwa wakulima kwa bei ndogo
Bei ya mazao mwaka huu ilikuwa nzuri Tangia wakati wa mavuno Jambo lililo kuwa tofauti na miaka mingine ambapo Bei ilikuwa chini Sana wakati wa mavuno, lakini siyo wakulima wote huuza mazao yao wakati wa kuvuna, wengi tu hutunza mazao yao nakuyauza wakati wanajiandaa kuaza msimu mpya
 
Kwa hiyo ulitaka kusemaje, unataka mkulima auze kwa hasara , unajuwa Bei ya mbolea mwaka Jana ilivyokuwa?
Inflation inapimwa na bidhaa nyingi, huku bidhaa za chakula zikiangaliwa kwa ukaribu sana, maana ndizo zinazoliwa kwa wingi ukilinganisha na bidhaa zingine.
 
Mkulima hauzi na kufaidika yeye. Kuna watu hapo katikati ndiyo manufaa yote yanaenda kwao.
Hao wapo lakini pia soko lililo la wazi msimu huu lilikuwepo na Bei nzuri ambapo mkulima alipata nafasi ya kuuza mazao yake bila kumtumia au kupitia kwa mtu yeyote yule
 
Nyie ndo mnafanya tununue unga kg 2000tsh....
 
Nyie ndo mnafanya tununue unga kg 2000tsh....
Tanzania imebarikiwa kuwa na ardhi kubwa Sana yenye rutuba , hivyo hujachelewa chukua hatua nenda ushike ujembe utavuna na kupata chakula Cha kutosha mwaka mzima
 
Anayelalamika aende akalime, aende akashike jembe alone, kilimo Ni biashara hivyo haiwezekani kila siku wakulima wawe wakupata hasara
Kweli kabisa wasilalamike. Mimi napendekeza kilo ya unga ifike hadi 10,000/= ili kila mmoja akalime huko!
 
Mkuu, anayefaidika na mazao yake kuuzwa nje ni wale wanaojiita madalali. Mkulima hana chake katika biashara hiyo.
Na ili mkulima afaidike 100% zoezi linatakiwa kuwa endelevu. Bashe anatakiwa kutorudi nyuma kwenye hili. Akisikiliza kelele tu ameharibu. Bora ajiuzulu kuliko kuachana na huu msimamo.
 
Mkulima hauzi na kufaidika yeye. Kuna watu hapo katikati ndiyo manufaa yote yanaenda kwao.
Amekubaliana nao kwa hiyari yake. Na zoezi la kuacha mipaka wazi likiwa endelevu mkulima atafaidika kwa asilimia. Leo funga kesho fungua ni kukaribisha njaa na kuharibu kilimo.
 
Kwenye hili hata mm nampa rais Samia 100%. Ni uwendawazimu kumpangia mkulima wapi pa kuuza na namna ya kuuza mazao yake ili kuwanusuru wadangaji, machawa, wacheza pool, bodaboda, mama ntilie, machinga na madalali wa viwanja eti wasife kwa njaa.

Yaani nguvu kazi ya taifa inafanya kazi za kidwanzi kama hizo inaacha kwenda kulima??

Kama kuna "kima" yeyote anayeona mazao yako bei juu aende mashambani akalime mazao yake
Mkuu kwa taarifa nilizo nazo toka kwa mfanyabiashara ni kwamba serikali imezuia kuuza chakula nje ya nchi baada ya bei za chakuka kuwa juu nchini.
Mleta mada anasifia kitu asichojua huku anaponda kitu inachofanya serikali bila kujua.
Katazo ni la kimya kimya.
CC: Lucas mwashambwa
 
Back
Top Bottom