Nampongeza Rais Samia kwa kusimama na wakulima kwa kuwaruhusu kuuza mahali popote palipo na Bei nzuri

Nampongeza Rais Samia kwa kusimama na wakulima kwa kuwaruhusu kuuza mahali popote palipo na Bei nzuri

Mkuu kwa taarifa nilizo nazo toka kwa mfanyabiashara ni kwamba serikali imezuia kuuza chakula nje ya nchi baada ya bei za chakuka kuwa juu nchini.
Mleta mada anasifia kitu asichojua huku anaponda kitu inachofanya serikali bila kujua.
Katazo ni la kimya kimya.
CC: Lucas mwashambwa
Hakuna wew chakula kilichozuiwa
Njoo Namanga uone jinsi malory yanavyopita na mahindi yake na mipunga

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Hujalamba uenezi wa mkoa Lucas. Basi hata ujumbe wa bodi ya maziwa na wewe ufuatwe na V8 siku za vikao na posho

Sent from my Infinix X605 using JamiiForums mobile app
Mimi namuunga mkono mh Rais wangu kwa kubeba jembe kwenda shambani ili nyie wamjini mpate chakula na Taifa letu liwe salama kwa kuhakikisha chakula kinakuwepo Cha kutosha nchini kupitia mikono yetu na nguvu zetu
 
Wanao sema eti watakufa njaa nawashangaa, wanamawazo mafupi sana nchi zenye majangwa, lini walikufa njaa.
 
Wewe ni chawa usie kuwa na connection unakaza mishipa yako utatulia

Mimi namuunga mkono mh Rais wangu kwa kubeba jembe kwenda shambani ili nyie wamjini mpate chakula na Taifa letu liwe salama kwa kuhakikisha chakula kinakuwepo Cha kutosha nchini kupitia mikono yetu na nguvu zetu
 
Ndugu zangu Sote tunafahamu kuwa secta ya kilimo katika nchi hii imeajiri na kubeba kundi kubwa Sana la watanzania, Ni secta ambayo ndio pumzi ya familia na Kaya nyingi, Ni secta inayotegemewa na watanzania wengi Kama shughuli kuu ya kiuchumi, Ni kimbilio la wengi, Ni ngazi ya wengi, Ni njia ipitayo na kupitisha watu wengi Sana kuinuka kiuchumi, kilimo Ni mgongo uliowabeba watu wengi Sana katika nchi hii, Ni ziwa ambalo kila mtanzania ananyonya , kilimo ni Mbeleko iliyowabeba wengi Sana,Kilimo Ni MAMA Mlezi wa Taifa hili,

Hivyo ukikipuuza kilimo Ni sawa na kuwa umewapuuza watanzania, ukikiacha kilimo Ni sawa na kuwa umewaacha watanzania wanyonge nyuma, ukikinyonya kilimo kibajeti Ni sawa na kuwa umewanyonya watanzania na ukikibana kilimo Koo Ni sawa na kuwa umewabana watanzania Koo na kuwanyima puumzi.

Sote Ni mashahidi namna ambavyo wakulima wa nchi hii kwa miaka mingi tu ambavyo wamekuwa wakipata hasara kubwa licha ya kuwa wamekuwa wakihenyeka na kuvuja jasho mwaka Hadi mwaka, lakini maisha ya mkulima yamekuwa yakibaki na kuwa duni tu kila siku, hii nikutokana na Bei mbaya ambayo mkulima amekuwa akiuza na kuipata, mkulima licha ya kutumia gharama kubwa katika uzalishaji lakini amekuwa akipangiwa Bei ya kuuza na mahali pa kuuza, amekuwa akipewa mashariti ya kwamba hutakiwi kuuza kule na kule na utauza hapa nchini pekee na mipaka ikawa inafungwa,

Hivyo mkulima amekuwa kwa miaka mingi akibeba misalaba ya watanzania wote, licha ya kulilisha Taifa hili lakini mkulima huyu amekuwa akibaki fukara Sana kwa kuwa Hana uamuzi katika kujitafutia na kuuza mahali ambapo soko Ni zuri na Bei ni ya uhakika,

Rais Samia alipoingia na kuapishwa kuwa Mkuu Wa nchi na Amiri Jeshi mkuu amekuja na mtizamo tofauti wa kukifanya kilimo Ni biashara ,hivyo biashara yoyote lazima itoe faida na itafutiwe soko zuri lakini pia kuwe na mipango mizuri yakuifanya biashara inawiri na kushamiri, mh Rais Samia amekataa kufunga mipaka kuzuia mahindi yasiuzwe nje ya nchi, Jambo lililopelekea mkulima kuuza Bei nzuri Sana mwaka huu tangia wakati wa mavuno,, huku mh Rais akihakikisha kuwa chakula kinakuwepo nchini Cha kutosha kwa usalama wetu

