Namshangaa sana mtu anayeishabikia CCM

Umaskini haujaletwa na CCM ingekuwa hivyo Mbowe ,Mengi na akina Bakhresa no wasingekuwa mabilionea

Matatizo yako usisukumie C CM sukumia ukoo wako na wewe binafsi kwa kulala fofofo wakati fursa ziko kibao
Hao kina bakhresa wako wangapi na wale wa kukopa songesha wakashindwa kurejesha wako wangapi?.
 
Kwa hiyo natakiwa nijenge kituo bora cha afya cha kwangu ili wazazi na watoto wachanga wasifariki kwa kukosa huduma ya afya? Kwa hiyo natakiwa nijitafutie chanzo cha maji safi na salama cha kwangu? Basi sawa nimekuelewa.
Kuna bima ya afya wewe ya kujitibu wewe na ukoo wako hata hela za bima ya afya tu hamna ukoo na familia yako choka mbaya!! So lazima mjenge kituo Cha afya kakateno bima ya afya Kama hamuwezi ulofa wenu msisukumie CCM

familia na Koo za wenye nazo huungana kuchimba visima kwa matumizu yao na hata kuuzia wengine

Wewe unatakiwa uitishe kikao Cha ukoo mchapane viboko kuwa maji ardhini yako kibao tunashindwa Nini Kama ukoo kuchimba kwa matumizi yetu?

Mnashindwa hata kuchimba kisima au Bwawa mdake maji ya mvua ? Look.Huko kwenu sio kwa kuoa Wala kuolewa ni kuchovu mno


Pia tandikaneni viboko kuwa inakuwaje ukoo mzima tunashindwa kununua bima ya afya ili kila mwanaukoo akipata shida anatibiwa hospitali za kueleweka?

Narudia Tena umaskini wako na familia yako na ukoo wako ukome kuisukumia CCM.
 
Kibaya machoni pako si lazima kiwe kibaya machoni pa mwingine and vise versa.
 
Aliyekwambia hii nchi haitakuja kutwangana ni nani?.Tumechelewa tu kwa vile watu wameridhika kwasababu tuna bahati ya kua na chakula chakutosha.ila haki ndio msingi wa nchi kua pamoja na hilo likikosekana tegemea lolote.hayo mambo ya majimbo ni visingizio tu unaleta.
 
Huwa najiuliza inawezekana vipi mtu ukashabikia Chadema
 
Ccm Katu haiwezi waletea maendeleo watz.Ccm na umasikini ni damu damu.rejea maagano ya ccm na shetani mapangoni bagamoyo ukazaliwa mwenge moto wa kichawi unaozunguka nchi kuwaroga watz Ili watawalike.
Ukiondoa umasikini na ccm itakufa.Case study ccm inakubalika Sana maeneo masikini.
 
Tozo nasimama na wananchi .Hakuna serikali hundred percent perfect duniani kupandisha miamala wamechemka Hakuna mwananchi alipendekeza Ni Zungu na matatizo yake
Acha ujinga Mpwa,, Zungu ndio bunge? Tuweni wakweli Ndugu zangu, tuna bunge la kipuuzi sana
 
Corona ipo Moshi na Arusha kwa sababu ya laana ya kushangilia kifo cha Magufuli
 
Nashukuru unanisaidia kushangaa na Mimi. Chama kinachouwa na kuteka watu kubambikia kesi kufukarisha watu makusudi kwa kubambikia watu kesi wanakipendea nini? Chama kinachoiba uchaguzi kwa asilimia Mia halafu watu wakihoji katiba mpya kinafunga watu midomo wasihoji kwa kisingizio tunajenga nchi mpaka uchaguzi mwingine.
 
Vyama vya Upinzani nchini Tanzania vimefanya nini cha maana ili tushawishike kuachana na CCM ili tuvishabikie vyenyewe kama ambavyo unahangaika Kutulazimisha hapa?

Ni kweli CCM kunaweza kuwa na Changamoto hasa kutokana na Ukongwe wake ila kwa Wapinzani wao hata bado hawajapewa Dhamana ya Kutuongoza Watanzania wameshaanza kutuonyesha Nyufa zao nyingi za Kimsingi ambazo kama wakipewa nchi wanaweza Kuharibu zaidi.

Ni Udhaifu mkubwa uliopo Upinzani ndiyo unaoifanya CCM ambayo inajua Kujisahihisha na Kujipambanua vyema kwa Wananchi wake izidi si tu Kukubalika na Kuaminika kwa Ustawi mzima wa Watanzania na Taifa zima la Tanzania.
 
Inakuaje mtu una shabikia chama cha siasa kama unavyo shabikia timu za mpira, akina sepetu ,akina rafiki nk?!?! Watanzania ni watu wa ajabu sana!
 
Unaposema wananchi hawafaidi matunda ya uhuru isipokuwa viongozi na familia zao umesahau kuwa kabla ya uhuru wananchi haohao walikosa haya yafuatayo:

1)Kuishi baadhi ya maeneo ya nchi yao.....mfano kule KICHANGA CHUI(MASAKI YA LEO)...daraja la selander lilikuwa mpaka wao na watu weupe.

2)Wananchi haohao hawakuwa na ACCESS ya kupata huduma za afya....hospitali zilikuwa kwa ajili ya weupe tu....mpaka akajitokeza "TAJIRI MMOJA MZALENDO...tajiri huyu mwenye asili ya kihindi akafungua ZAHANATI kwa ajili ya wazawa pale ilipo STESHENI POSTA.....
Baadaye akaja ndugu SEWA HAJI na kuendelea kutoa nafasi ya kutibiwa wazawa......

Je hospitali ,vituo vya afya na zahanati zilizoko SASA ZINAFANANA na zilizokuwa kipindi cha AWAMU YA KWANZA?je hakuna hatua za MAENDELEO makubwa kufikia sasa ?!!

3)Mkoloni aliacha barabara moja tu.....mikoa haijaunganishwa?!! Si faida kwetu wananchi wa kawaida?!!!

4)Baba zetu walikula UNGA WA YANGA na kuvaa ndala ,je Leo hakuna mabadiliko?!!

5)Mkoloni hakuacha CHUO KIKUU hata kimoja....Uganda alikijenga.......je leo hatuna vyuo vikuu mpaka "vichochoroni"?!!
 
Zero brain. No wonder why CCM is loved by ignorant people. Kazi ya serikali ni nini sasa?
 
Mnawaibia kura kwa nguvu ya dola Kama mnajiamini mnapendwa Sana na watanzania na Kama mnajiamini mna clean sheets kwenye ustawi wa taifa hili viambieni vyombo vya dola vikae pembeni na kuwe na tume huru ya uchaguzi plus katiba mpya mkishinda hata kata moja kwa haki nchi nzima achiliambali udiwani na urais nyie vidume.
 
Kujisahihisha? Give me a break. Wapi CCM imejisahihisha? Tuonyeshe matunda ya kujisahihisha. Au tuonyeshe nchi ilikuwaje kabla na baada ya ccm kujisahihisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…