Nampongeza Rais Samia kwa kusimama na wakulima kwa kuwaruhusu kuuza mahali popote palipo na Bei nzuri

Pm nikupe namba za wakubwa uache kujiabisha
Kazi yangu nikuyasema mazuri yote nayoyaona katika uongozi huu wa mh Rais Samia na serikali yake, Kama kuusema ukweli na mafanikio ya serikali hii Ni kujiaibisha Basi niache Niendelee kuaibika kwa kusema ukweli wa mafanikio ya serikali ,
 
Ameruhusu Rais au sheria?

Tuanze hapo ili wenye akili tuelewe
 
Unfortunately uhakika mkulima anapata hiyo bei? Au ndo nyie madalali mnatajirika hamjui hata shamba likoje.wafanyabiashara wa nje wasiruhusiwe kwenda vijijini wanununue katika masoko yetu mjini au wilayani na tuhakikishe tunaondoa madalali
 
Unfortunately uhakika mkulima anapata hiyo bei? Au ndo nyie madalali mnatajirika hamjui hata shamba likoje.wafanyabiashara wa nje wasiruhusiwe kwenda vijijini wanununue katika masoko yetu mjini au wilayani na tuhakikishe tunaondoa madalali
Wakulima wengi kwa mwaka huu uliopita waliuza mazao yao kupitia madalali , hata kama bei zilichangamka wengi hawakupata kilichostahili.
Kwa miaka inayokuja sidhani kama kuna mkulima atauza mazao kupitia madalali maana masoko yote wanakouzia hao madalali yanajulikana na bei pia zinajulikana.
 
Hayo ni mapungufu endelevu.
Lazima ujuwe pia kupata soko na kupenya katika soko la mwenzio yaana nchi jirani au ya kigeni inahitaji maelewano mazuri ushirikiano mzuri na ushawishi wa kidiplomasia, kwa hiyo lazima mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani apongezwe Sana kwa namna alivyojenga na kuimarisha ujirani mwema kupitia diplomasia yetu na ushirikiano wetu ambapo Sasa tunaishi Kama ndugu wa karibu, hii ndio sababu inayotusaidia kupata fursa mbalimbali zikiwemo hizi za masoko ya mazao nje ya nchi
 
Mkuu
Ninaongelea utaratibu unaoruhusiwa. Ni fungate au sheria imepitishwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…