Sasa wakulima wanafaidi jasho lao, wanafaidika na juhudi zao, Sasa vijana wanahamasika kujiingiza katika kilimo, Sasa uzalishaji wa kilimo unaongezeka kwa kila mtu , Sasa watu wanaitafuta Aridhi ili walime maana Sasa kilimo kinalipa na hakimtupu mtu, Sasa kilimo kinakwenda kuwa kimbilio lenye matumaini kwetu vijana, Sasa kilimo kinatoa nuru ya kuinuka kiuchumi, Sasa kilimo kinarudi katika mioyo ya watanzania waliokuwa wameanza kukata tamaaa baada ya kuwa wahanga wakupata hasara kila mwaka,

Nataka niwaulize mnaolalamika uamuzi wa mh Rais wetu mpendwa kutofunga mipaka, Hivi mnajuwa adha za kilimo? Hivi mnajuwa gharama za kilimo nyie? Hivi mnajuwa misukosuko ya kilimo nyie? Hivi mnajuwa ugumu wa jembe nyie? Mmewahi kulima? Mmewahi kushika jembe nyie? Mnajuwa hata namna ya kushika mpini wa jembe au jembe la kukokota na ng'ombe? Mnajuwa mkulima anaamka saa ngapi na kulala muda upi? Mnajuwa mwili wa mkulima unapata maumivu kiasi gani? Au kwa kuwa mnaona vitu vikija sokoni tu? Jembe Ni Vita inayohitaji kujitoa kujitolea na kuwa mvumilivu Kama Asikari Jeshi aliye vitani kupigania nchi yake, mkulima amechoka kupata hasara kila mwaka

Muwe na huruma na mkulima jamani, jaribuni kuvaa viatu vya mkulima muone Kama vitawatosha, vitawashinda kwa uzito na ukubwa wake, lazima vitawapwaya na mtavivua tu, Kama mnaona mkulima hastahili kufaidika na jasho lake Basi nendeni nanyi mkalime, nendeni mkashike jembe, msikae tu kunyonya jasho la mkulima huku mkiwa kimvulini

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Wanaouza kwa taarifa yako ni wafanyabiashara,wakulima waliuzia mazao yao shambani kitambo sana,
 
Chakula cha kutosha kwa muda gani?!

Na huko kutosha kwake kumezingatia affordability?! Kama nilivyosema, kuna globe food crisis... je, hicho chakula cha kutosha kimezingatia hayo?!
Kipo na Affordable kwa walio wengi labda wale wavivu wanaotaka kupiga alaf wale washibe. Aridhi bado ni kubwa tunataka watu wajiaali kwenye kilimo na bei nzuri ni kivutio kikubwa. Mlikuwa mnacheka humu tulipkosa soko la mahindi yetu Songea, nyanya ilula na mbaazi
 
Wanaouza kwa taarifa yako ni wafanyabiashara,wakulima waliuzia mazao yao shambani kitambo sana,
Nakwambia hivi mwaka huu Bei ya mazao ilikuwa Ni nzuri Tangia wakati wa mavuno hivyo mkulima alipata nafasi ya kuuza kwa Bei nzuri tu, lakini pia siyo wakulima wote wanaouzia mashambani Kama unavyofikiri wewe
 
Wanao sema eti watakufa njaa nawashangaa, wanamawazo mafupi sana nchi zenye majangwa, lini walikufa njaa.
Kama wanajuwa huwa Kuna kuwa na njaa Basi niwakati wao wakwenda kushika jembe na kulima maana Tanzania tumejaliwa kuwa na ardhi yakutosha Tena yenye rutuba nzuri kabisa
 
Kwenye hili hata mm nampa rais Samia 100%. Ni uwendawazimu kumpangia mkulima wapi pa kuuza na namna ya kuuza mazao yake ili kuwanusuru wadangaji, machawa, wacheza pool, bodaboda, mama ntilie, machinga na madalali wa viwanja eti wasife kwa njaa.

Yaani nguvu kazi ya taifa inafanya kazi za kidwanzi kama hizo inaacha kwenda kulima??

Kama kuna "kima" yeyote anayeona mazao yako bei juu aende mashambani akalime mazao yake
Mkuu hongera kwa post hii. Huo ndiyo ukweli mchungu
 
Back
Top Bottom